Tanzania tuna viongozi viongozwa tu

Henry Kilewo

JF-Expert Member
Feb 9, 2010
899
1,084
Hivi Tanzania tunaviongozi au viongozwa ? mimi sijui, je wewe wajua? Najua wajua ila huna sehemu ya kulisemea kwa muda muafaka , sasa ngoja mimi ni seme yale ninayo ya jua japokuwa najua nitakugusa vilivyo ila kwasababu wewe ni mbishi utabisha kuhusu haya , mimi nakubali ya kwamba Tanzania hatuna viongozi bali tunaviongozwa, kwanini na sema hivi ? kwanini ni seme sasa? Kwanini niwakatae kuwa siviongozi ni viongozwa? Ni kwasababu hawafahamu wajibu wao kwa wananchi wao? Au ni kwasababu yalikuwa simatakwa yao ya kuwa viongozi bali ni kwashinikizo? Hapa ndipo tunapo kosa viongozi wawajibikaji kwasababu siyo ridhaa yao kuongoza bali nikulipwa fadhila

Sasa hapa ndipo tunapokosa viongozi bora tunakosa maadili ya kitanzania na utu kwa ujumla kwasaababu siyo ridhaa yao yakuwa viongozi na kuwa kwenye sekta wasizo kuwa na utaalamu nazo na mwisho wa siku kuishia kuburuzwa na kuwa viongozwa kutokana nakutokuwa na uhakika kwa kile wanacho kifanya kwa sababu siyo matakwa yao kuongoza waliyo wengi bali ni matakwa ya kutetea masilahi ya waliyo wachache ,

Na nna watuhumu moja kwa moja kwasababu maadili ya uongozi yanataka mtu mwenyewe kuridhia kufanya jambo kwa masilahi ya umma bila kujali itikadi ya kichama, kidini au kikabila kwakuwa tayari kashakuwa kiongozi kwa hiyo anatakiwa kukubali matokeo ya kuongoza jamii inayomzunguka kwa ridhaa yake iliawajibike moja kwa moja na nafsi yake itakuwa inamuuma kwakuwa atakuwa amejihukumu kwakuikosea taaluma yake

Nimewaita viongozwa kwakuwa hawafahaumu wajibu wao bali wanasubiri kufahamishwa wajibu wao, unapopata kundi kama hili kwa taifa linalokuwa kwa kasi utaishia kwenye lawama ambazo kimsingi hazina maana kijamii na kitaifa bali ni hasara na niudidimizaji wa kimaendeleo kwakuwa pale utakapo kosea hakuna wa kukuwajibisha kwa kuwa wapo pale kwaridhaa yako na kwa masilahi yako hapa ndipo tunapo chemsha na kamwe hatutasonga mbele kwa misingi hii ya kiujanjaujanja

Tunaviongozwa kwasababu waliyopo madarakani hawataki kuwajibika pale wanapokuwa wameteleza bali kutaka kujulikana kuwa wao niwasafi na wao ndiyo wao moja kwa moja na huwa hawakosei kwa kuwa wao wamekuwa malaika au miungu watu, huu siuungwana bali ni udikiteta,utapeli na ukiukwaji wa sheria za nchi na upotoshaji wa maadili ya uongozi na kuharibu dhana dhima ya uongozi kwenye taifa letu,

kwanini na sema haya sasa? Ni kwasababu ya kwamba wote tunafahamu ya kuwa siasa ndiyo maisha ya watu kwa kuwa viongozwa wa kuu wanchi wanatokana na siasa kwa hiyo bila siasa wasingekuwepo kwenye mtiririko huwo , na nimeyasema haya sasa kwakuwa tunaelekea kwenye mchakato mzima wa kisiasa na nchi itakuwa macho na masikio kwenye siasa muda simrefu na vuguvugu limekwishaanza huko mkwenye majimbo yetu tunapotoka, watanzania wenzangu tumekwishajionea wenyewe matamko ya wazi wazi ya vitisho sasa tunasubiri nini? au mpaka kuvunde kabisha, tanzania tuisimamishe imara kwa kuipa chama kingine
 
maana wameshindwa kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi wa juu yao au chini wanavyo ya tumia madaraka yao vibaya kwenye taiafa hili takatifu na kushindwa kuonyesha misimamo yao wazi wazi
 
mi nadhani tatizo hapa ni dhana potofu na nidhamu ya uoga wailyo nayo hawa wanaoitwa viongozi,
na kushindwa kusimamia maamuzi yao wenyewe wanayo yaoni ni sahihi au si sahihi,

ilikuweza kumaliza tatizo hili ni kuuwa kabsa mfumo wa serikali iliyoko madarakani na kuwa na
serikali itakayo tuwezesha kuwa na mfumo washirikishi jamii ya maeneo husika ndipo tutapata
viongozi bora wenye maadili mwema na wenye uchungu na wananchi kwakuwa atakuwa anatambuwa
yakuwa bila wananchi siwezi kuitwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom