TANZANIA (taifa stars) vs CAMEROON !!!

wajimini nina swali,nikiangalia taifa stars kila mchezaji alikua na kitambaa cheusi mkono wa kulia,je tulikua twaomboleza au ndo mambo ya chenge hayo walikua wakitafuta siti uwanjani??!!?
maan anishasikiaga african teams hufanyaga mambo hayo

Mtaalam,

Wachezaji wa Taifa Stars walivaa kitambaa cheusi mkononi kuomboleza kifo cha mwanasoka mahiri Maulid Dilunga pia wali observe one minute silence b4 Ko
 
Mtaalam,

Wachezaji wa Taifa Stars walivaa kitambaa cheusi mkononi kuomboleza kifo cha mwanasoka mahiri Maulid Dilunga pia wali observe one minute silence b4 Ko

asante sana masatu maana siko bongo so habari za kusimama kwa dakika moja before game kwa ajili ya maulid dilunga sikuzijua vinginevyo nsingeask...maana nilishawahi sikia wachezaji wa kiafrica hufungwaga vi chenge chenge ili uwanjani kwenye process yao ya kutafuta siti za kupachika mabao na kucheza vizuri wangare!!
 
haya nimekutana na habari hizi tena kwenye magazeti yetuu kuwa safu yetu ya ushambuliaji itatisha kinyama mjini younde hadi kina song walie siku hiyooo

Washambuliaji Taifa Stars wadai kubuni mbinu mpya dhidi ya Cameroon

MSHAMBULIAJI wa Taifa Stars, Danny Mrwanda amesema wamebuni mbinu mpya ya kupambana na mabeki wa Cameroon ili kuhakikisha wanapata mabao kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi jijini Yaounde.

Stars iliikamata vilivyo Cameroon katika sehemu ya kiungo na ngome wakati timu hizo zilipotoka sare ya bila kufungana kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa Jumamosi iliyopita, lakini mashambulizi yake ya kushtukiza hayakuwa na madhara kwa wababe hao wa soka barani Afrika, zaidi ya kutoa nafasi moja ya wazi, ambayo Mrwanda alishindwa kuitumia baada ya kupiga kiki wakati akianguka.

Katika mechi hiyo ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, Mrwanda alichezeshwa kama mshambuliaji wa kwanza, akisaidiwa na Mrisho Ngassa, ambao vimo vyao ni vigogo kulinganisha na ukuta wa Cameroon wenye mabeki warefu, wakiongozwa na mkongwe Rigobert Song.

Hata hivyo, Mrwanda na Ngassa waliisumbua sana ngome hiyo lakini hawakuweza kuunganisha wavuni mipira ya juu kutokana na urefu wa mabeki hao wa Cameroon.

Akizungumza baada ya mazoezi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jana, Mrwanda alisema walitumia mbinu ya kuwakimbiza mabeki wa timu hiyo kwenye mchezo uliopita, lakini sasa watabadilisha mbinu hiyo na kutumia nyingine ambayo wana imani itakuwa na ufanisi.

''Tuliwakimbiza sana wale mabeki kwa kuwa tulijua hawawezi mpira wa kasi na kwa hilo tulifanikiwa kwa kiasi fulani kwa kuwa tulifanikiwa kuingia na mipira mingi ndani ya eneo la hatari, lakini tukashindwa kufunga,'' alisema mshambuliaji huyo anayesakata soka Kuwait.

?Lakini, nina imani watapata taabu sana mechi ijayo. Sasa tutabadilisha mbinu kidogo pamoja na kuwakimbiza tutaongeza vitu vingine ambavyo vitatufanya tupate mabao kwani nia yetu ni kuhakikisha tunafunga ili tujiweke pazuri na hilo hata kwa Cameroon linawezekana bora tuwe pamoja.?

Kocha wa Stars, Marcio Maximo, ambaye hakumchezesha mshambuliaji wake tegemeo Emmanuel Gabriel, bado anaonekana kutoridhishwa na safu yake ya ushambuliaji na jana alionekana kuendelea kufundisha mbinu za kupata mabao.

Kocha huyo Mbrazili amekuwa akifundisha washambuliaji wake na wachezaji wa kiungo kujaribu kiki za mbali na amekuwa akiwatumia sana Abdi Kassim, ambaye aliingia mwishoni mwa mechi na Cameroon, na Nizar Khalifan, ambaye alitoka kumpisha Kassim
 
na nikakuta habari hiziiii

Safari ya Cameroon: Mashabiki kulipia Sh800,000...malazi ujilipie

MASHABIKI wanaotaka kwenda kuishangilia Taifa Stars dhidi ya Cameroon, mjini Yaounde watalazimika kulipia dola 700 za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh800,000 za Tanzania), Shirikisho la Soka (TFF) lilisema jana.

Ofisa habari wa TFF, Florian Kaijage alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya nauli, ambayo alisema itagharimu dola 400, gharama za uwanja wa ndege, dola 190 na viza dola 110.

Kiwango hicho ni nafuu kuliko vile vilivyotangazwa wakati Stars ikienda Cape Verde, Burkina Faso na Senegal, ambavyo vilikuwa zaidi ya dola 1,100.

Alisema ndege hiyo ina uwezo wa kubeba watu 90. Mbali na wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la Stars, kutakuwa na nafasi 40 za ziada walizoachiwa mashabiki.
 
kwanza naona ni vituko vya maandalizi ya tff kwanini majamaa waondoke ijumaa??!why shudnt they go earlier wakajiandae na mechi??na kuzoea hali ya hewa?au wanataka wakifungwa ahuko waje hapa waanza toa visingizio vya uchovu na other pumbaz??

pili ni hili la ndege yetu hiyo....ndege ina uwezo wa watu 90 lakini kwa washabiki ni 40 tu...50 ni timu which shud b kwa watu 23,kocha,kocha msaidizi,dokta ambao jumla yao ni kama 30!!sasa hao 20 wa ziada ndio maafisa wa tff???ndio right procedure au wanatumia mgongo huo kwenda???!!!!!
 
jamani mechi ya leo huko younde vipi??tushapigwa ngapi???any link kufuatilia game???
 
Kipindi cha kwanza ndiyo kinakatika bila bila

Live Scoreboard 45' + CMR Cameroon 0:0 Tanzania TAN
22' NGA Nigeria 0:0 Equatorial Guinea EQG
 
Vijana wa Taifa Stars(siyo JK Boys) wanajitahidi, waweke juhudi zaidi kipindi cha pili kutocheza kwa kujihami na pia kupeleka mashambulizi ili ikiwezekana wajipatie bao.
 
Bubu...kama wamezoea kuitwa Hivyo let them do...kuna ubaya gani...? kwanini miaka ya nyuma hawakuitwa Ben Boys au Mwinyi Boys...(Mwinyi alikata tamaa kabisa na kusema kichwa cha mwendawazimu...)..JKN sijui....
 
Bubu...kama wamezoea kuitwa Hivyo let them do...kuna ubaya gani...? kwanini miaka ya nyuma hawakuitwa Ben Boys au Mwinyi Boys...(Mwinyi alikata tamaa kabisa na kusema kichwa cha mwendawazimu...)..JKN sijui....

Wamezoea toka lini? Nani kawazoesha? Hii timu ni Watanzania wote kama inafanya vizuri au la hivyo ni muhimu kuiita jina lake linalojulikana officially, siyo wakifanya vizuri wanakuwa JK Boys na wakifanya vibaya wanakuwa Taifa Stars. JK hatoi hela mfukoni mwake kuihudumia timu hii, pesa hizo ni za walipa kodi wote wa Tanzania hivyo hao ni wawakilishi wa Watanzania wote na siyo JK pekeee yake.
 
Namkubuka SteveD alivyosema kwamba wiki iliyopita kila akiona post mpya katika thread hii alikuwa anabanwa na haja ndogo....:), mimi kila nikifungua hiyo link ya FIFA naanza kuwa na wasi wasi
 
Half ya pili mambo bila bila ,ila tunazidi kuwachachafya wacamerouni ,nipo hapa natazama luninga,goli likiingia tu nitawapa habari,yaani wale wachawi wa bunge letu kwani hawakuisaidia timu kuingia na majuju Cameruni nabadala yake wameenda kuroga bungeni huku kama si kufilisika ni kitu gani ?
Wacha nijionee ,pita hapa badala ya dakika kama 20 pengine dua zangu zikawasaidia kurudi na ushindi ,usisahau halfu ni ya pili ngoma ni draw yaani sifuri kwa sifuri !
 
Nigeria ameshapata moja goli lilogungwa na Yakubu Ayegbini katika dakika ya 45 just goal & halftime. Kumbuka wanachezza na Equatorial Guinea kundi la nne.Mechi ya mwanzo alishinda Nigeria kwa goli hilo hilo moja.
 
dakika ya 61 bila bila
Live Scoreboard 61' CMR Cameroon 0:0 Tanzania TAN
Half-time NGA Nigeria 1:0 Equatorial Guinea EQG
 
Back
Top Bottom