Kibona
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 1,023
- 652
Mbona mie siwaelewi, hivi mnaongelea outside world ipi? kwa mfano Msumbiji hawajui kiingereza kabisa bora hata sie lakini mbona hawaoti kabisa kuamua kutumia kiingereza? nchi kama vile Korea, nchi za marekani ya kusini, Guinea, Ufilipino, vietnam hawajui kiingereza mbona naona bado hawawazi kuanza matumizi ya kiingereza? Tusidanganyane bwana watanzania kukosa exposure sio kwasababu ya lugha ni kutokana na mfumo ovyo wa ccm tangu zamani. nchi inaenda kwa propaganda na hivyo wananchi wamejaa hofu ktk kila kitu kiasi kwamba huwa hawathubutu kabisa. Nikupe mfano; kuna watanzania wengi wamekuwa wakizamia Afrika ya kusini huku hawajui kabisa kiswahili lakini wanaweza kufika na kufanya biashara hata kama wanakua wahamiaji haramu, sasa hao wanawezaje kama kiswahili ndo tatizo?Kiswahili ni kizuri lakini kimedumaza sana watanzania to the outside world. Leo hii watu wanahitimu shahada zao hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza kilicho nyooka hapana. Nenda kawaweke wahitimu wetu na wa Ug na Kenya kwenye labour market wafanyiwe usaili utaona tunashindwa badly. Let us be honest jamani, achilia mbali EAC! Ni lini humu nchini watu wameomba kazi kwa Kiswahili? Ama umeenda usaili unaofanywa kwa kiswahili kwenye nyadhifa muhimu? Jibu hapana!
Mimi nafikiri, kama tayari tunakifahamu Kiswahili kwa ustadi kabisa kwanini basi tusihamie kujifunza lugha nyingine na kuitumia? Kwanini tung'ang'anie tu Kiswahili na tunakijua?
Kwa wale wanaotembea na kutafuta ajira ng'ambo wanaweza kukubaliana nami kuwa Nchi zote za kiarabu hususan U.A.E ( Umoja wa Falme za Kiarabu yenye Dubai na Abudhabi----), Qatar na nyinginezo zimetoa ajira sana kwa waafrika wengi wao wakiwa wakenya.
Hawa jamaa wako kila mahari mpaka karibuni wanafanya kazi kama walinzi ama security guard wakiwareplace wahindi na wapakistan, lakini kwanini waajiri wanawataka? Jibu kiingereza sababu kazi nyingine haziitaji elimu kubwa huko middle east bali ufahamu tu wakiingereza na wanaajiriwa. Sasa sisi bado tunalalamika - ni ujinga tu.
Jamaa wanaenda na wanaita ndugu zao, wako mahotelini mpaka top hotels in town wapo! Sisi twang'ang'ana na Kiswahili, jamaa wanaanza na security guard kesho unamuona ameingia sales keshokutwa anafanya jambo lingine! Tukisubiri serikali itufanyie tutabaki kulalama pasipo msaada!
Anyway let us wake up and run badala ya kuendelea kupiga mayowe ya usingizi wakati mda umeshasogea!!!