Tanzania: Tuimejipanga vipi kufidia mapengo ya wataalam wakongwe wanaostaafu?

Ramthods

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
515
186
Leo katika tembea tembea zangu, nimepitia tovuti ya Inter-Consult nikakutana na news article kuwa aliyekuwa Mkurungenzi wa Inter-Consult Eng. Mark W. Njiu amestaafu baada ya kufikisha miaka 60.

Kwa wale wanaomfahamu Mark. W. Njiu wa Inter-Consult, ile kampuni ya ma engineers pale pembeni na millennium towers, hili jembe la Civil engineering limestaafu na kulazimika kuachia cheo cha ukurugenzi wa kampuni, baada ya kufanya kazi na Inter-Consult kwa zaidi ya miaka 30 kama Civil Engineer.

Swali la kujiuliza watanzania hapa ni je tumeandaa wakina Njiu wa miaka ya mbele?

Naona kama wataalam wanapungua, madaktari bingwa, ma professor etc na sina uhakika kama tuna watu walioandaliwa kufidia mapengo ya wazee kama hawa.

Hii ni changamoto kwa taifa, na sina uhakika kama tumejipanga katika hili.

Kwa taarifa kamili, bofya hapa: Inter-Consult Ltd | Top Management Change

Tanzania yangu naipenda.

Ram
 
Back
Top Bottom