Tanzania yasaini kupokea Bilioni 352/- (EURO 176) kutoka Ujerumani

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]04/10/2012
0 Comments

201719633.jpg
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Kluas Peter Brandes (kulia) wakisaini mkataba wa msaada wa miaka mitatu leo mjini Dar es Salaam ambapo Ujerumani itaipatia Tanzania msaada wa Shilingi bilioni 352. Msaada huo utasaidia kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, mfuko wa bajeti ya Serikali na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma.

Habari imeandikwa na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar Salaam --- Ujerumani imetoa jumla ya shilingi bilioni 352( euro milioni 176) kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kipindi miaka mitatu ijayo.

Makubaliano ya msaada huo yamesaini leo jijini na Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa kwa upande wa Tanzania na Balozi wa Ujerumani nchini Kluas Peter Brandes.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo kwa niaba ya Tanzania Waziri wa Fedha dr. Mgimwa alisema kuwa fedha hizo zitasaidia shughuli mbali za maendeleo katika kipindi cha mwaka 2012/13- hadi 2014/15.

Alisema kuwa msaada huo unalenga maeneo ya kuboresha utawala bora katika serikali za mitaa, kusaidia sekta ya afya , nishati , maliasili, maji, na kuboresha programu ya usimamizi wa fedha za umma.

Dr. Mgimwa aliongeza kuwa eneo jingine ambapo hizo zitaelekezwa ni pamoja na kusaidia mfuko wa bajeti kwa kipindi miaka mitatu hiyo na kusaidia ofisi ya Taifa ya Mkaguzi wa hesabu za serikali .

Alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA) na hivyo kuboresha hali ya uchumi na kijamii ya wananchi.

Aidha Waziri huyo wa Fedha alimuhakikisha Balozi wa Ujerumani nchini kuwa , Serikali itahakikisha fedha za msaada zinatuma katika maeneo yalipangwa kwa manufaa ya wananchi ili matokeo yake yaweze kuonyesha thamani ya fedha waliyotoa.

Naye Balozi Brandes alisema kuwa Nchi yake itaendelea kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania ili kufikia malengo ya kupambana na umaskini na hivyo kuboresha maisha ya Watanzania hasa waishio vijijini.

Aliongeza kuwa msaada waliotoa utasaidia wakazi wa mijini kupata maji safi na salama kwa ajili ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na maji yasiyo salama.

431042703.jpg
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa (kushoto) na Balozi wa Ujerumani nchini Klaus Peter Brandes (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya mkataba wa msaada wa miaka mitatu leo mjini Dar es Salaam.

Source:
http://www.wavuti.com/#ixzz28LVJk4xJ
 
Hizo pesa zinaenda kwenye MIRADI MINGI... UDOKOZI KIBAO
 
Kila mwaka wafadhili wanatumbukiza fedha kwenye shimo liitwalo Tanzania wakijua fika limejaa panya na viwavi. Hawa nao siwaelewi. Wanachangia maendeleo au maanguko ya taifa kwa kununepesha mapanya yetu? Baada ya miaka tutaangamiza vizazi vijavyo kwa misaada hii ambayo imegeuka nyenzo mpya ya ukoloni mamboleo.
 
Aisee umeongea vema. naendelea kupata uhakika kuwa watanzania akili zetu sawa na nyani. ukisoma kitabu cha Dambisa Moyo kiitwacho dead aid utagundua ninachosema. sijui nitumie lugha gani ili nieleweke. sirikali inashindwa kujenga uwezo, miaka 50 baada ya uhuru, bado inaomba misaada. hizi pesa matumizi yake ni pamoja na kuendeleza ukandamizaji dhidi ya wananchi, kupalilia rushwa na kuwafanya wananchi kuwa mabuda.
 
These beparis are not as stupid as how some of our leaders are. Wanajua fika kuwa watawabania hapa na pale na mwisho wa siku hizo pesa zinarudi ikibidi hata mara mbili yake.
 
Hakuna atakaye toa asijue anapata nini in return,
Wanajua tutawapa/ walishachukua nini kwa hiyo so called MISAADA yao. Taifa langu Tukufu Tanzania.
 
Back
Top Bottom