Tanzania yapoteza bilioni 478 kwa utoroshaji wa fedha nje

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
mpinaa.jpg

Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina


Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina, amesema kuwa Tanzania imekuwa ikipoteza Sh. bilioni 478 kutokana na utoroshaji wa fedha haramu kila mwaka.

Mpina aliyasema hayo, jana wakati akichangia makadirio ya matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha kwa mwaka 2012/13 katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tume ya Mipango iliyowasilishwa bungeni juzi.

Alisema ripoti ya dunia ya maadili (GFI), ya mwaka 2008 ambayo ilikuwa na kichwa cha habari, Fedha zinazotoroshwa Afrika” na raslimali za maendeleo zinazofichwa inaonyesha kuwa kwa miaka 39 (1977-2008), Tanzania ni nchi ya 13 kati ya nchi 20 zinazoongoza kwa utoroshaji wa fedha za umma na kuficha nje ya nchi.

“Katika kipindi hicho Tanzania imepoteza sh trilioni 11.6 ambazo zimefichwa nje ya nchi na wafanyabiashara na watendaji wa serikali,”alisema.

Alisema hayo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Ndikumana na Boyce katika mwaka 2008 na kwamba huo unafanana na utafiti uliofanywa na GFI.

Alisema katika taarifa ya Waziri haijaonyesha kushtushwa na taarifa hizo kwani hakuna mahali popote ambapo anaelezea wala kuainisha hatua zozote zitakazochukuliwa juu ya wizi huo wa fedha za umma uliofanyika mpaka sasa.

Alisema hakuna mkakati ambao seriklali imeweka kubaini na kuujulisha umma na Bunge juu ya watu wanaohusika na utoroshaji huo wa fedha za umma.

Alisema benki kuu wanajua akaunti zote na fedha ambazo watanzania wanamiliki katika mabenki nje ya nchi iweje leo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), hawajatoa taarifa yoyote inaleta mashaka kwa chombo hicho muhimu.




CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom