Tanzania wanataka kununua umeme Ethiopia

Kama ni kweli,Badra Masoud kataa kufanywa commedian!Sisi hatutaki kucheka wakati huu,tunamachungu mengi juu ya nchi yetu.
 
yaani sisi tanzania wenye maziwa, milima, hifadhi za wanyama, gesi, madini, mafuta tunaenda kuomba umeme ethiopia nchi ambayo imekua kwenye vita kwa miaka nenda rudi, nchi ambayo ilikua haiwezi kulisha wananchi wake bila kupata misaada ya chakula kutoka UN?...haki ya nani...sasa it is confirmed...tanzania hii nchi imelaaniwa sijui ni baba yetu wa taifa alitupa laana kabla hajafa au ni nini
 
Baada ya kujifunza kuwa wabunifu na namna ya kutumia rasilimali zetu zilizopo tunapenda kununua tu kila kitu huku sisi tukikaa kwenye vijiwe kushuhudia kila nchi ikibeba fedha zetu kupeleka makwao!
Kwanza hiyo stretching itagarimu shilingi ngapi, na jee tutahakikishaje usalama wa kupitisha hiyo power across kenya or across southern sudan and uganda??
 
Kweli kabisa jangwa lina tuuzia umeme katika nchi iliyozungukwa na maji!khaa kweli wataalam wetu ni bogus!
 
duh! hawa viongozi wa serikali ye2 wapmwe akili huwenda ilitakiwa wawe milembe huko chizi co lazma abebe makopo jaman
 
i smell a raw deal here..wakizibiwa mrija mmoja wa wizi wanatoboa mwingine..another richmond in the making,.mapacha watatu wanatafuta hela ya kustaafu
 
yakhe, si walisema gesi ya kule ntwalaaa, itazalisha umeme mwingineeee?

naomba kuchangia kidogo, kuhusu vyanzo vya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme, ethiopia wametuzidi sana sana nawaeleza, ni nchi ya pili kwa africa kuwa na chanzo kikubwa cha maji kuzalisha umeme, ya kwanza ni drc kwa kabila, hii nafikiri ni duniani inaongoza, sema ndio hawajaweza ku invest. Drc kuna maporomoko ambayo yanaweza kuzalisha mw 120,000 kwa pamoja, hakuna sehemu kama hii duniani, hili halina ubishi. Vilevile ethiopia wana potential kubwa sana kwenye kuzalisha umeme kwa upepo. Ila sasa ethiopia wako kwenye utekelezaji wa miradi kukuza mg kufikia 8000, si kwamba tayari wanazo, wako kwenye utekelezaji. Halafu unajua hawa wako mil 82 idadi yao wadau.

Nchi yenye kiwango kikubwa africa cha umeme kwanza ni rsa wana zaidi ya mw 40,000, then egypt wana kama mg 24,000. Ila egypt raia wake wamesambaziwa umeme zaidi ukilinganisha na rsa, kwa hivi wadau nimesema nichangie ukweli kimazingira.

Nasi tupige msuli tupate walau mg 3000
 
Nipashe walitoa hii habari nashangaa wanaomwita mtoa mada ni mwongo

Katika hatua nyingine, Badra alisema Tanzania inafanya mazungumzo na serikali ya Ethiopia ili kuangalia uwezekano wa kununua umeme kutoka nchi hiyo, “Njia kuu za kusafirisha umeme zitakapounganishwa na kukamilika, nchi yetu itaweza kununua umeme unaozalishwa kwa njia ya maji na unaouzwa kwa bei nafuu moja kwa moja kutoka nchi kama Ethiopia,” alisema na kuongeza: “Ethiopia wanazalisha nishati ya umeme megawati 10,000 na kubakiwa na ziada ya megawati 8,000.”


Alikuwa akizungumzia mkutano wa mawaziri wa nishati wa nchi za Afrika Mashariki na Kati kuhusu mtandao wa usambazaji wa nishati hiyo unaojulikana kama Eastern Africa Power Pool (EAPP) unaozihusisha nchi 11 za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djibout, Ethiopia, Libya, Jamhuri ya Sudan na Misri.

Source: TANESCO: Mameneja 29 wamesimamishwa kazi; Hakuna mgawo; Mazungumzo ya kununua umeme kutoka Ethiopia yanaendelea - wavuti.com
 
i smell a raw deal here..wakizibiwa mrija mmoja wa wizi wanatoboa mwingine..another richmond in the making,.mapacha watatu wanatafuta hela ya kustaafu

si kweli na hakuna kitu kama hiki,hivi nyie watu hata taarifa za habari hua hamtazami?mbona Prof muhongo alitoa ufafanuzi mzuri tu jana star tv na wala sio huyo badra masoud,kwlei nchi ina watu legelege na wasio critical ndo maana mnaenda na upepo ivi ivi
 
nipashe walitoa hii habari nashangaa wanaomwita mtoa mada ni mwongo

katika hatua nyingine, badra alisema tanzania inafanya mazungumzo na serikali ya ethiopia ili kuangalia uwezekano wa kununua umeme kutoka nchi hiyo, "njia kuu za kusafirisha umeme zitakapounganishwa na kukamilika, nchi yetu itaweza kununua umeme unaozalishwa kwa njia ya maji na unaouzwa kwa bei nafuu moja kwa moja kutoka nchi kama ethiopia," alisema na kuongeza: "ethiopia wanazalisha nishati ya umeme megawati 10,000 na kubakiwa na ziada ya megawati 8,000."


alikuwa akizungumzia mkutano wa mawaziri wa nishati wa nchi za afrika mashariki na kati kuhusu mtandao wa usambazaji wa nishati hiyo unaojulikana kama eastern africa power pool (eapp) unaozihusisha nchi 11 za tanzania, kenya, uganda, rwanda, burundi, jamhuri ya kidemokrasia ya kongo (drc), djibout, ethiopia, libya, jamhuri ya sudan na misri.

source: tanesco: Mameneja 29 wamesimamishwa kazi; hakuna mgawo; mazungumzo ya kununua umeme kutoka ethiopia yanaendelea - wavuti.com

nipashe na waziri wa nishati ipi ni reliable source ya information kama hii,waziri alilizungumza jana star tv na alisema hakuna mpango huu bali nia ni kuzalisha umeme wa gas,makaa ya mawe,jua na upepo
 
kuna mwanasiasa ambae sio kigeugeu?
nipashe na waziri wa nishati ipi ni reliable source ya information kama hii,waziri alilizungumza jana star tv na alisema hakuna mpango huu bali nia ni kuzalisha umeme wa gas,makaa ya mawe,jua na upepo
 
Ama kweli ukiona elimu ni ghali basi jaribu ujinga!
ndo hivyo tena mkuu, mzee alitumia miaka kama 25 hivi kuelimisha Watz ambapo ilikuwa kazi ngumu sana na wengine wametumia nguvu kidogo sana kulipeleka taifa katika ujinga.
MATOKEO: Kila mmoja wetu anayaona lakini hayafurahishi maana inafikia hata waziri wa elimu yenyewe hajua structure ya nchi yake!!!! ...keep walking

 
meneja wa mawasiliano wa tanesco badra masoud amesema serikali yetu inafanya mazugumzo na serikali ya ethiopia ili kuangalia uwezekano wa kununua umeme kutoka nchi hiyo. umeme wao unazalishwa kwa njia ya maji na unaouzwa kwa bei nafuu moja kwa moja kutoka nchini ethiopia. ethiopia wanazalisha nishati ya umeme wa megawati 10000 na kubakiwa na ziada megawati 8000. nilivyosoma hii habari nilicheka na kukasirika mda mmoja.
Tanzania tuna mito na vyanzo vingine vingi zaidi ya ethiopia. sasa inakuaje wenyewe wanaweza kua na megawati 10000 alafu sisi tushindwe? hii ni haibu kwa nchi yetu

kabla ya kufikiria kununua umeme ethiopia tupeni kwanza mikakati mliyonayo kuhusu gas yetu hapa nchini sio mnaturudisha kule kwa yule shetani richmond bado hajasahau hilo mjue.
 
Jamani huu ni ujinga gani Tanzania imegundua gasi inayoweza kutosheleza mahitaji ya UK,France na Germny kwa pamoja sas iweje tusiitumie gasi yetu kufua umeme wa bei rahisi ????????.
 
meneja wa mawasiliano wa tanesco badra masoud amesema serikali yetu inafanya mazugumzo na serikali ya ethiopia ili kuangalia uwezekano wa kununua umeme kutoka nchi hiyo. umeme wao unazalishwa kwa njia ya maji na unaouzwa kwa bei nafuu moja kwa moja kutoka nchini ethiopia. ethiopia wanazalisha nishati ya umeme wa megawati 10000 na kubakiwa na ziada megawati 8000. nilivyosoma hii habari nilicheka na kukasirika mda mmoja.
Tanzania tuna mito na vyanzo vingine vingi zaidi ya ethiopia. sasa inakuaje wenyewe wanaweza kua na megawati 10000 alafu sisi tushindwe? hii ni haibu kwa nchi yetu

ndugu yangu hujui kuwa tanzania ni kame kuliko Ethiopia hivyo hatuwezi kuzalisha umeme wa nguvu za maji? pia hujui kuwa sani hatuna uweze wa kuzalisha moja kwa moja mpaka tununue kwa third part? ndo maana naipenda nchi yangu Tanzania majibu mepesi kwa maswali magumu.
 
Jamani huu ni ujinga gani Tanzania imegundua gasi inayoweza kutosheleza mahitaji ya UK,France na Germny kwa pamoja sas iweje tusiitumie gasi yetu kufua umeme wa bei rahisi ????????.

Tanzanians free gifts of nature we give freely to the world ooh what a tragedy!
 
si kweli na hakuna kitu kama hiki,hivi nyie watu hata taarifa za habari hua hamtazami?mbona Prof muhongo alitoa ufafanuzi mzuri tu jana star tv na wala sio huyo badra masoud,kwlei nchi ina watu legelege na wasio critical ndo maana mnaenda na upepo ivi ivi
dili la richmond,karamagi alitangaza kama alivyotangaza huyo muhongo wako!!!!!keep sleeping,you can't trust this administration you novice!
 
Overview of EEPCo

Having total area of 1.1 million km 2 , 122 billion m 3 of water resource per annum and 75.8 Million populations in the Horn of Africa, Ethiopia is often referred to as the water tower of Africa Ethiopia. This implies Ethiopia has an enormous potential for hydropower developments, next to DRC in Africa, with the generating capacity of about 45,000 MW from hydro. In addition to, Ethiopia has a capacity of generating more than 1,000 MW from Geothermal and more than 10,000 MW Wind and Solar . Nevertheless, currently the deployment is restricted to 800-900 MW, i.e. less than 2.5% of the overall potential resource.
The Ethiopian Electric Power Corporation ( EEPCo ), with the vision of "being a center of excellence in providing quality electric service at every one's door and being competitive export industry", is making unreserved efforts to utilize the untapped water resources for hydropower developments. The company is also working to realize its mission of "providing adequate and quality electricity generations, transmissions, distributions, and sales services through continuous improvement of utility management practices responsive to the socio-economic development and environmental protection need of the public". It was named in 1997- after serving in the name of Ethiopian Electric Light and Power Authority which was established in 1956 .

The corporation has two electric energy supply systems: the Interconnected System (ICS) and the Self Contained System (SCS). The main energy source of ICS is Hydro power plants and for the SCS mini hydro's and diesel power generators allocated in various areas of the country.
 
Back
Top Bottom