Tanzania yaongozwa kwa remote ya kishirikina (uchawi)

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,826
966
Wadau hii ni kwa mujibu wa gazeti la mwananchi

Dar es Salaam. Maalim Hassan Hussein, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mtabiri maarufu nchini, marehemu Sheikh Yahya Hussein, ametabiri mambo 18 yatakayotokea mwakani, likiwamo la kufariki ghafla kwa kiongozi mmoja mzee ambaye yumo kwenye mbio za urais mwakani.

Hussein alisema jana kuwa kiongozi huyo atadondoka ghafla kwenye jukwaa na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.Akitangaza utabiri wa mwakani, alisema: “Kiongozi huyo atakufa wakati akipelekwa hospitalini.”

Alisema pia mwandishi mmoja mashuhuri nchini atakufa kifo chenye utata kitakachoitesa Serikali na familia yake katika kutafuta sababu za kifo chake.

Mtabiri huyo alisema nyota inaonyesha kwamba misiba miwili ya kitaifa itatokea mwakani.

Kuhusu uchaguzi wa kiti cha urais mwaka 2015, alisema kati ya kundi la vijana na wazee, nyota zinaonyesha kwamba watakaofaidika ni vijana.

“Lakini kuna wazee pia wanaoweza kufaidika, hawa ni wale wenye sura za ujana, yaani babyface au wenye kupenda mambo ya ujana na kushirikiana na vijana,” alisema.

Alisema ili Tanzania ilinde sifa ya kuwa nchi yenye amani na utulivu ni kuwa na Rais kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili au mwenye ndoa ya dini tofauti.

Alisema utabiri unaonyesha kuwa mwaka 2015 utatawaliwa na nyota yenye kupendelea vijana, hivyo ni vyema vyama vya siasa vikawasimamisha kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani.

Kuhusu mauaji, fujo na ghasia alisema vitatawala katika uchaguzi ujao na kwamba Serikali inatakiwa kuweka tahadhari kubwa.

Pia alitabiri viongozi wawili wa siasa na dini kukumbwa na kashfa ya ngono itakayowasababisha anguko la utumishi wa kutukuka na familia zao.

Alisema mwaka ujao utakuwa na mafuriko na dhoruba vitakavyosababisha madhara, hivyo tahadhari ichukuliwe kuanzia sasa.

Alisema kutakuwa na vifo vya ghafla vya wasanii, wanamichezo na watu maarufu kama ilivyokuwa mwaka 2014.
 
Mkuu ndiyo maana ndani ya Chama Chetu yupo mzee maarufu tunayemtegemea kwa ulinzi wa Chama na Nchi kwa ujumla! Huyu mzee almaarufu kama Ngombale Mwiru, sifa yake na vigezo vya kuendelewa kupewa wadhifa ni Uganga wa Kienyeji! Na Serikali inaogopa washirikina kupita maelezo! Tar 30 mwezi mmoja kuelekea uchaguzi mkuu waliondoa marufuku iliyokuwa imewekwa dhidi ya waganga wa jadi iliyokuwa imewekwa kwa minajili ya kulinda walemavu wa ngozi-Albino
 
Mzee huyu kaacha kazi yake nzuri tu ndani ya chama , kaingia genge la washirikina na waganga wa kienyeji mchana kweupeeeee!

Misafara ya wakuu kwenda Bagamoyo na ving'ora vyao haviishi, kila wiki mara moja au zaidi.
Maalbino watakoma kuzaliwa!!
 
Mkuu ahsante kwa taarifa yako! Nimeipokea!
 
Mkuu ndiyo maana ndani ya Chama Chetu yupo mzee maarufu tunayemtegemea kwa ulinzi wa Chama na Nchi kwa ujumla! Huyu mzee almaarufu kama Ngombale Mwiru, sifa yake na vigezo vya kuendelewa kupewa wadhifa ni Uganga wa Kienyeji! Na Serikali inaogopa washirikina kupita maelezo! Tar 30 mwezi mmoja kuelekea uchaguzi mkuu waliondoa marufuku iliyokuwa imewekwa dhidi ya waganga wa jadi iliyokuwa imewekwa kwa minajili ya kulinda walemavu wa ngozi-Albino
Nina masikitiko mno kuona nchi yangu inakumbatia wachawi kama huyo Ngombale Mwilu anaye fikiri niheshima kuto kuapa kwa kitabu kitakatifu kama Bible.Mambo yao yao yanafikia ukingoni. Mungu yuko kazini maana hawezi kuvumilia dhihaka iliyo pitiliza
 
Back
Top Bottom