Tanzania tumepigwa bao na Wakenya, Kiswahili is not the official language of EAC!

We should dare face it once and for all ... Kazi ya kiswahili kama lugha moja ya Taifa ... Imeshafanyika .... imemalizika na kutufikisha mahali ..hatuwezi kuendelaea bila lugha ya kiingereza kupewa umuhimu sawa na Kiswahili...!!

Mawazo ya kikoloni mpaka kwenye mishipa ya damu

Tunaweza kuendelea bila kiingereza kwani kiingereza si ardhi, watu, siasa na uongozi bora.
 
wakiingia na wasudani a kusini watataka lugha zao hahaha itanogaje hiyo,,,,then ili upate uwakilishi huko ujue lugha walau 3
 
Sasa unayemlalamikia ni yule aliyekataa kukitumia au yule ambaye alipendekeza akakataliwa? Kama Kenya wanakizungumza vizuri lakini wamekataa kukitumia then sisi tuna lawama gani? Labda baada ya muda watu wataona umuhimu wa kiswahili na kubadilisha mawazo, lakini sioni tulichoathirika kwa uamuzi huu.
Sijaona mahali kuwa Kenya imekataa Kiswahili kitumike kama lugha rasmi. Ninachoona ni ukosefu wa uongozi katika upande wetu kutetea au kuhimiza Kiswahili kitumike kama lugha rasmi. Sidhani tungepata upinzani kutoka kwa Kagame. Sidhani tungepata upinzani kutoka kwa Mu7.
Sidhani tungepata upinzani kutoka kwa Kibaki. Na ukiangalia upesi upesi kama ni kura Kiswahili kingekubalika.
 
Hii nchi ya ajabu sana tena inafaa kupigiwa kura iingiye katika maajabu ya Dunia
1. Wananchi wake hawajui Kiswahili wala Kiingereza
2. Watu wake wanatetea kiswahili lakini watoto wao wote wako English Medium, tusiotetea kiswahili watoto wetu wapo shule ya msingi vingunguti
3. Serikali yake haijulikani kama inaendesha shughuli zake kwa lugha gani, mafaili yamejaa kiswakinge kitupu
4. Rasimu ya muswada wa kuandaa katiba iliandikwa Kiingereza, mikutano ya kutoa maoni iliendeshwa kwa kiswahili
5. Bunge linaendesha mijadala ya kutunga sheria kwa kiswahili, Sheria iliyotungwa inakuwa katika English
6. Website za Wizara zote zimeandikwa kwa Lugha ya Kiingereza, wakati Rais katangaza Wizara zote kwa Kiswahili
7. Tunatekeleza miradi ya kuondoa umasikini kwa kiswahili, miradi yenyewe imeandikwa kiingereza
8. Mwalimu anasomea Diploma kwa Kiingereza, lakini anaenda kufundisha shule ya msingi kwa Kishwahili
9. Mwalimu wa somo la English, darasani anafundisha kwa kiswahili
10. Mwenyewe ni sangoma wa Korogwe, ndani ya hata videge vya Precission vyenye wahudumu watanzania anatoa order ya maji eti waler!(water)
11. Hospital Daktari anakuuliza ugonjwa kwa kiswahili, dose anakuandikia kwa kiingereza

....................orodha haishii hapo, yaani ni vurugu mechi tu hii nchi. Hebu ndugu zangu tuwe serious, Kiswahili tunachoongea ni cha hovyo kuliko tunavyoongea kisukuma cha ukereweni, tujiulize suali hili. Tutakosa nini ikiwa tukianza kujifunza nakuendesha mambo yetu yote kwa kiingereza from nursery to the parliaments. Ikiwa hoja kiswahili kitakufa, mbona kinyamwezi na kinyagatwa nk havijafa pamoja na juhudi kubwa za kueneza kiswahili. Believe me kama tanzania itaanzisha approach ya kiingereza for everything, Kenya tunaotishika nao tutawaburuza kama watoto hao. Eti force=Kani, huku anasoma acceleration akirudi kuwa mwalimu then anamfundisha mwanafunzi mchapuko-shame on us!
 
Mawazo ya kikoloni mpaka kwenye mishipa ya damu

Tunaweza kuendelea bila kiingereza kwani kiingereza si ardhi, watu, siasa na uongozi bora.

Tunaweza kuendelea bila kingereza kabisa hilo halina shaka ... Mimi naona tatizo kubwa ... Ni nani wakutuogoza kufikia hapo!! Ni viogozi gani hao wenye kujiamini na wenye mantiki sahihi vichwani na kwenye vinywa vyao ...kutuogoz akifua mbele kufikia hapo ...wote waliobaki ..hawajui hata wanachotaka ...hicho ..wanachotaka wataikifikiaje. Nani mwenye kujiamini kwa dhati ya moyo na fikra leo hii tanzania anaweza ..kutetea kiswahi kama lugha ya kuifikisha tanzania kunakotakiwa ndani ya utandawazi unaoitawala dunia...!! Kwa hiyo ni kweli tunaweza kuendela bila kingereza...?
 
Ama hakika, utumwa ulikuja na mengi sana...
Mnataka kuona reality? ondoeni matumizi ya lugha ya kiswahili JF kibakie kiingereza kisha mtaona matokeo..

Mkuu Mkandara ..

Kiswahili kinahitaji ... Wa Kukisimamia ... Kukitetea... Kukisimamia si kama Lugha tu ..lakini na tamaduni zote za nidhamu na mausiano sahihi ya kijamii ..kwa sasa hayupo...
 
hapa tumeshindwa,sasa sijui ile kampeni ya umoja wa Afrika (AU) tutaweza kukifanya kiswahili ndio lugha ya Afrika.?
 
Kiswahili ni kizuri lakini kimedumaza sana watanzania to the outside world. Leo hii watu wanahitimu shahada zao hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza kilicho nyooka hapana. Nenda kawaweke wahitimu wetu na wa Ug na Kenya kwenye labour market wafanyiwe usaili utaona tunashindwa badly. Let us be honest jamani, achilia mbali EAC! Ni lini humu nchini watu wameomba kazi kwa Kiswahili? Ama umeenda usaili unaofanywa kwa kiswahili kwenye nyadhifa muhimu? Jibu hapana!
Mimi nafikiri, kama tayari tunakifahamu Kiswahili kwa ustadi kabisa kwanini basi tusihamie kujifunza lugha nyingine na kuitumia? Kwanini tung'ang'anie tu Kiswahili na tunakijua?
Kwa wale wanaotembea na kutafuta ajira ng'ambo wanaweza kukubaliana nami kuwa Nchi zote za kiarabu hususan U.A.E ( Umoja wa Falme za Kiarabu yenye Dubai na Abudhabi----), Qatar na nyinginezo zimetoa ajira sana kwa waafrika wengi wao wakiwa wakenya.
Hawa jamaa wako kila mahari mpaka karibuni wanafanya kazi kama walinzi ama security guard wakiwareplace wahindi na wapakistan, lakini kwanini waajiri wanawataka? Jibu kiingereza sababu kazi nyingine haziitaji elimu kubwa huko middle east bali ufahamu tu wakiingereza na wanaajiriwa. Sasa sisi bado tunalalamika - ni ujinga tu.
Jamaa wanaenda na wanaita ndugu zao, wako mahotelini mpaka top hotels in town wapo! Sisi twang'ang'ana na Kiswahili, jamaa wanaanza na security guard kesho unamuona ameingia sales keshokutwa anafanya jambo lingine! Tukisubiri serikali itufanyie tutabaki kulalama pasipo msaada!
Anyway let us wake up and run badala ya kuendelea kupiga mayowe ya usingizi wakati mda umeshasogea!!!
 
Lowassa: nimesikitishwa sana, lugha yetu imedhalilishwa sana, tumeaibishwa sana, serikali ni lazima ilivalie njuga jambo hili, na kiswahili kiwe ofisho langweji ya afrika mashariki.

Sitta: aah..mimi ni waziri mgeni tu katika wizara ya afrika mashariki...hili swala ni zito kidogo...nawaahidi watanzania nitalifuatilia kwa nguvu zangu zote kuwashughulikia mafisadi wote waliohusika na njama hizi.

Pinda: siyo kweli, au rais wetu atakuwa amedanganywa kuhusu jambo hili.

Kikwete: kelele za milango yote ya afrika mashariki hazininyimi usingizi. Someni kwa bidii mjue kinyamwezi, maana kenya nao wangesema ooh na sisi kijaluo je? Uganda nao wangetaka kibaganda, na rwanda kitutsi...english is a very common language, so take care my friends.
 
Watu bwana,sasa kiingereza kikitumika kina matatizo gani?mnataka kufananisha kiswahili na kihisipinyiola au kifaransa?
Kila wakati inferiority complex zinatusumbua, hovyo!!
 
Watu bwana,sasa kiingereza kikitumika kina matatizo gani?mnataka kufananisha kiswahili na kihisipinyiola au kifaransa?
Kila wakati inferiority complex zinatusumbua, hovyo!!
Mama naona mwenye inferiority complex ni wewe. Maana hapa unakiweka Kifaransa na Kihispania juu ya Kiswahili. Kwamba haviwezi kuwa kwenye mizani sawa.
 
Kiswahili ni kizuri lakini kimedumaza sana watanzania to the outside world. Leo hii watu wanahitimu shahada zao hata kuandika barua ya kuomba kazi kwa kiingereza kilicho nyooka hapana. Nenda kawaweke wahitimu wetu na wa Ug na Kenya kwenye labour market wafanyiwe usaili utaona tunashindwa badly. Let us be honest jamani, achilia mbali EAC! Ni lini humu nchini watu wameomba kazi kwa Kiswahili? Ama umeenda usaili unaofanywa kwa kiswahili kwenye nyadhifa muhimu? Jibu hapana!
Mimi nafikiri, kama tayari tunakifahamu Kiswahili kwa ustadi kabisa kwanini basi tusihamie kujifunza lugha nyingine na kuitumia? Kwanini tung'ang'anie tu Kiswahili na tunakijua?
Kwa wale wanaotembea na kutafuta ajira ng'ambo wanaweza kukubaliana nami kuwa Nchi zote za kiarabu hususan U.A.E ( Umoja wa Falme za Kiarabu yenye Dubai na Abudhabi----), Qatar na nyinginezo zimetoa ajira sana kwa waafrika wengi wao wakiwa wakenya.
Hawa jamaa wako kila mahari mpaka karibuni wanafanya kazi kama walinzi ama security guard wakiwareplace wahindi na wapakistan, lakini kwanini waajiri wanawataka? Jibu kiingereza sababu kazi nyingine haziitaji elimu kubwa huko middle east bali ufahamu tu wakiingereza na wanaajiriwa. Sasa sisi bado tunalalamika - ni ujinga tu.
Jamaa wanaenda na wanaita ndugu zao, wako mahotelini mpaka top hotels in town wapo! Sisi twang'ang'ana na Kiswahili, jamaa wanaanza na security guard kesho unamuona ameingia sales keshokutwa anafanya jambo lingine! Tukisubiri serikali itufanyie tutabaki kulalama pasipo msaada!
Anyway let us wake up and run badala ya kuendelea kupiga mayowe ya usingizi wakati mda umeshasogea!!!

Njomoli ,

Kwangu Mimi huu ni mtizamo sahihi,

Niongezee tu kuwa sidhani kama kuna mtu anaweza kukibeza kiswahili hasa kwa kazi ambayo kimetufanyia kama taifa.Umuhimu wa lugha unakuja pale unapoitafiti na kuiona kuwa imetumika kuleta mafanikio gani ya kijamii na kiuchumi. Kiswahili kimmetumika kutuuunganisha na kutupa uhuru, kimefanikisha umoja wa kitaifa, uzalendo na kujenga Utanzania ..mambo ambayo niwazi hasa ukilinganisha na nji za jarina. Kiswahili kimetumika kusaidia nchi za jirani kupigania na kujitwalia Uhuru ...kwa hiyo huwezi kusifia lugha bila kuonyesha thamani yake kwenye jamii. ...Hivyo Kiswali kimetumika kufanikisha yote hayo ..hivyo kwanba ..yeyote anagweza kujifunza bila aibu yeyote lugha hii ya kiswahili ...kwani matunda yake yanonekana. Na aliyekipa kiswahi THAMANI YAKE wote tuna mjua... Hiwezekani tu .. Kiswahili ni Ligha changa ..Lakini JK Nyrere alikipa heshima kwani alikitumia kufanya mambo ya heshima na ya ubinadamu.

Sasa tuangalie swala la utandawzi ... ni kweli kiswahili hakitatusaidia sana hapo ..sababu haina sifa na uwezo wa kubeba jukumu hilo kwa uchanga wake ...Hivyo ni jambo la busara ...Kutokujifanya vipofu na kuendelea kukinganaina inapofika kwenye swala la ajira kwa afrika ya mashariki na kimataifa.

Jambo lingine ni kuwa heshima ya thamani ya kiswahili inapwaya kulingana na kile ambacho ilikwisha kifikia na sasa kinaangaka. Kiswali ndio iljenga Utu na misingi ya Chama cha TAA na TANU .... KIMSINGI KISWALI KINASIMAMIA NA KUJIKUTA KUTANGAZA NA KUSAMBAZA ..UTU NA UBINADAMU KWA NCHI ZA JARANI ....KISWAHILI hakinedani kabisa na UFISADI ...kwani hakikuwahi kubeba jukumu hilo kwenye historia yake....

Ili sifa ya kiswhahili iendelee kudumu na kubakia kwenye sifa yake na mataifa yote kukienzi ..Chama tawala na serekali yake irejee misingi ya Utu na ubinaadamu kama bidhaa rasmini inayobebwa an lugha ya kiswahi!!
 
Azimio Jipya,
Kwanza kabisa nitoe shukurani zangu za dhati kwakuweza kuandika tena ingawaje sikuwa nimekujibu lakini naamini utanielewa si mda mwingi nautumia kwenye mtandao!

Umeeleza sawia kabisa thamani na faida ya Kiswahili kwa jamii ya watanzania pamoja na jirani zake wa Afrika ya mashariki na kati na popote lugha hii adhimu inapozungumzwa. Ni busara pia kukubali kama vile ulivyosema kuhusu Mwl. Nyerere ambaye halikitambulisha na kukiongezea nguvu ili kipate kutambulikana.

Nimekuwa nikifikiri wakati fulani ingawaje haya ni mafikara yangu tu waweza nirekebisha ninapoenda kombo kuhusu uchumi wa nchi zetu na lugha hii.

-Naamini kabisa kama taifa la Tanzania lingekuwa lenye uchumi mkubwa kama wa Kirusi, Kifaransa ama Kiiengereza uendelezwaji wa lugha hii ungekuwa mkubwa;
Kwa mfano - utambulisho (identity) wa nchi unatokana na lugha pia, kila lugha yeyote Duniani inapozungumzwa watu huyakumbuka mataifa yanayo zungumza lugha hiyo. Ndiyo maana wafaransa na waingereza hawana mchezo juu ya kuziendeleza lugha zao na kuchangia muendelezo wa lugha hizi kwenye nchi mbalimbali ili kuendelea kujitangaza na kujitambulisha.

Kwa mantiki hiyo basi, nasi pia lugha hii imetusaidia lakini hatujaenda mbali sana kulingana na uchumi wetu. Kwasababu kila mtu anakimbilia kujifunza lugha hizi kubwa hususani Kiingereza kwa sababu za utandawazi, kama nchi yetu ingekuwa nitaifa lenye uchumi mkubwa kama vile Uchina ni nani ambaye angetuzuilia hata kwa jina la utandawazi kuendelea kuitambulisha lugha yetu hii.

Lakini hivi leo uchumi wetu unalazimisha kujifunza na kutilia maanani lugha hizi hasahasa Kiingereza, Dunia ya leo huju kiingereza unapata shida kweli kweli lakini kama tungekuwa tumejitosheleza kiutaalamu, kisayansi na kiteknolojia pamoja na kiuchumi tungekuwa tunatoa ajira zetu wenye kiasi ambacho hatutoweza tetereka kama tukinyimwa kazi penginepo kwasababu ya lugha. Ndio maana Wachina hawababaishwi na kutokujua kwao lugha kama unataka kuwajua vyema utajifunza tu lugha yao na vivo hivyo warusi.

Kwahiyo ndio kusema utandawazi unatusukuma lakini hasa uchumi wetu. Kama uchumi wetu ungekuwa unatutosheleza na tunaweza toa ajira zakutosha kwa watu wetu wanaofikia takribani milioni 40 utandawazi ungekuwa lolote si chochote.
Wacha niishie hapa wakati mwingine.

Heri ya mwaka mpya!
 
Mkuu mbona hii ni aibu. Yaani AU imekifanya kiswahili moja ya Lugha zake na tukawa tunadhani kwamba Ban Kimoon atatusaidia kikiweka huko UN. Sasa kama siyo lugha ya haka kakipande ketu ambapo inajulikana ndiyo mama wa kiswahili, so kuna hatari kwamba hata AU wataifuta achilia mbali UN! Kiswahili ndio ingekuwa utambulisho wa EAC, sasa kama siyo EAC itakuwa na utambulisho gani?
 
mitanzania mingi inapenda kiswahili maana IQ ya kujua kiingereza haina.mnaniboa.na hata mijitu ya vyuo ni mijinga.someni novels basi.rwanda na burundi wanaongea kifaransa sasa wameongezewa kiswahili na kiingereza hawalalamiki.

mbona una kauli mbaya mkuu? kwani wewe si mtanzania? watu wanalalamika kwa hoja iweje wewe unatoa matusi? kama hujakubaliana na kulalamika kwao pinga kwa hoja si matusi.
 
Nimecheka sana hii post hasa 9 na 11 Duu hii nchi kweli inabidi iingie kwenye kitabu cha Mwajabu ua Dunia
Hii nchi ya ajabu sana tena inafaa kupigiwa kura iingiye katika maajabu ya Dunia
1. Wananchi wake hawajui Kiswahili wala Kiingereza
2. Watu wake wanatetea kiswahili lakini watoto wao wote wako English Medium, tusiotetea kiswahili watoto wetu wapo shule ya msingi vingunguti
3. Serikali yake haijulikani kama inaendesha shughuli zake kwa lugha gani, mafaili yamejaa kiswakinge kitupu
4. Rasimu ya muswada wa kuandaa katiba iliandikwa Kiingereza, mikutano ya kutoa maoni iliendeshwa kwa kiswahili
5. Bunge linaendesha mijadala ya kutunga sheria kwa kiswahili, Sheria iliyotungwa inakuwa katika English
6. Website za Wizara zote zimeandikwa kwa Lugha ya Kiingereza, wakati Rais katangaza Wizara zote kwa Kiswahili
7. Tunatekeleza miradi ya kuondoa umasikini kwa kiswahili, miradi yenyewe imeandikwa kiingereza
8. Mwalimu anasomea Diploma kwa Kiingereza, lakini anaenda kufundisha shule ya msingi kwa Kishwahili
9. Mwalimu wa somo la English, darasani anafundisha kwa kiswahili
10. Mwenyewe ni sangoma wa Korogwe, ndani ya hata videge vya Precission vyenye wahudumu watanzania anatoa order ya maji eti waler!(water)
11. Hospital Daktari anakuuliza ugonjwa kwa kiswahili, dose anakuandikia kwa kiingereza

....................orodha haishii hapo, yaani ni vurugu mechi tu hii nchi. Hebu ndugu zangu tuwe serious, Kiswahili tunachoongea ni cha hovyo kuliko tunavyoongea kisukuma cha ukereweni, tujiulize suali hili. Tutakosa nini ikiwa tukianza kujifunza nakuendesha mambo yetu yote kwa kiingereza from nursery to the parliaments. Ikiwa hoja kiswahili kitakufa, mbona kinyamwezi na kinyagatwa nk havijafa pamoja na juhudi kubwa za kueneza kiswahili. Believe me kama tanzania itaanzisha approach ya kiingereza for everything, Kenya tunaotishika nao tutawaburuza kama watoto hao. Eti force=Kani, huku anasoma acceleration akirudi kuwa mwalimu then anamfundisha mwanafunzi mchapuko-shame on us!
 
Acha tupigwe bao, mwisho wa siku kiswahili chenyewe hakina 'dili'. Raia wanakosa kazi kwa sababu wanashindwa kujielezea vizuri kwenye interview za kiingereza, na asilimia kubwa ya post za kazi unaambiwa uwe fluent kweny English so hapo kiswahili bado kina maana gani kuwa official EAC language
 
Back
Top Bottom