Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,804
- 1,871
Habari kuwa tatizo la umeme Tanzania ni sugu, sikulipokea kwa mshangao hata kidogo. Picha ya tatizo hili nililielewa pale Rais mstaafu Mwinyi akiwa madarakani, alipolieleza tatizo kama limetokana na upingufu wa maji katika mto Ruvu. Ama wengine wakaeleza kuwa matope yamejaa katika mto huo. Yote hayo kwangu yalikuwa ni majibu ya kisiasa.
Katika nchi zilizoendelea asilimia 80 ya umeme wao hutokana na Nuclear energy. Na katika chanzo hicho cha umeme ndio unaaweza kupata umeme rahisi na imara. Ni kitu cha ajabu sana hawa hawa watu wanapokuja kueleza maaendeleo katika nchi zetu, hufurahia tu pale wanaposema 5% tu ya watanzania wana acces ya umeme. Lakini kuja na maelezo ni jinsi gani wao waliondokana na adha hiyo hawapendi kabisa kujadili. Lazima tujiulize ni kwanini? Je wanatutakia mema?
Pindi nchi zinazoendelea zinapojitosa katika Nuclear power, basi zitasakamwa na kutishiwa kupigwa mabomu. Iran ni moja kati ya nchi zinazoendelea ambazo hazikujali vitisho, na bila majadiliano ikajenga mtambo wa Nuclear kwa matumizi ya amani. Sakata lake limechukua zaidi ya miaka 20, kusakamwa na kutishiwa kila leo. Kibaya zaidi ni kuona nchi zinzoendelea zikaungana mkono na nchi zilizoendelea kama Marekani, Israel na Uingereza kuisakama Iran. Eti kisa ni kutoiruhusu Iran kuwa na Bomu la Nuclear. Lakini "National Convention On Nuclear Power" imeweka wazi katika Article 1, kama ninavyoinukuu hapa chini:
"ARTICLE 1. OBJECTIVES
The objectives of this Convention are to:
a. Accelerate the expansion of nuclear power in industrialized nations
and in the developing areas of the world;
b. Assure that peaceful uses of nuclear energy do not further the
proliferation of nuclear weapons, by providing assured supplies of
specified goods and services including those capable of supporting
the proliferation of nuclear weapons;
c. Protect against nuclear terrorism involving the potential sabotage of
nuclear installations or transport systems or the theft of nuclear
material or hazardous radioactive materials; and
d. Maintain high safety standards and efficiency and operational
performance."
Soma convention nzima katika www.pysics.havard.edu/~wilson/energypmp/nuclear-forum.pdf
Soma vizuri hicho kipengele "b" kimeeleza wazi kuwa kuwa kila nchi duniani ina haki ya kuwa na Nuclear Energy kwa matumizi ya amani. Sasa iweje hawa hawa wakubwa walioandika hii convention wanaipinga na nchi nyingine sizizoendelea nazo eti zinaunga mkono licha ya kufahamu kipengele hicho.
Mimi nafikiri, nchi zisizoendelea ni lazima zishikamane kuiunga mkono Iran na kuzishinda nchi zilizoendelea. Kama Iran ikifanikiwa basi itakuwa rahisi kwetu kuleta ajenda kama hiyo na ikapita. Kuiunga mkono Iran, hatutafanya hivyo kwa faida ya Iran, bali kwa Faida yetu wenyewe. Waswahili wanasema, mwenzako akinyolewa wewe tayarisha kichwa chako. Kwa hiyo kabla hatujatayarisha vichwa vyetu ni lazima tuhakikishe kuwa kichwa cha Iran hakijanyolewa.
Tatizo la umeme Tanzania na nchi nyingine za Afrika litatoweka pale Afrika tutapokuwa na umeme utokanao na Nuclear. Nchi nyingi za Afrika kama Kenya, Uganda, Angola n.k zimeshaanza kudokeza hayo katika level ya kitaifa. Lakini lazima ieleweke kuwa hiyo sio kazi rahisi, si katika kuipata Teknolojia hiyo bali kwa nchi mabeberu kutukubalia. Na hii itawezekana pale nchi zote zinazoendelea kuwa na lao moja katika hili la Nuclear Energy kwa matumizi ya amani.
Nilitarajia katika mkutano wa UN safari hii, mwenyekiti wa African Union angeliongelea hili, lakini haikuwa hivyo. Ninamuelewa Gadafi anapopata frastratio na kichefu chefu akiisoma Charter ya UN na kuichana na kuitupa. Hii ni kwa sababu Charter hiyo ina double standards. Hiyoa haiwezi kutufujisha popote pale.
Tuungane kupigania kupata Nuclear Energy kwa matumizi ya amani, ili tukuze uchumi wetu. Huwezi kumuita muwekezaji katika hali ya umeme wa mgao. Hapa hatupo makini.