Tanzania tunapata snow/theluji - maajabu!

imewahi tokea kenya mwaka jana
effects za global warming na climate change
 
imewahi tokea kenya mwaka jana
effects za global warming na climate change

Ndio hapo sasa.
Ukiona tumeshindwa kukabili maisha katika hali ya hewa "nyepesi" isiyo na changamoto nyingi, imagine ndio tunapata hali ya hewa ngumu yenye changamoto ngumu.Wananchi watapata shida isiyo kifani.Ndio wataelewa kwanini wenzetu nchi zilizoendelea zenya "hali ya hewa ngumu" wako wachungu sana kufuatilia matumizi na mapato ya nchi. Hawawezi kuchekelea mafisadi na kuwaacha wapete na wizi bila kuchukuliwa hatua.
 
Snow inaanguka huko Mufindi utadhani tuko yuropa na marekani!
Mwisho wa Dunia unakaribia?
Je Watanzania wamejiandaa kwa hali ya hewa ya namna hii?

wow wow wow!Mabadiliko ya hali ya hewa hayo.. Hebu Tausi tuwekee picha basi ukipata wasaa.

Ila maeneo ya Mufindi ni baridi, au nimekosea? sijawahi fika
 
Hakuna cha ajabu. Kwa miaka mingi kumekuwa na joto ambalo sio kawaida ya Mufindi. Wenyeji wa Mufindi wanafahamu kuwa miaka ya nyuma theluji ilikuwa inaanguka. Ieleweke kuwa Mufindi ni moja ya sehemu zenye hali ya baridi sana kwa Tanzania. Theluji kama inayoanguka Mlima Kilimanjaro ilikuwa pia inaanguka huko. Kwa kuwa baridi iliyopo Mufindi sio kali sana kama Kilimanjaro, theluji hiyo huwa inayeyuka baada ya muda, na ndiyo sababu watu wengi hawakuwa na taarifa. Tukumbuke kuwa enzi hizo hakukuwa na mobile phones, television na hata cameras hazikuwepo kwa wingi kiasi cha wenyeji kupiga picha na kuzionyesha. Ila takwimu zipo.

Kwa waliosoma vizuri Geography, katika Afrika karibu na Equator theluji haiko Mlima Kilimanjaro peke yake, ipo pia milima ya Ruwenzori huko Uganda. Kilichokuwa unique kuhusu Mlima Kilimanjaro ni kwamba theluji ilikuwepo bila kuyeyuka kwa mwaka mzima, na kwa miaka yote. Hali hiyo sasa inabadilika hasa kutokana na uharibifu wa mazingira tunaoufanya binadamu kama kukata miti n.k.
 
Juzi nilkuwa uko ilikuwa full ukungu!
Izi mabadiliko so maana Njombe nowdays kuna Malaria kama DSM.
Kuna haja ya personal initiatives kwenye environment conservation!
 
Sio jabu,
nafikiri inaweza kuonekana kwamba ni ajabu kwa sasa kwasababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.....kuwa na joto zaidi,

lakini Mufindi na Makete hilo ni jambo la kawaida.
 
Mbona mbeya inadondoka tunaita mvua ya mawe tena miaka ya tisini snow ilishuka ikakaa siku 3.
 
Mpiga Nyoka, Mvua ya mawe na theruji ??? ni vitu viwili tofauti kabisaaa

Kweli mkuu. Mpiga Nyoka mvua ya mawe kwa kiingereza inaitwa 'hailstorm'. Theluji kwa kiingereza ni 'snow'. Mvua ya mawe inaweza hata kujeruhi na kuleta maafa kama kubomoa vioo na kadhalika. Snow ni nyepesi, laini, kwa wengine inakera lakini ikikuangukia haiumizi.
 
hata siwaelewi ni snow imedondoka au ni mvua ya mawe??
kama ni snow haiwezi kuwa na madhara kwani itayeyuka mda sii mrefu nijuavo Mufindi joto lake haliwezi kuwa chini ya centgrade 3.
 
Snow inaanguka huko Mufindi utadhani tuko yuropa na marekani!
Mwisho wa Dunia unakaribia?
Je Watanzania wamejiandaa kwa hali ya hewa ya namna hii?

mufindi ni kawaida sana,nakumbuka nikiwa ktk mafunzo ya JKT zamani maeneo hayo yote ya mufindi na mafinga snow kwao si jambo la mshangao sana
 
Back
Top Bottom