Tanzania VS Uganda

Najua ni kidonge kichungu kumeza ila ukweli ni kwamba uwezo wa Tanzania katika kila kitu ni mdogo sana na hawa wanasoka wetu wana rekodi ndefu tu ya kufeli. Labda ni vyema wahisani wa soka la Tanzania wakawekeza katika michezo mingine, labda riadha ambayo imewahi kutuletea heshima miaka ya nyuma.

Wakishindwa hilo wawekeze katika kutatua matatizo mengine ya kijamii na kiuchumi yanayotukabili na lau watashindwa haya basi watuongezee sisi wanahisa marejesho ya umilikaji wa hisa (dividends).
 
Nani huyuuu, Mandela labda, sina uhakika aliwahi sema " Success is going from one failure to another without loosing hope" yaani kwa kiswahili " Mafanikio ni kupitia kufeli sehemu moja na kufeli sehemu nyingine bila kukata tamaaa" Kama hivyo ndivyo basi naamini tusiikatie tamaa stars tupe muda tu, mbona imechukua ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati? Tusidharau mafanikio madogo kwani ni hayo hayo ndio yanaashiria yale makubwa. Naamini miaka ijayo Stars inaweza kuwa timu tishio sio afrika Mashariki na Kati tu bali afrika nzima na dunia. Tusiikatie tamaa!
 
Kichwa cha mwendawazimu hao

Lengo kuu ilikuwa sio kuchukua kombe. Tuliposikia kuna Misri basi tukaona hatuwezi kuchukua kombe kama tulivyofanya challenge. Wadau wakasema tuzitumie kwa maandalizi ya kukutana na afrika ya Kati katika kusaka tiketi ya kombe la afrika 2012. Kama ni kichwa cha mwenda wazimu basi sio stars peke yao bali wadau wote wa soka bongo! Saikolojia inasaidia sana kushinda soka, sie tulikata tamaa kabla hata hatujakama pipa kuja Misri basi tusishangae Kongo au Uganda ikichukua kombe ili.
 
nami nashangaa mpaka sasa kimya, walionyesha kuwa itakuwa live ila mpaka mida hii kimya
 
Back
Top Bottom