Tanzania tuna Bahati mbaya, tunaenda mbele na kunarudi nyuma

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Mwalimu Nyerere aliweka msingi wa taifa. Mwinyi alijitahidi kwa uwezo wake kutupeleka mbele lakini nadhani kwa upole wake aliwaacha watu wakachezea nchi kwa rushwa wanavyopenda na nchi ikaporomoka. Kumbuka Mwinyi alikuta nchi imefuta kiwango cha ujinga kwa asilimia 95 akaturudisha hadi chini ya 40. Inflation ilikuwa karibia 40%. madeni ya nje yalikuwa makubwa hivyo tukawa hatukopesheki, udini na ukabila ukawa juu, nchi ikawa na nyufa nyingi.

Mkapa akaja, akarudisha heshima ya serikali, ikapunguza inflation, akalipa madeni nchi ikakopesheka tena, akarekebisha udini na ukabila nchi ikaenda. Ni ukweli kuwa alikuwa na kashfa za rushwa kwa serikali yake na huo ndio udhaifu wake mkubwa.

Kikwete akaja kwa mbwembwe, ari mpya, nguvu mpya. Cha kwanza akaanza kuharibu yote ya Mkapa, tumia akiba ya fedha za kigeni kwa kusafiri sana, mfumuko wa bei ukawa mkubwa sana, nchi ikaanza tena kuzungumzia udini, malumbano makubwa serikalini, uwajibikaji zero. Elimu ikadorora sana kwa kuwa walijenga shule kwa mbwembwe bila kuwa na walimu, vitabu hata madawati na vyoo. Leo nimesoma report ya CAG, tanzania kati ya 2008-2010 tumekopa sana. Tunakaribia asilimia 60% ya pato la taifa na ukivuka hapo hukopesheki tena. maadili ya serikali yameporomoka, kila kitu hakiendi. Mapato ya kodi hayakusanywi kikamilifu, rushwa kila mahali. kwa hiyo nchi imerudi ilikotoka na juhudi za Mkapa zimeuawa.

Sasa tunasubiri rais ajaye aanze tena from the scrarch. Wasiwasi wangu, tusipopata rais mzuri 2015 ili ajenge tena tutakwisha. Maana atachukua nchi from 0 above sea level. Akiwa kama JK ina mwaana tuta sail below sea level. Katika uchaguzi ambao wa TZ inabidi tuwe makini jamani ni 2015. Tuache siasa, maana siasa hazitusaidii sana. Tuangalie ni nani anaweza kutupeleka mbele na tukimpa tuhakikishe anafanya kazi. Asipofanya tuwe mbogo, la sivyo.............
 
Hiyo kweli ni bahati mbaya, MBAYA SANA!

Huwa naamini nchi yoyote kuendelea (katika nyanja zote za raia na mazingira yao) inahitaji kweli mkono wa MUNGU (wengine wanaiita bahati). Huwa naangalia mifano mingi huku duniani katika hilo, mfano rahisi sana ni nchi ya Marekani. Kati ya maraisi wake 44, ni maraisi 4 tu ambao wanaonekena kuwa walikuwa bomu (hii ni kwa kulinganisha tafiti na statistic mbalimbali). Hivyo wana asilimia hizi: marais wazuri 91% kwa wabovu 9%. Kwa hivyo wana maraisi 40 ambao kwa ujumla walikuwa wazuri na kati ya hao 40 kuna "exceptional genius" kadhaa kama Abraham Lincoln, Roosevelt, Reagan nk.

Angalia Tz, marais 4, wawili bomu, mmoja ni utata mtupu. Hivyo basi wabovu 75% na 25% mwingine (probably above average). Yaani maendeleo katika rate hiyo ni ndoto.
 
Back
Top Bottom