Tanzania ya kinyumenyume!

spotisana

New Member
Jan 3, 2011
2
0
Hodi hodi great thinkers. Ninashangazwa sana na mfumo wa kisiasa ulioanza Tanzania.Inakuwaje tunakwenda kinyumenyume kwa mambo mengi siku hizi? Mtu anayelaani ufisadi na kuwalaani mafisadi kwa sasa ni adui wa kundi fulani, atasakamwa sana na kutishiwa kufukuzwa kundini.Anayetuhumiwa ufisadi ndiye MTU SAFI na mwenzetu sana kundini!Kinyume. Leo hii anayepigana nchi yetu maskini isilipe pesa nyingi kwa tapeli anaitwa adui na kujengewa hoja kwamba amekiuka taratibu za uwajibikaji wa pamoja.Anayefagilia maskini siye tulipe pesa hizo nyingi kwa tapeli ndiye mtu bora na MWENZETU SANA! Kinyume. Yako mengi lakini leo nimeona niweke jamvini hayo mawaili katika kupiga hodi tu jamvini humu mwa great thinkers.
 
KARIBU SANA IlA NAFIKIRI UMEKOSEA HILI SIO JUKWAA LA MICHEZO(SPOTISANA)HII MADA IMESHAJADILIWA SANA ANGALIA THREAD KABLA HUJAANZA KUPOST MADUDU,LALA UNONO
 
Mkuu, spotisana ni jina langu na si mwanamichezo au sitakiwi humu jamvini kwa ubaya wa jina langu tu? Lala unono nawe pia.
 
Back
Top Bottom