Tanzania secures 1.8tri/- loans from China for construction Road 230 km and pipeline gas mtwara

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Rais Jakaya Kikwete Akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hui Liangya

Pg.2.JPG

Rais Jakaya Kikwete akipeana Mkono na Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu alipomtembelea ikulu, Dar es Salaam.
dande-2.jpg

Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha ikulu Jijini Dar es Salaam jana Naibu Waziri Mkuu wa China, Hui Liangyu
--
200px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatano, Septemba 5, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hui Liangya kuhusu masuala mbali mbali yanayohusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam mara tu baada ya Mheshimiwa Liangya kuwasili nchini kwa ziara ya siku tatu katika Tanzania kama sehemu ya ziara ya nchi za Afrika, viongozi wote wawili wameeleza kuridhishwa kwao na hali na ustawi wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais Kikwete ametumia nafasi ya ziara hiyo ya Mheshimiwa Liangya kuishukuru China kwa michango yake katika jitihada za maendeleo za Tanzania.


Amesema Rais Kikwete: "Jamhuri ya Watu wa China imetusaidia mengi katika jitihada zetu za maendeleo kuanzia kwenye ujenzi wa Reli ya TAZARA, ujenzi wa Uwanja wa Taifa, ujenzi wa Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar Es Salaam, ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, na ahadi ya kusaidia kuanzisha Benki ya Kilimo Tanzania. Kwa hakika Jamhuri ya Watu wa China imetusaidia mengi na tunaishukuru sana."


Rais Kikwete pia ameitaka China kuendelea kuisaidia Tanzania hasa katika maeneo ya jinsi ya kuongeza kasi ya uchumi. "Tunataka kwa kweli kujifunza kutoka mifano ya mafanikio ya marafiki zetu wa karibu kama China. Hivyo, bado tunaendelea kusisitiza ushirikiano wa China katika kuanzisha na kuendesha maeneo maalum ya uzalishaji –Special Economic Zones "


Naye Mheshimiwa Liangya amemwambia Rais Kikwete kuwa China itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Tanzania ambao umekuwa unashamiri tokea ulipoanzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Tse Dung.


Mheshimiwa Liangya amesema kuwa undani wa miradi yote ambayo China inasaidia katika Tanzania ungejadiliwa kwenye mkutano kati yake na Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda katika mazungumzo rasmi yaliyofanyika baada mchana wa jana


Kiongozi huyo wa China pia ameisifu Serikali ya Mheshimiwa Kikwete kwa uamuzi wake wa kuanzisha Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na kuongeza kuwa mpango huo umeandaliwa kwa umakini mkubwa. "Nawapongezeni kwa uamuzi wenu wa busara wa kuanzisha tena Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Ukitekelezwa vizuri unaweza kusukuma kwa kasi zaidi maendeleo ya nchi yetu."


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

5 Septemba, 2012

 

Kila baada ya Miezi Miwili Viongozi wa Kichina Wanazuru Tanzania... HII INATISHA TAIFA LETU...
 
Hapo mwisho kwenye statement ya kiongozi wa uchina,ni makosa ya kiuandishi ama ni kitu gani?je alimaanisha kusema maendeleo kwenye "nchi yenu"?
 
Hapo mwisho kwenye statement ya kiongozi wa uchina,ni makosa ya kiuandishi ama ni kitu gani?je alimaanisha kusema maendeleo kwenye "nchi yenu"?

Waliotoa taarifa ni ikulu, kama kawaida ni kosa la walioandaa taarifa/tamko.

Inawezekana pia kuwa "lost in translation".
 
Hivi karibuni tutaanza kuwa na watunza bustani na watumishi wa ndani wachina kwa jinsi mambo yanavyoelekea halafu kibaya zaidi hatuna mikakati zaidi ya kupiga siasa wageni wanakuja kuchuma shamba la bb wanahamishia kwao,uzi wa madawa naona mods wameufuta ila too late ushasambaa kila kona sahv watu washaanza kurushiana kwenye emails zao hadi mabarabarani ushaanza kugawiwa
 
huyu rais hajui hata majukumu yake nina imani hana kazi za kufanya ... Huyu si angetakiwa akutane na kina bilal ama pinda sasa jk naye kujichukulia majukumu yya mwenzake ndio nini?
 
Hapo mwisho kwenye statement ya kiongozi wa uchina,ni makosa ya kiuandishi ama ni kitu gani?je alimaanisha kusema maendeleo kwenye "nchi yenu"?

Umeona eenh!!

Nami imenishitua sana. Kama mtu anaweza kuwatamkia wazi namna hii halafu bado mnaendelea kumchekea. Aibuu!!

Ni kweli inajulikana kuwa China kama yalivyo mataifa ya Ulaya na America yapo kwa maslahi yao zaidi. Lakini anapowaambia wazi namna hii amekudharau sana wewe uliyemuhitaji.
 
huyu rais hajui hata majukumu yake nina imani hana kazi za kufanya ... Huyu si angetakiwa akutane na kina bilal ama pinda sasa jk naye kujichukulia majukumu yya mwenzake ndio nini?

Pamoja na uliyosema, kautafute ule uzi wa Ridhiwan Kikwete na kashfa ya Madawa ya Kulevya ambao nafikiri ulipewakichwa "JK auza ncha kumwokoa Ridhiwan asinyongwe"
 
Back
Top Bottom