Tanzania tunahitaji Rais mzee, Waziri Mkuu kijana

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Kwanza nieleze mimi ni mfuatiliaji sana wa siasa za nchi mbalimbali. Nilichogundua ni kwamba marais wengi wazee ni wazuri sana kwa sababu zifuatazo:
(i) Kwanza wana busara sana
(ii) Pili na kubwa zaidi, kutokana na umri hana ambitions kubwa za kutumia urais ili awe tajiri.

Mifano mizuri ni rais wa Zambia kwa muda mfupi amefanya makubwa sana, mandela, Wade(though ana tamaa ya kipindi cha tatu), Kibaki nk. Marais wote hawa ambao walipata urais uzeeni hawajakubwa na kashfa za rushwa.

Ila tukiwa na rais mzee ateue kijana kama waziri mkuu ili akimbizane na mambo ya kila siku.

Ningefurahi kama mmoja wa wazee hawa angeukwaa urais: Dr. Slaa, Sitta, Lowassa, Dr Salim bado ana nguvu na kiukweli anaweza akawa Rais mzuri zaidi
 
Mbona haujataja Marekani, Uingereza, kama mifano yako umeishia hapa Africa pekee? just thinking aloud
 
Lowassa hawezi kuacha tamaa ya hela maana ndiyo imemfikisha hapo pili lowassa anapenda sana madaraka na atataka kua kama Moi wa Kenya yaani awepo tu kwenye siasa kwa kutumia hela zake na vijana wake atakaowapandikiza...Tz inahitaji better........Dr Slaa anafaa ila timu hana, CDM bado wachanga watacheza bahati nasibu na nchi maskini kama hii itakua hatari..Sitta anafaa anaonekana kukerwa na mambo mengi, Salim amechoka siasa hatofaa tena, nafikiri Sumaye nae ni mzee na anafaa
 
Siasa zetu si vizuri kufananisha na mataifa makubwa. US au UK wana viongozo vijana sana lakini wao wana mechanisms za ku control corruption. umeshawahi kusikia rais USA au PM wa UK ana tatizo la rushwa? Ile ni dunia nyingine ni Open society ila yetu ni closed society busara na uadilifu wa kiongozi binafsi ni muhimu
Mbona haujataja Marekani, Uingereza, kama mifano yako umeishia hapa Africa pekee? just thinking aloud
 
Lowassa hawezi kuacha tamaa ya hela maana ndiyo imemfikisha hapo pili lowassa anapenda sana madaraka na atataka kua kama Moi wa Kenya yaani awepo tu kwenye siasa kwa kutumia hela zake na vijana wake atakaowapandikiza...Tz inahitaji better........Dr Slaa anafaa ila timu hana, CDM bado wachanga watacheza bahati nasibu na nchi maskini kama hii itakua hatari..Sitta anafaa anaonekana kukerwa na mambo mengi, Salim amechoka siasa hatofaa tena, nafikiri Sumaye nae ni mzee na anafaa

Hapo kwa sumae anafaa ntakuwa tofauti na yeye kwani mambo yake ni makubwa sema yamejificha sana. Pia kusema slaa hana timu umekosea sema labda ni kwavile vijana uweke shaka hapo ila wanaonekana wana msimamo
 
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Wilbroad P. Slaa amemteua ndugu Zitto Z. Kabwe kuwa waziri mkuu wa Tanzania. TBC1 News Nov. 2015.
 
lowassa hawezi kuacha tamaa ya hela maana ndiyo imemfikisha hapo pili lowassa anapenda sana madaraka na atataka kua kama moi wa kenya yaani awepo tu kwenye siasa kwa kutumia hela zake na vijana wake atakaowapandikiza...tz inahitaji better........dr slaa anafaa ila timu hana, cdm bado wachanga watacheza bahati nasibu na nchi maskini kama hii itakua hatari..sitta anafaa anaonekana kukerwa na mambo mengi, salim amechoka siasa hatofaa tena, nafikiri sumaye nae ni mzee na anafaa

haya ya kusema chama au watu fulani bado ni wachanga ndiyo tatizo la watanzania wengi na ccm inalitumia sana hilo tatizo kuendelea kuwa madarakani.

Ili kubadilika inabidi tufute haya mawazo kwenye bongo zetu.

Rais hafanye kazi na wanachama wa chama chake tu. Bali na wataalam mbalimbali ambao wengine ni wa chama chake, wengine wa vyama vya upinzani na wengi hawana chama. Kitu muhimu hapa ni utalaam wao na uzalendo wao na sio chama wanachotoka.
 
Eee Mungu rais awe Magufuli na Waziri Mkuu Tindu Lissu sijui inawezekana? It is my wish anyhow

This is once again the 50% correct outcome in politics which to me is a political mileage that my wish granted. Pole Lissu if and only if we had a very efficient and balanced political system it would be 100% wish. Again my wish guys no conflict.
 
Back
Top Bottom