Tanzania yaongozwa na Katiba ya CCM au Katiba ya nchi? Kikwete aiogopa CCM?

Kitu ambacho huwa kinanishangaza ni pale Nnape ama Salva anatoa tamko lenye mapungufu kwa niaba ya taasisi zao.
Hivi kweli vichwa vyote kwenye CC hawakuona tunachokiona?
Kama hawakuona basi ni dhahiri kwa nini kama taifa tupo mahali tulipo!
 
jk-mawazo.jpg

Ni jambo lililonishangaza Kikwete kuitisha kikao cha Chama kwa ajili ya kujadili na kuomba ridhaa yao kufanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri. Kwa hali ilivyo inaelekea hata yaliyotokea kwa akina Jairo na wengineo aliogopa kuchukua hatua kwa kuogopa chama chake.

Serikali huongozwa na katiba ya nchi si katiba ya Chama, sasa Rais anapoomba ridhaa ya chama kufanya mabadiliko serikalini ina maanisha nchi inaongozwa na katiba ya Chama badala ya Katiba ya nchi?

KAMA ULIFUATILIA MATANGAZO YA BUNGE TBC MHESHIMIWA ZITTO ALIVYOWASILISHA HOJA YA KUMPIGIA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI WAZIRI MKUU NILIMUONA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI MHESHIMIWA WEREMA AKITAFUTA KIFUNGU KWENYE KATIBA CHA KUANGALIA HILO JAMBO WATAKWEPA VIPI NA AKAMKABIDHI WAZIRI MKUU MHESHIMIWA PINDA NAE AKAKISOMA VIZURI AKAGUNDUA KWAMBA HAWAWEZI KUN'GOLEWA KWA HIYO KAMA RAISI AMEWASILISHA KATIKA CHAMA CHAKE NADHANI TUMWACHE AFANYE HATA KUTUMIA HIYO KATIBA YA CCM KWANI HATA AZIMIO LA ARUSHA LILIAFIKIWA KWENYE CHAMA NA LILIKUJA SAIDIA NCHI LEO TUSIONE TABU KUFANYA AZIMIO LA MAGOGONI PLOT NO 1 KWANI HII KATIBA YENYEWE NDO TUNALALAMIKA NIMBOVU INAWEZEKANA INA VIFUNGU VINAVYOWALINDA WEZI NA KUWAITA WALIOSTAAFU WALIOJIUZULU SASA INAWEZEKANA TUKAGUNDUA KATIBA HIHII IKAWA INA KIFUNGU KINACHORUHUSU WATU KUGOMA KUJIUZULU NA TUKAJA KUWA NA WAZIRI MKUU ALIYEGOMA KUJIUZULU NA AKAENDELEA KUFANYA HARAMBEE ZA KUCHANGISHA HATA MBOLEA AKAWA NA LIUJIKO TU HEBU TUONE LEO CCM NA FALSAFA YA KUVUA GAMBA ILIONEKANA INAWASHINDA TUJARIBU HILI AZIMIO LA MAGOGONI PLOT NAMBA MOJA.
 
Kitu ambacho huwa kinanishangaza ni pale Nnape ama Salva anatoa tamko lenye mapungufu kwa niaba ya taasisi zao.
Hivi kweli vichwa vyote kwenye CC hawakuona tunachokiona?
Kama hawakuona basi ni dhahiri kwa nini kama taifa tupo mahali tulipo!

Zaidi ya usemayo RealMan, bunge ndilo lenye kuchukua uwakilishi uliokamilika kitaifa, na ndio maana ni mhimili mmojawapo kati ya mihimili mitatu ya kuongoza nchi. Rais anapopata kigugumizi cha kutekeleza yale ambayo mhimili mmojawapo wa serikali ambao ni bunge na kuridhia kuamuliwa na Chama ni walakini mkubwa sana. Kuna siku mswada wa sheria ya nchi Rais Kikwete atahitaji uidhinishwe na chama chake wakati bunge ndilo lililotunga na kuridhia.
 
Jamaa kapoteza uelekeo na hajiamini tena hata kwa yale yaliyo ndani ya mamlaka yake.kweli moto wa chadema unaunguza mpaka mazima moto!
 
Mkuu Ribosome,
bado kitambo kidogo utaanza kumutukana mzazi wako. Inakuwaje waziwazi unasema nyerere hakufanya chochote. Je asingekuwa yeye hiyo CCM yako ingekuwepo au Tanzania ingekuwa kama hunayoiona leo. Au kwa kuwa hakumsapoti baba yako kuingia madarakani 1995. Hivi nyinyi magamba utawala wenu mumekopi wapi, watu msiojitambua kuwa ni akina nani munaamini ya leo tu ya kesho na vizazi vyenu mumesahau. Huwa mnakaa na kujua miaka hamsisni ijayo mali zenu za wizi zitakuwa wapi na vitukuu vyenu vitaisi vipi. Mnachimba madini ovyo mnaach mashimo nadhani mumeanza na uranium huku umeme hakuna mtaacha mionzi juu ya ardhi kama urithi kwa wanenu. Usimtetee mtu asiyejua kujiongoza maana mwisho wa siku watasema yeye ndie mdhaifu si chama. Chama kimeundwa na watu wala si mada watu wakiamua kufuata ideology nyingine basi ujue huna chako. Bado kitambo kidogo hamtaona huo utukufu wenu hakuna kijani wala njano itakayobaki maana mwatenda yale ambayo binadamu na Mungu hapendezwi. Kumbukeni ufalme wote usiotenda yaliyo kweli hufutwa.
 
Tanzania ya leo ndio aliyoiacha Nyerere? usitake nikucheke. Nyerere aliiacha nchi iko juu ya mawe, hakuna chakula, hakuna fedha, hakuna mafuta, benki kuu ameichoma moto, wizara ya mambo ya ndani ameichoma moto (kuficha madudu yake).

Na mijitu ilikuwa kila anachosema inajichekesha tu kama misukule.

Usitake tuseme hovyo humu. Kama huyajuwi kaa kimya, sidhani hata kama ulikuwepo, unahadisthiwa hadithi za uongo na wewe unakubali tu.
 
Mh.Rais amekua akivunja au kupangua baraza la mawaziri lakini hatukuwahi kusikia ya kua Mh.JK kupata ushauri kutoka kwa kamati kuu ya CCM,kwa hii imekaaje?Je Mh.Rais hawezi kuona madudu yanayotendeka katika serikali yake bali kwa msaada wa darubini ya kamati kuu ya CCM?Au ni geresha na njia ya kujinasua katika hali ngumu aibu kutokana na maovu ambayo yamefichuliwa na CHADEMA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Sasa wewe hukupendezewa?
 
Hali hii imetushangaza wengi kusikia amepata baraka za CC! Siku zote na inaeleweka hivyo kuwa, Rais ana teua na kupanga baraza lake la mawaziri kwa kadri atakavyo-ona inafaa. Sasa hii ya kwenda kuomba baraka za CC imekujaje. Hii ni ishara ya maji kuzidi unga. Mengi tutayasikia, CCM inakufa ndani kwa ndani!
 
Wabongo bana, nyie kila jambo lazima malalamiko.
 
jk-mawazo.jpg

Ni jambo lililonishangaza Kikwete kuitisha kikao cha Chama kwa ajili ya kujadili na kuomba ridhaa yao kufanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri. Kwa hali ilivyo inaelekea hata yaliyotokea kwa akina Jairo na wengineo aliogopa kuchukua hatua kwa kuogopa chama chake.

Serikali huongozwa na katiba ya nchi si katiba ya Chama, sasa Rais anapoomba ridhaa ya chama kufanya mabadiliko serikalini ina maanisha nchi inaongozwa na katiba ya Chama badala ya Katiba ya nchi?
Watanzania tumeshavuka enzi za chama kushika hatamu, hii ni era ya CONSTITUTION SUPREMACY Rais amepewa mamlaka na katiba na anavyombo vinavyomruhusu kuvitumia kufanya maamuzi ya taifa, ni fedheha kubwa sana kwa nchi yetu kuwa na rais asiyekuwa rais bali ni kibaraka wa chama tu, hii nchi haiongozwi na katiba ya ccm, wala CC ya ccm si chombo cha kikatiba kwenye nchi yetu, kinawezaje kukutana ikulu kikafanya maamuzi ya nchi? Nimeudhika kwa kitendo hiki!
 
Ndugu zangu, wadogo wangu, na wakubwa wangu, nianze kwa kukiri kwamba siijui sheria hatakidogo lakini hiki kitendo cha rais wetu kuomba ridhaa kwa kamati kuu ya chama kuvunja ama kutovunja baraza la mawaziri kimenishitua kidogo yaan sijui kama nisuala la kisheria au ndo mkuu amejichanganya? naomba kwa wote mnaoijua sheria mnisaidie kwa hili....nimtizao tu!
 
Huko ni kutapatapa kwao kuizima hoja ionekane ni ya chama chao sio kwamba imeasisiwa na CDM...ndio maana wanahaha kuibaka hiyo ajenda ya uwajibikaji!!kumbuka alishasema upepo.......(Rais wa matukio)na upepo..
JK ni rahisi wa matukio, kitu kingine asichopenda ni kuonekana yeye ndiye aliye watosa jamaa zake maana anajua wazi kuwa naye ni mwizi tu hivyo kama mawaziri wanathubutu kuvuana nguo hadharani anauhakika gani watamwacha. Tukumbuke kwenye NEC yao Nywele nyeupe alimwagia maji machafu. JK siku zote anaamini Watanzania ni walewale tu wasio na uelewa wa mambo, tena watu wa kutumika tu.
 
Atayaonaje ikiwa yeye ndiye manju jamani!!!!!!!
mh.rais amekua akivunja au kupangua baraza la mawaziri lakini hatukuwahi kusikia ya kua mh.jk kupata ushauri kutoka kwa kamati kuu ya ccm,kwa hii imekaaje?je mh.rais hawezi kuona madudu yanayotendeka katika serikali yake bali kwa msaada wa darubini ya kamati kuu ya ccm?au ni geresha na njia ya kujinasua katika hali ngumu aibu kutokana na maovu ambayo yamefichuliwa na chadema.mungu ibariki tanzania.
 
CCM bado wapo kwenye hangover ya utawala wa chama kimoja hata baada ya miaka 20 kupita tangu tuwe kwenye mfumo wa vyama vingi. Wanadhani mamlaka ya rais kufanya jambo lolote lazima yapate baraka za politburo kama vile tuko Cuba au Korea Kaskazini. Ni aibu sana
 
Hapo ni wazi Vasco da gama kachemka na kama ilikuwa ni Azimio la Kamati ya Bunge ingejadiliwa katika vikao vya kawaida vya CC.Wabunge wa ccm na kamati yao ni chombo cha kawaida tu kama ilivyo UVCCM au UWT na kama wana maazimio yao kwenye cc yanafuata utaratibu wa kawaida tu wa vikao.
 
Wee Jogoo, kawike kule acha utaahira wako hapa! Wabunge gani wa CCM waliotaka Mawaziri wajiuzulu zaidi ya wale watano? Hao wengine si waligoma kusaini, sasa ni wapi walipokuwa wakitaka mawaziri wang'oke? Au ni pale Pius Msekwa Hall ambako hata waandishi walizuiwa kufika? Hiyo taarifa ya hao wabunge iko wapi? Au umekosea ulikuwa unamaanisha wabunge wa CDM na wachache mashujaa kutoka Chama cha Magamba wakiongozwa na Deo?

Nijuavyo mimi, huwezi kujua ni lini JK ni Rais na wakati gani ni Mwenyekiti wa Magamba, labda mpaka pale anapojitokeza hadharani akiwa amevaa vitenge vya kijani! Ukiangalia kwa makini, vikao vyote vya juu vya Magamba utawakuta akina Pinda, Bilal na mawaziri karibu wote! Sasa huyu ****** wa Bwagaroho aliogopa nini kuitisha Baraza la Mawaziri au akakaa na "Majengo yaliyopinda" na "Bila Hili" wake wakapangua safu ya Cabinet? Huko kwenye CC alikuwa akimtaka nani ambaye angemshauri ndipo asikie, au Vuvuzela "Nepi"?
Ama kweli, ukicheka na nyani utavuna mabua. Magamba walicheka na JK sasa wanavuna Kejeli!
hivi mbona tunapenda kuchuja taarifa na kubaki na tunazozipenda? kilichofikishwa kwenye CC ni taarifa ya wabunge wa CCM iliyopendekeza mawaziri wajiuzulu. CC imebariki azimio hilo. simple & clear. hayo ya kuongoza kwa kutumia katiba ya ccm ni tafsiri potofu.
 
Back
Top Bottom