TANZANIA TUITAKAYO.... TBC na SERIKALI VYAHUSIKA

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
[h=6]TBC anzisheni CHANNEL YA TBC BUNGE [ yaani mambo ya bunge tu mwanzo mwisho, zaidi ya hapo majimboni, vikao vya kamati za bunge kama hakuna BUNGE? ]
Mbona channel za MUZIKI wanaweza hali wakijiendesha kwa kodi zetu? Kwa nini tuweka mambo ya MUZIKI mbele kwenye chombo cha serikali [MIZIKI YENYEWE YA KIKONGO ] wakati kuna mambo kama ya BUNGE na shughuli za majimbo havina nafasi?
Kama tusipoweka vipaumbe vyetu sawa, tutaendelea kuchechemea na kunyumba kimaendeleo pamoja na kunyima watu nafasi ya kupata taarifa muhimu hasa za bunge, ni lazima tuwe na uwezo wa kujua neno kwa neno ya kile kinachoendelea bungeni muda wote wa kikao.
Bunge lipewe channel yake hapo TBC na iwe na kazi hiyo tu, likianza DODOMA hakuna kukata mwanzo mwisho na likimalizika shughuli za kamati ziwe zinarushwa hewani, hakuna siri ya kuficha,
Itafungua wananchi zaidi na itakuza utendaji wa bunge, pia itaongeza uelewa na upatikanaji wa taarifa za bunge kwa wananchi, kitu ambacho ni muhimu sana kwa lolote taifa.
[/h]SOURCE : CHANGE TANZANIA GROUP ON FACEBOOK
Log In | Facebook
 
Tusimamia misingi ya upatikanaji taarifa muhimu wa wananchi, bunge ni kama tunamelipoteea wakati ni kikao muhimu sana,
 
Bunge limejaa mipasho ya Sendeka na Kilango,ubabe wa Anne Makinda....wanaoafiki waseme ndioooooooo! Bola muziki wa zamani wa wakongo!
 
Bunge limejaa mipasho ya Sendeka na Kilango,ubabe wa Anne Makinda....wanaoafiki waseme ndioooooooo! Bola muziki wa zamani wa wakongo!

hao wanaofanya mipasho tunawajuaje katika jamii kisha kuwakataa?
watu wanatakiwa kuwasikia kwa masikio yao, hii ni muhimu sana katika ujenzi wa taifa, hasa upatikanaji wa habari.
WRONG + WRONG IS NO RIGHT
 
mawazo yako ni mazuri mkuu lakini hii tbc haiwezi kufanya kitu kama hicho kwani siku hizi hawapendi hata bunge kwani wanajua serkali yao na wabunge wao wa CCM watahaibika kutokana na ukilaza wao na jinsi walivyo na hoja nyepesi na majibu mepesi kwenye mambo na hoja za muhimu.
 
Back
Top Bottom