Tanzania yapewa angalizo kuhusu EPA

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
Kikundi cha mazungumzo cha Umoja wa Makanisa Tanzania kinachoundwa na Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikiristo Tanzania (CCT), kimeishauri Serikali kutotia saini makubaliano ya Mkataba ya ubia wa Uchumi (EPA) kati ya Jumuia ya Afrika Mashariki EAC Tanzania na Jumuiya ya Ulaya (EU).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mratibu kikundi hicho Jesca Mkuchu, alisema wanapongeza juhudi za serikali za kuweka mbele maslahi ya wananchi wa Tanzania katika mkataba wa ubia huo.

Mkuchu alisema kuwa kikundi chao kinaishauri serikali kuboresha ushiriki wa wananchi wa Tanzania kwa ujumla katika mchakato wa majadiliano ya mkataba wa ubia wa uchumi na pia kuongeza uwazi wa majadiiano na kuwa na uwakilishi mpana wa raia wa Tanzania.

Aliongeza kuwa Serikali inapaswa kuelimisha umma juu ya masuala ambayo hayaeleweki vizuri kwa umma wa Tanzania yanayohusu mkataba huo na athari zake pamoja na kuweka majadiliano ya ubia huo yanayozingatia ustawi wa wananchi, wakiwemo wakulima wadogowadogo, wavuvi na wajasiriamali.

Alisema endapo serikali haitazingatia ushauri huo, wanahofia nchi kuingia katika mapungufu mbalimbali yakiwemo kukosekana kwa mapato kutokana na kodi ndogo za mapato ambapo kutapunguza kiasi cha fedha ambazo zingeweza kutumika katika kuwepo na uhakika wa chakula na kugharamia huduma nyingine za kijamii.

Mapungufu mengine ni uzalishaji wa ndani kutokuhimili ushindani wa bidhaa za vyakula vya kilimo zinazoingizwa kutoka EU.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom