Tanzania wamekopeshwa na IMF

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Tz wamekopeshwa na IMF dola 400bil, Kuna mikakati ya kurudisha au hilo deni litasamehewa??

Au mpaka kizazi cha 2040??

TUJIULIZE, SISI HATUWEZI KUZALISHA.

Hebu tujadili hili??wana THINKTANKER
 
Tunahitaji kujua masharti ya mkopo kwanza. Hizi tabia za kuambiana tu ooh tumepewa mkopo wa sh. kadhaa ni very irresponsible. Taarifa za mikopo zitolewe kwa ukamili.
 
Tz wamekopeshwa na IMF dola 400bil, Kuna mikakati ya kurudisha au hilo deni litasamehewa??

Au mpaka kizazi cha 2040??

TUJIULIZE, SISI HATUWEZI KUZALISHA.

Hebu tujadili hili??wana THINKTANKER

Kisendi mhola wang'wa baba?
Huu mkopo ni ajili ya miradi gani? Maana zaweza ishia mfukoni mwa Rostam Aziz tu na kuliachia taifa mzigo mzito wa kulilipa.
 
ifm hawana uwezo wa kuikopesha TZ $400bil
kwa kifupi bajeti ya TZ $7 bil
tafadhali fanya uhakiki wa kiasi kilichokopeshwa
 
Last edited:
Ni kweli tz wamekopeshwa hicho kiasi, na bajeti ya Tanzania kwa mwaka ni zaidi ya Tirioni 3
 
The International Monetary Fund (IMF) board has approved USD336m Exogenous Shocks Facility Arrangement for Tanzania to completes fifth review under the Policy Support Instrument.
 
Last edited:
Tunahitaji kujua masharti ya mkopo kwanza. Hizi tabia za kuambiana tu ooh tumepewa mkopo wa sh. kadhaa ni very irresponsible. Taarifa za mikopo zitolewe kwa ukamili.

kama tutaanza hivi tutafika mbali wote inabidi tuanzie hapo chanzo ni muhimu na si kulopoka tu. na inabidi tujulishwe hiyo hela ina investiwa vipi maana wameshaanza sasa sijui stimulus package, tanesco wanahitaji hela hii jamani viongozi wetu 'wamelo' nyie.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Tz wamekopeshwa na IMF dola 400bil, Kuna mikakati ya kurudisha au hilo deni litasamehewa??

Hivi tunazijua dola 400 bilioni zikoje jamani au tunasema tu? Hii ni dola 400 milioni au bilioni? Tunajua tofauti ya milioni na bilioni na kati ya dola na shilingi?

dola 400 billioni ni dola milioni 400,000 !

Lets get these figures right before we confuse people, isn't this supposed to be the home of great thinkers? Apparently some of us can't tell a million from a billion.
 
inategemea na hio hela itatumika kwenye malengo yake? kama itatumika kwa malengo yake basi inaweza kusaidia na ikarudishwa baadae.tatizo ni kwamba misaada mingi haitumiki kwenye malengo yaliokusudiwa.tanzania hatuna sababu ya kuwa maskini sema viongozi wetu ambao walisoma kwenye mfumo wa elimu ya kukalili wanashindwa kuwa creative kwenye kuendeleza nchi.kwa vile hawana mbinu ya kutumia elimu yao kuleta maendeleo kwenye nchi wanajikuta wanafanya ufisadi hili wajilinde kimaisha kwani wasipofanya hivyo na ikatokea bahati mbaya mtu akatoka serikalini hatoweza kumudu maisha ya kawaida kwa vile hana elimu ya kujiendeleza.
 
Ni kweli tz wamekopeshwa hicho kiasi, na bajeti ya Tanzania kwa mwaka ni zaidi ya Tirioni 3

Trilioni 3 nini? Maembe? Machungwa? Dola za Zimbabwe? Yen za Japan? Yuan za China? Dola za Marekani? Au shilingi za Tanzania?

Let's think before posting and arguing about things we do not have a clue about.Tanzania mikopo yetu ni ya range ya dola bilioni 5 mpaka 10, hiyo 336/ 400 ni millions in USD siyo billion, sasa kama unai convert na kuipeleka kwenye Tanzanian shilliongs na kupata roughly 400 billion Tanzanian shillings, usiseme 400 bilion USD.

Hivi tutaweza international trade kama simple convertion tu kimbembe?
 
400 bil Tshs au dola 336 mil.

Kukopa sii vibaya sema tu pesa hiyo itumeke vizuri!

Kudaiwa sii dhambi!
 
Wadanganyika nyinyi watu wa ajabu saaaaana. Badala ya kusahihisha na kuendelea ku discuss issue mko mabishana ni dola au shilingi. Hii inawasaidia nini? Jiulizeni tu hivi hawa wakubwa wetu wanapokopa pesa hii huwa wanahitaji kwa ajili ya nini? nini vipaumbele? au ndio zikifika zinastimulate safari za viongozi kwa kuwa eti wanaenda kutafuta pesa?
Kulipa ni sisi wote tunalipa lakini kukopa sisi hatutakiwi kujua.
Haya wabunge wetu tunawapa kazi. Wakati wa bajeti tuwasikie mnamuuliza Mkulo mnasikia? na isiishie hapo tu bali monitor usage of this money!
 
Wewe unataka watu wa discuss mkopo ambao haujaeleweka ni wa kiasi gani?

Halafu nani anarudisha discussion kwenye dola au shilingi wakati watu washatoka huko kama siyo wewe?
 
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Tanzania kupitia BOT imekopeshwa na IMF jumla ya USD336 million. Kwa kawaida BOT ndio wanakopa mikopo kutoka IMF kwa niaba ya Serikali kwa ajili kusaidia urari wa malipo(Balance of payment) ya nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom