Tanzania ya JK na Kodi ya Watanzania

Mkanya

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
599
14
magari%2Bya%2Bkikwete.jpg


Kwa hisani ya Michuzi blog.
 
Haya ndiyo tuliyokuwa tunayasema kwamba kuwa sababu ya utawala (uongozi) wa kishikaji kila mtu anajifanyia mambo apendavyo tu! Nchi hii hakika inahitaji mtu mwendawazimu kidogo kwa maana aliyejasiri katika kufanya maamuzi muhimu kwa ustawi wa taifa.
Mimi hapa ni mtumishi wa umma, katika muda wangu wote wa utumishi ndani ya serikali, hakika sijaona sababu ya kwa nini Serikali inajitwisha mzigo wa kununua magari mengi kiasi hicho ambayo gharama za kuyaendesha zisingetumika (maana hakuna faida ukilinganisha na kuwekeza kwenye miradi ya kunufaisha jamii) zingeweza kulipia ada wanafunzi wa vyuo vikuu vizuri tu. Hata nilishangaa siku moja Mkapa (Rais mstaafu) alipokuwa akihutumia umati katika chuo kikuu Makerere nchini Uganda hivi karibuni alizilaumi nchi za magharibi.
Hivi kweli Tanzania na rasilimali zote hizi tunashindwa nini hadi kufikilia kwamba hatuwezi mpaka nchi za magharibi zitufanyie mambo fulani? Mpaka ajitokeze mtu kichaa atuchape fimbo ndiyo hasa tujue wajibu wetu na matatizo yetu wenyewe?

Tunatakiwa kama nchi kujua matatizo yetu yote na hatua inayofuata ni kuchukua hatua ya kuyatatua, sasa yalikuwa machache kabla ya serikali iliyopo sasa hivi lakini yameongezeka na hakuna ndani ya mfumo wa serikali hii anaweza kujitambua na kusituka ili kujirekebisha kwa ajili ya kutafuta mafanikio zaidi kwa maisha ya watanzania.

Utakuta Kikwete hata safari anazoenda nje, nyingi ni kuzilaumu nchi za magharibi tu kwamba hazizisaidii nchi maskini kama Tanzania na Afrika kwa ujumla. Lakini akiulizwa vipa umbele vya nchi yake sijui kama vipo! Na kama vipo haviendani na mahitaji halisi ya nchi na watu wake, bali vinalenga kunufaisha kundi fulani tu ambalo ni la maswahiba wake.

Nilikuwa namsikiliza alipokuwa anahutubia juzi juzi huko Cuba, hakika ni aibu!! Ni aibu kama nchi kukosa dira halisia. Anasema waje kuwekeza nchini, lakini umeme ndiyo hivyo tena. Labda jambo moja niwakumbushe watanzania, kwamba dunia ilivyosasa hivi ni kama kijiji, jinsi tulivyokuwa gizani tena ni vigumu hata mtu wa kijijini Tanzania kujua tatizo kuliko dunia ya watu walioendelea kiuchumi kwamba tanzania tulikuwa gizania kwa zaidi ya mwezi hivi.

Sasa mwekezaji nani utakayemwambia aje kuwekeza naye abebe au aende benki kukopa na kuzika fedha zake katika mazingira hayo yasiyo na uhakika wa nishati ya umeme.

Anasema nchi ina usalama kisiasa (political stability); je watu wako wana kipato cha kutosha kununua bidhaa ya mwekezaji akizalisha kutoka kwenye uwekezaji wake? Hivyo, tunatakiwa kuwafanya watu waondokana na umaskini wa kipato, wasiishi maisha ya chini ya dolla moja kwa siku. Tukuze uchumi wa mtu mmoja mmoja ndipo tutakapovutia wawekezaji kutoka nje waje kuwekeza katika sekta zinazozalisha kwa ajili ya kuwauzia wananchi wa Tanzania.

Vipengele vyote vinavyohusika na Pro-poor macroeconomic vitatuliwe ili uchumi wa nchi ukue na hatimaye baadaye kama kitagawiwa katika usawa kwa wananchi (equity allocation), basi hata lile pengo la maskini na tajiri litapungua. Maana mwekezaji yeyote yule soko lake kubwa hutegemea wateja wa kima cha chini na kati maana ndio walio wengi katika nchini. Tuwasaidie hawa! Mishahara ya watumishi wenyewe haitoshi lakin kamati nyingi tu huwa zinaundwa na kutumia fedha nyingi wakati mapendekezo ya kama hizo hata siku moja hayajawahi kutekelezwa kama yanayoelekeza. Wapi na wapi tunalaumu nchi za magharibi wakati wenyewe hatujitambui? Wapi na wapi kuomba nchi za magharibi waje kuwekeza kwetu wakati hatutambui nini tukifanye kwanza ili nao wavutiwe kuja?

Neno mafisadi ndani ya vyombo vya habari kila siku vinasikika si ndani tu hata kwa walio nje ya nchi, sasa nani anaweza kuja kuwekeza wakati mazingira ya fursa za uchumi yako tu kwa wale wenye nacho? Wengi hawana hizo fursa na wakijaribu kuwa nazo basi mafisadi wanatangulia na kuwaburuza ili wabaki masikini siku zote. Mungu anilinde na atulinde sote, lakini kubwa atubadilishe ili tuweze kutumikia wananchi.
 
Inabidi aje kiongozi mwendawazimu fulani asijali uswahiba. Shangingi marufuku, badala yake subaru ndo zitumike
 
Tatizo lenu watanzania hamfanikiwi kwa sababu mnashindwa kujua who is
R= Responsible
A= Accoutable
C= consult-able
I = Informed

Kwenye hiyo picha kama ukiwa makini, unatakiwa ujue nani ni Accountable... huyo ndio unatakiwa kula sahani moja na yeye... sio yule ambale ni just Informed...

Hata hivyo inasikitisha katiba inasema aliye-responsible na day-2-day business of government kwamba ni waziri mkuu... lakini ninyi mnasema ni rais kweli elimu ni muhimu.
 
No no no this is too much, Gari za kubeba wagonjwa unakuta zimechoka lkn kubeba majani ya ng`ombe za .......... unakuta gari zuri mno kama ilivyo katika pics
 
sasa wabebee wapi majani jamani?? gavamenti haina mapikapu kama yale ya mgombani.
 
Labda ni gari la wizara ya mifugo...

Kweli inawezekana kuwa ni la wizara ya mifugo!! Ila wizara ya mifugo hawafanyi tafiti, na tafiti taasisi za serikali zinazofanya tafiti numba zake ni SU. Sijui kama hii gari ya thamani kiasi hiki na ingekuwa inamilikiwa na mtu binafsi kama angekuwa tayari kubebe majani!

Serikali iliwahi kutetea kuwa wanayahitaji sana haya magari kwa mzingira yake, kumbe ni kubebe majani, Kwanini basi wasinunue pick-ups double cabin ili mbele ibebe watu na huku nyuma watie nyasi zao?

Ni matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma. Pinda kiongozi wa serikali inabidi atueleze!
 
Msishangazwe na hilo, wala hayajaanza leo hayo mambo!! Kwenye nyumba za serikali watu wamegeuza mashamba... Kuna kipindi zamani ilikuwa fashion kwa kila nyumba oysterbay kuwa na ng'ombe!!! Sasa ukizingatia zilikuwa nyumba za serikali then hata nyasi zilikuwa zikibebwa kwenye magari hayohayo ya serikali!!!! Na nyasi ni mfano tuu...hayohayo magari ya serikali ndiyo yanatumika kusambaza maziwa na mayai mahotelini na madukani!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom