Tanzania VS Uganda

huyo ni othuman machupa yupo denmark, naona staz washapoteana wanawaruhusu sana kuingia golini kwetu
 
Ila kiungo hakuna kitu ndio maana beki zinateseka. Labda kipindi cha pili watabadilika
 
Namuona kama Said Maulid ndani duh jamaa kaitwa huyu SMG huwa namkubali sana nadhani anacheza soka la kulipwa kule Mos

SMG sio matani, anacheza sana. Mie mbona naona kama Stars inacheza vizuri. Nashangaa kusikia wanasema tumezidiwa, mie nadhani tunashambulia zaidi kuliko wanavyoshambulia wao.
 
Tunaitaji kushinda hii mechi ili kuingia nusu fainali. Uganda wanahitaji sare. Lakini hayo yote pia yanategemea mechi ya Misri na Burundi. Burundi akishinda( akiachiwa, maana hakuna njia watamfunga Misri) inabidi wahesabu tofauti ya magoli ya kufungwa na kushinda, ikifika hapo inaweza kula kwetu mana tulichapwa mengi. Nadhani Burundi akijitahidi weeee atapata sare vinginevyo iende uwanjani na kapu la kubebea magoli yao ya kufungwa!
 
Mkuu tuombe tushinde tu hii game ..biashara itakuwa imeisha..burundi hawezi kumfunga Misri ng'o
 
staz wamezidiwa katikati ya kiwanja ndio maana uganda wanatushambulia sana, kwa mchezo huu wanaweza kusawazisha beki itachoka
 
na tatizo lingine tunashindwa kumiliki mpira kwa hiyo muda mwingi tunautumia kutafuta mpira na hata tukiupata tunaupoteza kizembe sana ila Inshaalah Mwenyezi Mungu atatusaidia
 
tukishinda tunasonga mbele endapo misri atamfunga burundi ana ata droo kitu ambacho kipo wazi kabisa
 
Back
Top Bottom