Tanzania yaongozwa na Katiba ya CCM au Katiba ya nchi? Kikwete aiogopa CCM?

hahaaa! hakunaga rais kama jeeikeii. mlishaambiwa na mwalim 1995, huyu ni muhuni. lkn kwa vile kumbukumbu zenyu ni fupi, mkamchaguwa. mtalijuwa jiji. siku nyongine msirudie kutuchagulia n@7! halafu mkaliita rais!!!

"chaguo la Mungu".

Huyo Nyerere unaemtaja ni kipi alichokifanya kikafanikiwa? Hakuna hata moja.
 
Mkulu aliwahi kusema uraisi wake hauna ubia lakini mawaziri wake wamegeuka vibaka wa pesa za umma sasa naona comfo ziro yaani kuwafukuza wezi hadi kamati kuu mbona simwelewi? Jamani nishaurini maana nimechanganyikiwa na huyu babariz
 
jk-mawazo.jpg

Ni jambo lililonishangaza Kikwete kuitisha kikao cha Chama kwa ajili ya kujadili na kuomba ridhaa yao kufanya mabadiliko ya baraza la Mawaziri. Kwa hali ilivyo inaelekea hata yaliyotokea kwa akina Jairo na wengineo aliogopa kuchukua hatua kwa kuogopa chama chake.

Serikali huongozwa na katiba ya nchi si katiba ya Chama, sasa Rais anapoomba ridhaa ya chama kufanya mabadiliko serikalini ina maanisha nchi inaongozwa na katiba ya Chama badala ya Katiba ya nchi?

Kinachoonekana ni kwamba "hang-over" ya mfumo wa chama kimoja bado haijaisha miongoni mwa wanaCCM. Chini ya mfumo huo chama kilishika hatamu za uongozi. Kinachoamuliwa na Kamati Kuu ya chama ndiyo ilikuwa kauli ya Serikali yaani "party supremacy".
Hata hivyo sio tatizo serikali kujadiliana na chama chake. Lakini kuna vituko viwili hapa kwetu!
Moja, Mwenyekiti wa mkutano wa Kamati Kuu ni rais! Kumbuka yeye pia ndio mwenyekiti wa chama! Sasa rais anajiagiza mwenyewe kupitia chama?
Pili, baada ya kikao Serikali ingetoa tamko sio chama. Kwani hapa Serikali ilienda kutaka ushauri tu kwa chama. Hivyo, nilitazamia chama kingekaa kimya na kuiacha Serikali itamke.Ilieweke wananchi wa TZ wamempa rais yeye binafsi na makamu wake ridhaa ya kuongoza taifa sio chama chake. Utakumbuka kwenye uchaguzi mkuu alichaguliwa mtu kuwa rais sio chama! Hayo mambo ya tiketi za vyama ni utaratibu tu wa chaguzi tulionao kwa sasa!
 
Mkulu aliwahi kusema uraisi wake hauna ubia lakini mawaziri wake wamegeuka vibaka wa pesa za umma sasa naona comfo ziro yaani kuwafukuza wezi hadi kamati kuu mbona simwelewi? Jamani nishaurini maana nimechanganyikiwa na huyu babariz

Ungeshauriwa kabla ya kumchagua. Wewe ulimchagua mcheza ngoma, rafiki yake Kanumba, mzee wa ma- trip; ulitegemea nini? Ukipanda mwembe usitegee kuvuna chungwa! Habari ndo hiyo.
 
Jamani, ange badilisha baraza la mawaziri bila kuitisha kikao cha cc angelikuwa anafata matakwa ya saini 74 za wabunge na wenzake wasinge muelewa. "Weak leader"

Ameharibu zaidi kuitisha kikao hicho cha chama kujadili mageuzi ndani ya baraza la mawaziri kwa kuwa ameshajifunga kwa chama kuchagua wale ambao chama kinataka wapewe uwaziri, maana yake hakuna jipa na tusishangae hali kujirudia kama si kuwa mbaya zaidi.

Waliongeza wizara ili wengi wawemo na hata kuongeza manaibu, matokeo yake hakuna anayeridhika na mbaya zaidi ameongeza chachu ya migongano zaidi. Hii hali kutulia si rahisi hadi people's power washike nchi kusafisha uchafu la sivyo nchi itasambaratika kivyake.
 
Kifupi Kikwete kadhihirisha uoga wa kuchukua mamuuzi magumu. Anatumia chamam chake kama 'ngao' ya kujikingia ili asilaumiwe na hao marafiki zake.
 
I would have loved this way!

Tamko la chama lingekuwa "Rais amekubali kuvunja baraza" na sio "CC imemkubalia Rais kuvunja baraza"

Logically and legally it makes no sense CC kufanya kazi ya Rais.

Kwa nini mnawapa nafasi wenye kutania kwamba wataalam waliweka nazi badala ya kichwa??
 
Mkulu aliwahi kusema uraisi wake hauna ubia lakini mawaziri wake wamegeuka vibaka wa pesa za umma sasa naona comfo ziro yaani kuwafukuza wezi hadi kamati kuu mbona simwelewi? Jamani nishaurini maana nimechanganyikiwa na huyu babariz

Inaonyesha hiyo kamati ina ubia na urais wake
 
:frusty: Naona kama wabunge wa CCM/CC waliahirisha tatizo. Fine, maana wamekumbuka shuka lkn wezi wapelekwe kortini. otherwise .......! Toka nianze kufatilia politics za kibongo sikumbuki ka Mzee Ruksa na chinga boy ka waliwahi kufanya consultation kwa CC kabla ya mabadiliko ya GVT. Nijuzeni JF!
 
Kinachoonekana ni kwamba "hang-over" ya mfumo wa chama kimoja bado haijaisha miongoni mwa wanaCCM. Chini ya mfumo huo chama kilishika hatamu za uongozi. Kinachoamuliwa na Kamati Kuu ya chama ndiyo ilikuwa kauli ya Serikali yaani "party supremacy".
Hata hivyo sio tatizo serikali kujadiliana na chama chake. Lakini kuna vituko viwili hapa kwetu!
Moja, Mwenyekiti wa mkutano wa Kamati Kuu ni rais! Kumbuka yeye pia ndio mwenyekiti wa chama! Sasa rais anajiagiza mwenyewe kupitia chama?
Pili, baada ya kikao Serikali ingetoa tamko sio chama. Kwani hapa Serikali ilienda kutaka ushauri tu kwa chama. Hivyo, nitazamia chama kingekaa kimya na kuiacha Serikali itamke.Ilieweke wananchi wa TZ wamempa rais yeye binafsi na makamu wake ridhaa ya kuongoza taifa sio chama chake.Utakumbuka kwenye uchaguzi mkuu alichaguliwa mtu kuwa rais sio chama! Hayo mambo ya tiketi za vyama ni utaratibu tu wa chaguzi tulionao kwa sasa!

Umechanganua vizuri sana YanguHaki@, ushauri ni kitu cha kawaida na ndio njia bora katika uongozi vinginevyo ukiwa isolated ni hatari katika uongozi na ukaonekana ni utawala wa imla. Binafsi sikutegemea Nape akiwa kiongozi wa chama cha siasa atoe kauli ya Serikakali kuridhia mapendekezo ya bunge ya kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri. Hali kadhalika kikao hicho cha chama kufanyika rasmi Ikulu na kutangazwa kwamba ni kikao cha chama wakati Ikulu ni ofisi kuu ya Serikali nchini, ni kwazo kubwa sana. Kuna njia nyingi ambazo angeweza kuomba ushauri kwa chama na ikawa ni mambo yake binafsi katika uongozi bila kuutangazia umma kwamba chama kimekaa kujadili namna ya kufanya na kutekeleza mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Jambo jingine ambalo limenikuna kicha ni YanguHaki@ unapobenua hali ya Rais akiwa ndiye mwenyekiti wa chama anapojiagiza kufanya utekelezaji katika serikali yake wakati jambo lipo ndani ya uwezo wake kikatiba, haona semina elekezi zimewachanganya hawa viongozi wetu, hii haija kaa sawa.

Tunapata maswali mengi yanayokanganya sana hapa, labwa wahusika na mambo ya utawala serikalini au baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wenye uelewa mpana wangejaribu kutufafanulia hapa.
 
Mchambuzi,
UInataka kunambia Nyerere alipokuwa akivunja baraza la mawaziri alifanya vikao vya chama na kushauriwa alivunje?.. sidhani mkuu wangu hili itabidi nilifanyie utafiti maana linaondoa maana ya katiba na mamlaka ya rais ikiwa chama ndicho kinaamua, Hivi unataka kunambia hata anapochagua mawaziri huwa kuna kikao cha chama kinachomchagulia mawaziri? maana kama wanaweza kuvunja basi wanaweza pia kumchagulia..

Hujui kuwa Nyerere alikuwa dikteta? hujui kuwa Nyerere hakuna hata moja lililofanikiwa katika maamuzi yake ya kidikteta?
 
I would have loved this way!

Tamko la chama lingekuwa "Rais amekubali kuvunja baraza" na sio "CC imemkubalia Rais kuvunja baraza"

Logically and legally it makes no sense CC kufanya kazi ya Rais.

Kwa nini mnawapa nafasi wenye kutania kwamba wataalam waliweka nazi badala ya kichwa??

Hilo tamko la chama lingeeleweka vema kama chama peke yao toka Lumumba wangekaa kikao na kutoa tamko kwa serikali kuwa wanaridhia ushauri wa bunge nisingeibua mashaka kwani ni jambo la kawaida na chama kina haki ya kushauri serikali wakati wo wote.

RealMan kama ulivyosema Kamati Kuu ya CCM kwenda Ikulu kufanya maamuzi ya serikali hapo no sence at all.
Kwa lugha rahisi Kikwete anaburuzwa na CCM katika kuongoza nchi bila kutumia utashi wake.
 
hivi mbona tunapenda kuchuja taarifa na kubaki na tunazozipenda? kilichofikishwa kwenye CC ni taarifa ya wabunge wa CCM iliyopendekeza mawaziri wajiuzulu. CC imebariki azimio hilo. simple & clear. hayo ya kuongoza kwa kutumia katiba ya ccm ni tafsiri potofu.
Mimi nafikiri hoja ya kuwawajibisha mawaziri na wengine pale bungeni iliibuliwa na Mh. Lissu kabla ya Mh. Zitto kupigilia msumari wa mwisho! Baadaye, kilifuatia kikao cha wabunge wa CCM kujadili mustakabali wao.
 
Jamani, ange badilisha baraza la mawaziri bila kuitisha kikao cha cc angelikuwa anafata matakwa ya saini 74 za wabunge na wenzake wasinge muelewa. "Weak leader"

Maana yake mwoga na hajiamini licha ya kuanikwa wozo wote ule bado ana kigugumizi cha kuchukua uamuzi
 
Inaonyesha hiyo kamati ina ubia na urais wake

Njia ya ulaji, maana kuingia Ikulu kumshauri rais kuna malipo ya dinari ambayo hayatoki chamani bali serikalini. Kama posho za vikao zingetoka chamani kikao kingefanyika Lumumba. Pale magogoni maji ya kunywa, juice na vitafunio ni kutoka pesa ya mvuja jasho.
 
Hilo tamko la chama lingeeleweka vema kama chama peke yao toka Lumumba wangekaa kikao na kutoa tamko kwa serikali kuwa wanaridhia ushauri wa bunge nisingeibua mashaka kwani ni jambo la kawaida na chama kina haki ya kushauri serikali wakati wo wote.

RealMan kama ulivyosema Kamati Kuu ya CCM kwenda Ikulu kufanya maamuzi ya serikali hapo no sence at all.
Kwa lugha rahisi Kikwete anaburuzwa na CCM katika kuongoza nchi bila kutumia utashi wake.

Na sheria hii uliileta wewe:

Sheria ya Ukaguzi wa Umma (The Public Audit Act, 2008) inatoa pia madaraka kwa Kamati za Bunge za Kiuchunguzi, kwa niaba ya Bunge zima, kujadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kisha Kamati hizo kutoa Taarifa zake Bungeni.

"38 (1) The Public Accounts Committee, Local Authority Accounts Committee, Parastatal Organisations Committee shall discuss the reports of the Controller and Auditor General after they have been tabled in the National Assembly.
(2) Upon the completion of hearing the Parliamentary Oversight Committees shall prepare and submit to the National Assembly reports which may include comments and recommendations.
 
Wanabodi, tunaendelea kutafiti, endapo Mkulu kuomba kibali/ruhusa/baraka/support etc. ya CC ili kufukuza kazi wateule wake kama amevunja ama hajavunja katiba ya nchi. Kitu ambacho tunajiuliza, alipokuwa anawateua aliomba kibali cha CC au walimpa ushauri? Lakini pia, alishawahi kusema uraisi wake hauna ushirika na mtu yeyote. Je, una ushirika na CC?

Ni kama hali fulani ya kukosa mwelekeo hivi. Inawezekana anajikuta kwenye hali ngumu hadi anashindwa amwite nani kumshauri. Tutaona mwisho wa hizi ngonjera.
 
1.jpg

Ukiziangalia sana picha hizi zinasononesha, zimejaa mashaka, wajumbe wanaonyesha nyuso za kumsuta mtu, hali ya kuchanganyikiwa si ya kubuni ila yajidhihirisha. Mungu atunusuru kama alivyowanusuru.

Waziri Mkuu Pinda anatoa maelelezo ya kilichojilia bungeni, Rais wa Zanzibar Shein ameinama akiwa katika fikra nzito, wajumbe wengine wakijaa mshangao, Kikwete haonyeshi kama kuna kipya. Ni tafsiri yangu tu.
 
Back
Top Bottom