Tanzania tuna: Viongozi, Watawala au Mabwana?

Ahsante saana wakuu kwa mada hii murua. Ni katika suala zima la kuongoza au kutawala. Mabadiliko yoyote katika jamii yanatokana na siasa amabayo ni safi na uongozi bora. Nataka nitoe mfano wa nchi ya china. Anayepewa contract husaini mkataba,lakini ikitokea likatokea lolote kama kula fedha kabla ya kitu alichopewa kufanya hakikuisha na hakipo kwenye kiwango knachoridhisha,serikali hutaifisha mali ya yule mtu yote na isipotosha inaingia kwa wana familia pia,hivyo mtu akionyesha wizi,hata kabla serikali haijamshtukia basi wan familia wana wajibu wa kutoa taarifa ili likitokea la kutokea awajibishwe yeye kama yeye.

Turudi nyumbani, mimi ni mtanzania halisi. Tanzania ni tajiri kuliko hata nchi za ulaya nyingi tu,umaskini wetu ni namna tunavyotumia raslimali zetu tulizonazo. Na hii ipo mikononi mwa viongozi wenye madaraka serikalini.

Tumekuwa na watawala,wanaojiangalia wao bila ya kuwa na uchungu na nchi na maisha ya watu duni kwa ujumla, Watu vijijini bado wankosa sh 100, hamuwezi kuamini lakini huo ndo ukweli,utadhani hatujapata uhuru.
Nafasi ya kiongozi ni kuleta mamabdiliko katika jamii anayoiongoza na hivyo maendeleo hupatikana.

Hatuna watu wenye uchungu na umaskini wa nchi yetu,wao wanaangalia miradi yao kama inaendeshwa vyema au la. Nasema hivi kwa sababu hawana muda wa kujua hata matatizo ya wananchi wao ni yapi na wawasaidieje? Wanasubiri uchaguzi wakawanunulie pombe,baiskeli,magodoro, na mambo mengine mengi.

Mabadiliko hayategemei historia iliyopo na iliyokuwepo,huwezi kusema kwa kuwa baba yako hakujenga nyumba ya tofali na wewe kama mtoto huwezi kuijenga hata ukiwa na fedha. Huku ni kudidimia kwa fikra,inawezekana yeye hakuona umuhimu kwa wakati ule. Ninacotaka kusema hapa ni maendeleo na mabadiliko,tuangalie tuko wapi na tunataka nini ili tufike wapi,c kuangalia waliokuwepo mwanzoni walifanyaje, na sisi ndo tufuate mtindo uleule.
Naamini tukiwa na viongozi waadilifu basi yote yanawezekana.
 
Susuviri,

..Kikwete aliteuliwa Naibu Waziri wakati wa utawala wa Raisi Mwinyi. tena aliteuliwa akitokea CCM, siyo Jeshini.

..una maana gani unapodai Nyerere alim-handpick Kikwete kuwa Junior Minister? au unataka kusema Nyerere ndiyo alim-recommend Kikwete kwa Raisi Mwinyi?

..kwa upande mwingine Mwinyi alimpenda sana Kikwete. kumbuka alimtoa kigogo Al-Nuur Kassum pale Nishati na Madini na kum-promote Kikwete kuwa Waziri. that single move said a lot about how Mwinyi viewed Jakaya Kikwete.

..baadaye Mwinyi akamteua Kikwete kuwa Waziri wa Fedha, baada ya kumuondoa Prof.Malima kutokana na ripoti ya Controller and Auditor General Mohamed Aboud, na shinikizo la wafadhili.

..Kikwete pia alipata msaada mkubwa sana toka kwa Mwinyi wakati wa mchakato wa kugombea ticket ya CCM mwaka 95. Msuya pulled a suprise win ktk kura za NEC akafuatiwa na Kikwete, na watatu akiwa Mkapa.

..baada ya hapo Dr.Lawrence Gama alianza kumsaidia Cleopa Msuya. Kikwete alimjia juu Lawrence Gama kwa kukiuka misingi ya dhamana ya Katibu Mkuu wa CCM kwa kumsaidia mgombea mmoja dhidi ya wengine.

..wako wanaodai Mwinyi alikuwa upande wa Kikwete ktk ugomvi wake na kambi ya Lawrence Gama na Cleopa Msuya. baada ya ugomvi huo, njozi za Uraisi za Cleopa Msuya zilizimika.

..actually ugomvi wa Kikwete na kambi ya Msuya inawezekana ndiyo uliopelekea Mkapa kushinda tiketi ya CCM. kura karibu zote alizopigiwa Msuya zilihamia kwa Mkapa alipopambanishwa na Kikwete.

..kuna theory nyingine though, inayodai kwamba Mkapa alishinda kutokana na kura za wajumbe wa ZNZ. inasemekana there was a last minutes deal btn Mkapa na Dr.Salmin Amour.

..SAMAHANI NIMEWATOA NJE YA MADA. NILIDHANI UKARIBU WA JK NA MZEE RUKSA ULIPASWA KUTOLEWA UFAFANUZI HAPA.

NB:

..kuna kipindi Baba wa Taifa alinukuliwa akisema alitamani ndani ya CCM wawepo "Vikwete" wengi zaidi kutokana na kazi nzuri ya Jakaya Kikwete akiwa mtumishi wa CCM.
 
Jokakuu:

Wakati anateuliwa kuwa naibu katibu, Jeshi na Chama lilikuwa intertwined. Hata kama angeteuliwa kutoka jeshini bado jeshi lilikuwa ni sekretariat ya CCM.
 
Zakumi said:
Jokakuu:

Wakati anateuliwa kuwa naibu katibu, Jeshi na Chama lilikuwa intertwined. Hata kama angeteuliwa kutoka jeshini bado jeshi lilikuwa ni sekretariat ya CCM.

Zakumi,

..hayo unayoyazungumza ni mambo ya kisomi-somi. actually you are correct. lakini, mara nyingine huwa napenda kuzungumza mambo free-free kama nipo kwenye kilabu cha komoni.

..sasa ni hivi:

..kwa kumbukumbu zangu JK alikuwa mwalimu wa siasa Tanzania Military Academy--Monduli. hapo namchukulia alikuwa jeshini.

..baadaye akapelekwa Mtwara au Lindi kuwa Katibu wa Chama wa Mkoa. hapo nachukulia alitoka Jeshini.
 
JokaKuu, I stand to be corrected, lakini nakumbuka nilikuwa naangalia hotuba ya JK alipoteua baraza lake na alizungumzia Mwl Nyerere alimwambia he will learn on the job alipompa wadhifa wa junior minister. But after reference nimegundua you are right in facts, lakini sasa je JK alidanganya umma? I wish tungekuwa na YouTube maana hii nakumbuka clearly anecdote yake maana nilikuwa horrified and mortified kwamba uwaziri utajifunza on the job!
About the close relaiton of JK na Mwinyi you are absolutely right, kuna hii intertwining ambayo ni vyema tukaiweka into context
Kuhusu uhusiano wake na jeshi nadhani hakuna haja kubishana maana ndipo alipotoka na akapata ukada wa chama lakini no previous civilian experience. Ndo nilikuwa namaanisha.
Thank you for the clarification.
 
Chochote kile alichofanya kabla kuwa rais kimeipa sifa za kuwa rais. Vilevile yeye kuwa katika cabinet kwa zaidi ya miaka 15, kuna nullify upupu wote aliofanya miaka ya nyuma.

Na kama anashindwa, there is something wrong with the guy or the system.

Kwa maoni yangu binafsi: The system of our governance has reached a saturation point.
 
JokaKuu, I stand to be corrected, lakini nakumbuka nilikuwa naangalia hotuba ya JK alipoteua baraza lake na alizungumzia Mwl Nyerere alimwambia he will learn on the job alipompa wadhifa wa junior minister. But after reference nimegundua you are right in facts, lakini sasa je JK alidanganya umma? I wish tungekuwa na YouTube maana hii nakumbuka clearly anecdote yake maana nilikuwa horrified and mortified kwamba uwaziri utajifunza on the job!
About the close relaiton of JK na Mwinyi you are absolutely right, kuna hii intertwining ambayo ni vyema tukaiweka into context
Kuhusu uhusiano wake na jeshi nadhani hakuna haja kubishana maana ndipo alipotoka na akapata ukada wa chama lakini no previous civilian experience. Ndo nilikuwa namaanisha.
Thank you for the clarification.

Susuviri:

Unajua speculation katika forum za kibongo zinachuliwa kama kweli. Facts zilizopo ni kuwa ana digrii ya uchumi. Hata kama haikuifanyia kazi fani aliyosomea lakini yeye kuwa commission officer wa jeshi na kuwa kwenye cabinet kwa zaidi ya 15 kunampa sifa zote za kuwa rais.

Kuboronga kwake kunaweza kuwa na factors nyingi na mojawapo ni system mbaya ya utawala.

Watanzania bado tunaamini kuwa CCM na mfumo wa utawala alioacha babu bado unafanya kazi.
 
................Ni lini tutaanza kuzalisha uzao wa Viongozi wenye maono, wachapakazi, jasiri, wabunifu, fanisi, wanyenyekevu, waadilifu, wakweli, wasiopenda makuu na wenye kuelewa maana ya Uongozi na umuhimu wa kuhamasisha na kutetea haki za jamii zao na si kujifikiria wao kwanza?.............

Hakuna hata siku moja ambayo utajikuta umeamka na kukuta kuna hayo hapo juu.

Juhudi kama hizi za JF inabidi ziimarishwe ili kidogo kidogo watawala/viongozi/mabwana watasikia na kurudisha discipline tuitakayo
 
Mchungaji,

Mimi niliacha kuwaita viongozi siku ile walipotukuza kutawala kuliko kuongoza. Waliamua kwa makusudi kuchanganya mambo hayo mawili na matokeo yao kiu yao haiko kwenye kuongoza bali kwenye kutawala.

Sababu yao kuwa hivi ni moja; ni rahisi kutawala kuliko kuongoza! Mtawala haitaji maono anahitaji maneno! Mtawala mara zote hutumia nguvu kuliko hoja; hana ushawishi wa wananchi bali utisho; na mtawala mara zote hutumia madaraka kufanikisha anachotaka wakati kiongozi huwafanya watu watende na kutekeleza mambo kwa sababu wanaona umuhimu wa mambo hayo.

Ndiyo maana tangu mapambano haya ya fikra tuyaanze nimekuwa nikiwaita "watawala wetu" na hatimaye watu wengi sasa (labda siyo wote) wanaanza kuwaona hivyo.

Watawala wanataka kuwa juu yetu si kwa sababu wanataka kutuongoza tufike mahali fulani; la hasha wao wanataka kuwa juu yetu kwa sababu ya madaraka na ujiko unaokuja na madaraka hayo. Naweza kusema pia kuwa wanataka madaraka kwa ajili ya kile ambacho kinaitwa "the pomposity of power".

Ving'ora, saluti, "ndiyo mzee", "tumsikilize", "mgeni wa heshima" bla bla bla! Ukiwaonesha dharau japo kidogo watakurupuka na kuanza "hivi wewe hujui mimi ni nani?"! Maana yake "mimi ni mtawala wako".

Kwa hivyo wala nisikuchoshe, hawa siyo viongozi bali ni watawala. SIku wakianza kutuongoza kweli watatambua utawala na cheo ni dhamana tu! Hawatatukuza vyeo vyao na nafasi zao kuliko maono na mwelekeo wa taifa.
 
Kama kawaida ya sisi Watanzania hii ni blah.. blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah nyingine kutoka kwa Kishoka.......
Swali.... umefanya nini kuondoka na hiyo hali????????????????? Au unalia na kulalamika tu...blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah
blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah blah

Ama kweli mkeo akiwa malaya basi kila ukiona mwanaume unahisi ni mgoni wako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom