Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,894
kufuatia njaa iliyokithiri somalia (haijawahi kutokea ndani ya miaka 60) Tanzania imeahidi kuisaidia Somalia tani 300 za mahindi. Huu ni moyo wa utoaji
na hakika likiwa limefanyika kwa moyo basi Mungu ataibariki Tanzania mara dufu.
Lakini kuna jambo moja tuu linanishangaza, hivi ni kweli Tanzania inawapenda watu wake? Leo bungeni nimewasikia wabunge kama watatu
wanalalamika majimboni kwao kuna njaa kali na chakula walichoahidiwa (iwe cha bure/au cha gharama nafuu/gharama halisi) hakijapelekwa zaidi ya
miezi miwili sasa. Huu ndo mwendelezo tabia ya kujali watu wa nje kuliko wazawa? Sipingi kusaidiwa kwa somalia, maana hakika tunapaswa kufanya
hivyo lakini maneno matakatifu yanasema mtu asiyewajali watu wa nyumbani mwake ameikana imani, ni mbaya kuliko asiye amini! Nawasilisha
Kuwajali watuj wa Nje ni kawaida ya JK maana amekuwa waziri wa mambo ya nje muda wote au mmesahau ? Pia kumbuka JK ni mpenda sifa sana mie sishangai kuwapa chakula hicho kama alidiriki kuongopa mchana kweupe kwa ma CCM wenzake tena Darisalama juu ya barabara za juu kwa juu unategemea nini ?