Elections 2010 Tanzania Tumebakiwa na Hii Tu Kwa sasa!!

CAMARADERIE

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,419
1,920
Hiki nikikiona tu hufarijika kidogo......na kusahau mengine...otherwise aargh

tanzania.jpg
 
Heri wewe unapata faraja..........

mimi nikiona hiyo NJANO hapo nachanganyikiwa na kuumwa zaidi kwa sasabu kuu mbili

1: CHICHIEMU
2: Madini yetu na ndugu zetu wanaopoteza maisha yao na mali zao walizotegemea miaka nenda rudi huku hao hao CHICHIEMU na mibw...na yao ikifaidi damu za ndugu zetu kwa kuota mitumbo

Naona Muunganiko wa njano hii na ile ya CHICHIEMU na najisikia uchungu sana

Hiyo NYEUSI nayo mkuu inantoa machozi sana............fahari ya mtu mweusi imepotea,.....hatuthaminiwi tena na weusi wenzetu mbele ya weupe......hawa wamekuwa na kauli kwa weusi wenzetu ambao wametuuza na hata wao wenyewe wamejiuza hawana sauti tena. Ukikaa wewe mweusi (hapa kwa tafisri ya uzawa wa kiafrika na sio ubaguzi wa rangi) na wakuja kutoka nje kwenye mizani moja ni lazima ile kwako.................wanawakabidhi kila kilicho chetu na kutuacha watupu kwenye nchi yetu

Hapa ndipo ninapomkumbuka Mwalimu anaposema tutaondoa wakoloni hawa (weupe) lakini tusipokuwa makini wataibuika wakoloni weusi watakaokuwa hatari zaidi ya hawa tunaowaondoa

Hii ni kwelii............tuliwaondoa kwa kuwa wanaiba kwetu na kuwekeza kwao bara ulaya.......lakini leo haya majikoloni meusi yanaiba huku kwao waliko bibi zao, mama zao, wajomba zao, shangazi zao n.k kisha wanaenda kuwekeza ulaya (kule kule tulikokataa pesa zetu na mali zetu zisiende) ambako hakuna ndugu zao zaidi ya mabw...na zao.......je haya yanayotelekeza ndugu zao na kuweka fedha zao mabilioni (samahani namaanisha vijisenti) sio wabaya kuliko wale wa awali?

Nahisi machozi kunitoka ninapoitazama bendera ya nchi yangu na kuangalia ile picha niliyofundishwa shule ya msingi juu ya Tanzania yangu iliyojaa madini kila kona na rasilimali nyingine nyingi adimu........NAKULILIA TANZANIA YANGU na ninapoanza kuimba ule wimbo "TANZANIA TANZANIZA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE" basi huanguka kilio kiso kifani kwa uchungu.....hata hivyo bado nakupenda Tanzania kwa kuwa wewe ni mwema ila haya majambazi kadhaa yanaharibu sifa yako njema
 
Hiyo rangi ya njano wanavyoigaragaza, inatia huruma. Kama tumeshindwa kulinda rasilimali zetu ni bora tufute rangi kadhaa kwenye bendera yetu.
 
Naelewa hayo...nafarijika kuwa hawajaichakachua tu...au kuiuzilia mbali...sijui iko patented?
 
Back
Top Bottom