Tanzania yatoa chipukizi kucheza soka ya kulipwa Ulaya

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Date::11/2/2008
Tanzania yatoa chipukizi kucheza soka ya kulipwa Ulaya

Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

HATIMAYE Tanzania imetoa nyota watatu wa mpango wa Vodacom Global Soccer Star (VGSS) ambao wataondoka karibuni kwenda Ulaya kujiunga na mpira wa kulipwa.

Nyota hao, Cosmas Mwazembe, Francis Casto (Mbeya) ambao watajiunga na timu ya Reading FC ya Uingereza inayocheza Ligi Daraja la Kwanza baada ya msimu uliopita kushuka daraja kutoka ile ya Barclays Premier League wakati Salum Saad (Zanzibar) atajiunga na shule maalum ya michezo iliyopo Marbella Hispania .

Mdau maarufu wa michezo nchini, Kanali Iddi Kipingu, mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuwatangaza nyota hao aliipongeza Kampuni ya Vodacom kwa kudhamini mpango huo.

Alisema Tanzania inapiga hatua kubwa kwa upande wa michezo kwani kwa mara ya kwanza inakuwa na wachezaji wa kulipwa katika ligi kubwa na maarufu duniani, yaani Uingereza.

Alisema wachezaji hao pia wataimarisha timu ya taifa ya Tanzania (Stars) kwa siku za usoni na kuomba wadau wengine wa michezo wajiingizie katika mchakato kutafuta na kuendeleza vipaji kwa vijana kwani ndiyo njia pekee ya kuifanya Tanzania isomeke katika ramani ya soka duniani.

Vijana hao wamepatikana kutokana na kura za Watanzania ambao walikuwa wakiwapigia kura vijana 35 waliokuwa kambini jijini Dar es Salaam kwa wiki tano na hatimaye wamepatika watatu.

Habari za ndani ya Vodacom Tanzania zinasema kwamba awali alitakiwa kijana mmoja tu kujiunga na timu ya Reading, lakini baada ya kuridhishwa na kiwango chao, timu hiyo iliomba ipatiwe wachezaji wawili.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraem Mafuru alisema kwamba zaidi ya vijana 11,000 kote nchini walipitia mchujo huo ambao umewezesha vijana watatu kuwa nyota.

Aliwapongeza vijana hao na kusema kwamba Vodacom Tanzania itanendelea kuwekeza katika soka.

Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga aliipongeza Vodacom kwa kuanzisha programu hiyo ya kusaka vipaji.

Alisema ni faraja kubwa kwa Tanzania kuanza kuwa na nyota wake Ulaya ambao wamekenda huko baada ya kuonyesha vipaji katika vya kusakata soka katika umri mdogo.

Mpango huo wa kusaka vipaji ulianza Mei mwaka huu na vituo vya kukusanyikia vijana viligawanywa katika kanda ambapo vijana wenye umri wa miaka kati ya 16 na 22 walikusanywa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya Zanzibar na Arusha.
 
Mwanzo mzuri sana nin imani hao vijana wakikaza msuli na kuwa kwenye first 11 katika hiyo timu watakuwa wamewafungulia njia wanasoka wetu. Jambo kubwa ninaloshauri hao vijana kwa kuwa bado wadogo wanahitajika kupata mafunzo ya lugha ili waweze kwenda sambasamba na maisha ya uingereza otherwise watarudia yaliyofanywa na Athumani China aliposhindwa kucheza soka Uingereza kwa kisingizio cha kuwa mpweke kumbe lugha nayo ilimfanya ajione mpweke zaidi kwani hakuweza ku-interact na watu wengine...
 
over-excited? We need TFF to show the WAY and not Vodacom or any other private sponsors! Sports (any) development should undertaken by the government (TFF) and invite the sponsors to support the initiative, but not other way around!
 
over-excited? We need TFF to show the WAY and not Vodacom or any other private sponsors! Sports (any) development should undertaken by the government (TFF) and invite the sponsors to support the initiative, but not other way around!

Baba Enock

Taratibu ndugu yangu... cha maana kuna bangusilo ameonyesha njia, tukikaa tusubiri TFF, tutaishia kunawa.

Hiyo ya kila kitu kianzie serikali kama kinanitisha kidogo, ndio future hiyo au past?

Mt
 
Baba Enock

Taratibu ndugu yangu... cha maana kuna bangusilo ameonyesha njia, tukikaa tusubiri TFF, tutaishia kunawa.

Hiyo ya kila kitu kianzie serikali kama kinanitisha kidogo, ndio future hiyo au past?

Mt
Ni kweli MTM ukitaka kusubiri kila kitu serikali wakati mwingine unaweza kuja kushangaa wenzako wamevuka mto we unashangaa tu so mi nawapa Big up sana vodacom kwa hili wala halina ubaya wowote...
 
Back
Top Bottom