Mzee Mbegu
Member
- Jul 5, 2010
- 47
- 10
Wana JF,
Mimi nina wasiwasi mkubwa kwamba kama raia kwa ujumla wetu tumepoteza uwezo wa kufanya upembuzi wa jambo lolote la kijamii bila ya kuweka personal or political bias zetu pembeni. Naombea kwamba pengine hili ni tatizo tu hapa JF, na sio huko kwenye kaya zetu. Hivi kwa nini tumeishia kujitazama kwamba sisi (au kundi la watu fulani) ndio lina haki ya kutoa maoni, na maoni yao ni sahihi zaidi wakati ya wengine wote ni ya kuwadharau tu kwavile wametoka ukoo fulani maarufu?
Nadhani Thuwein Makamba ana haki ya msingi kusikilizwa bila ya hoja zake kupindishwa. Hivi ukiishi nje ya nchi zaidi ya miaka 5 na umetembelea nyumbani kwa siku 90 tu kati ya hizo, maana yake ni kwamba umepoteza haki na uhuru wako wa kikatiba kujadili yanayotokea nyumbani? Wangapi humu JF hamjarudi nyumbani zaidi ya miaka 10 na bado mnajazba kuchangia hoja za nyumbani? Katiba ile ile ambayo wengi wenu mnapigania kwa maslahi ya wengine mnaminyia huyu kijana Thuwein! Kama hoja zake hazifai, basi hazifai on merit, sio kwa vile tu eti ni mtoto wa Mzee Makamba. Yeye akitoa maoni yake basi lazima anayo hidden agenda. Jiulize wewe mwenyewe huwa una maslahi binafsi katika kila jambo unalolisema? Haiwezekani. Kwanza huyu jamaa ameanza mada yake kwa kutoa full disclosure kwamba Kikwete ameteua watu ndani ya familia yake kushika nyadhifa. Wangapi humu ndani mkitoa maoni yetu mnatoa disclosure ya conflict of interest mlizonazo huko uraiani? Hii sio desturi ya wengi, na nadhani huyu kijana ameonyesha njia hapa. Tena asingefanya disclosure, bado mngemshutumu!
Sasa kwende kwenye hoja zake. Kijana Thuwein amechanganua kwa maoni yake suala la freedom of the press katika vipindi vya awamu zote nne. Akasema Kikwete, love him or hate him, he is very tolerant of free press compared to past presidents. Uhuru wa kujieleza uliopo leo sio ule wa wakati wa Mwalimu. Sidhani kwamba huyu Thuwein alimaanisha kwamba Kikwete hajafanya matendo ya hapa na pale ambayo yanakiuka freedom of the press. Ushahidi upo to the contrary. Kwahiyo, that is not the point. Nilivyomuelewa mimi ni kwamba amepima wastani wake. Hivi wangapi leo wanadhani kwa wastani Nyerere angevumilia kutukanwa kama anavyotukanwa Kikwete leo hii? Tena haimaanishi kwamba uhuru huu wa leo umeletwa na Kikwete, la hasha. Umeletwa na wananchi wenyewe kupigania haki yao kwa muda mrefu kuwa na uhuru zaidi wa habari na maoni. Lakini suala ni kwamba Kikwete amevumilia mangapi ya kweli na ya uwongo bila ya kuchukua hatua za kuzima habari? Uhuru tulionao leo hii ni jambo ambalo lilikuwa geni sana kwa wananchi wa Egypt chini ya Mubarak, kwa wananchi wa Tunisia chini ya Ben Ali. Huo ndio ukweli. Tena huna haja ya kwenda mbali. Tazama jirani yetu Malawi ambapo nchi nzima ina magazeti matatu binafsi na yote yanafungiwa kila kukicha. Ukiwa pale Blantyre, mji mkuu, magazeti yanaonekana mitaani lunch time, na kopi zake ni chache sana. Kuna TV moja tu ya Serikali (private TVs zimezuiliwa bila sababu maalum) na kutwa nzima TV inaonyesha hotuba za Rais ama sivyo wanaweka kwaya za injili. Siku nzima! Hakuna talk shows, hakuna kuongea siasa kwa namna yoyote. Ni jambo la kujiuliza je tungekuwa kama wao, au kama Zimbabwe, Egypt, au Tunisia ambapo freedom of speech ni finyu je hali yetu ingekuwaje? Tupime hili bila kuleta hoja za kando kando.
Kuhusu generational change in leadership, hili nashindwaga kuelewa kwanini watu fulani hawalipendi kabisa, tena basi vijana! You would think kwamba vijana wangeungana katika hili bila kujali vyama au itikadi. Sijui ni kwa vile wanajua vyema vipenzi vyao watu kama Dr Slaa, Samuel Sitta, Membe au Lowassa tayari ni wazee katika zama za dunia ya leo? Letu ni Taifa la vijana, sasa kwanini tusiseme vijana competent wasipewe nafasi? Off course, umri peke yake sio hoja. Lazima kiongozi awe na utashi, uwezo, maadili na mengineyo. Kwahiyo mtu yeyote anayesema kwamba kiongozi mkuu ajaye awe amezaliwa baada ya mwaka 1961, haina maana kwamba akose sifa zingine zote! Haina maana kwamba sifa pekee ni huo umri mchanga. Lakini utashangaa kuona watu wanajibu hoja hii kwa kutoa logic za namna hii ambazo hazina msingi na wala hazipeleki mbele majadiliano.
Mwisho, imesemwa kwamba huyu Thuwein ameneemeka kutokana na familia yake. Cha kushangaza ni kwamba katika miaka yote ambayo baba yake amekuwa Katibu Mkuu CCM na kaka yake amekuwa Msaidizi wa Rais Ikulu na sasa Mbunge, huyu kijana ameamua kuwa nje ya nchi akijiendeleza mwenyewe kimasomo. Wanaomfahamu Marekani wanajua jinsi gani alivyosota huko. Hakwenda shule zinazojulikana, amesoma maeneo ambayo kwa Marekani ni vijijini. Na inaonekana scholarships na kazi za kujishikiza ndizo zimemsaidia kumaliza elimu yake. Kama angekuwa ni mtu wa kutegemea familia, basi angeweza amerudi nyumbani siku nyingi na kujaribu kunufaika binafsi na hayo maisha ya juu kupitia familia yake. Lakini badala yake yupo Sudan ya Kusini akiishi maisha ya shida vijijini akisaidia watu wa kawaida kiafya. Naamini angeweza kufanya hiyo kazi vijijini hapa Tanzania (ambapo hali kitaifa ni bora kuliko kule Sudani Kusini), lakini pengine alitaka kuwapo sehemu ambayo hatajulikana kwamba ni mtoto wa kigogo ili apate uzoefu wa kitaaluma bila kunufaika bila haki.
Maelezo mengi haya nimeyapata kwenye LinkedIn profile yake www.linkedin.com/pub/thuwein-yusuf-makamba/30/194/918 na ukisoma Thesis yake pia ambayo ipo online unaona mawazo haya.