Tanzania tuko kwenye feudalism!

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
4,973
15,304
Nimejaribu kufanya tathmini ya maisha tunayoishi watanzania wa leo nikajaribu kukumbuka somo la historia na nimegundua system ya maisha na uongozi wetu unafanana kwa kiasi kikubwa na middle ages (miaka ya 1400) kule ulaya. Kipindi hicho, watawala walikua wanawagawia mashamba marafiki zao (feudal lords) ambao nao waliyatumia kuwanyonya wanyonge. Viongozi na watawala walitajirika kwa kujilimbikizia mali zilizotokana na kodi za wananchi wanyonge hivyo kuwawezesha kuishi maisha ya kifahari! Enzi hizo, hakukuwa na demokrasia na wale wote walioonekana kupingana na utawala walikiona. Sasa fananisha na viongozi wa tz, tafakari, chukua hatua.
 
ukisema hivyo unakosea. Sasa tuko kwenye ubepari chotara. Sasa kuna viwanda, ubinafsishaji, soko huria, kumiliki mali, n.k. Kadhalika ndani yake kuna mfumo hafifu wa ujamaa. Bado watanzania tunajaliana sana. Hakuna mambo ya rent in kind karne hii
 
However said that we produce what we dont consume and consume what we dont produce hit the nail on the head. This coupled with runaway corruption explains our poverty.
 
ni vigumu sana kutambua tuko kwenye stage gani kwani ukichunguzi kwa umakini tabia za mifumo yote ya maedeleo tunayo kuanzia slave mode mpaka ubeberu upo tz
 
ukisema hivyo unakosea. Sasa tuko kwenye ubepari chotara. Sasa kuna viwanda, ubinafsishaji, soko huria, kumiliki mali, n.k. Kadhalika ndani yake kuna mfumo hafifu wa ujamaa. Bado watanzania tunajaliana sana. Hakuna mambo ya rent in kind karne hii
Mkuu tembelea mikoani rent in kind ipo tene kwa kiwango kikubwa
 
Back
Top Bottom