Tanzania`s future in Manji`s hands?

Vita ya Manji na Mengi hiyo! Ila Mengi naye apungeze kasi, maana siku akinasa kwenye mtego kama wa Mchungaji Mtikila, itakuwa noma!!!
 
Hii issue ya Manji ukijumlisha na Viongozi wa Mashirika ya Fedha ambao wali husika na Wizi wa EPA, unaweza kuona ni watu gani wanao tuongoza, na tunakoelekea, kwenye primitive accumulation of wealth, ndio maana tunaona akina Mkapa wanaweka kiwango kidogo cha mishahara na sheria mbali mbali za kuwasaidia wawekezaji, kumbe wao wenyewe wamo humo.
 
Masaki,
The roundtable sponsored by Barrick, Zain, Arthumas Group,Artumas group and Coca-Cola)

Mkuu hapa sioni kabisa ugonvi wa Manji na Mengi zaidi ya sisi tufumbia macho ukweli ambao kesho tutakuja shikana mashati...Kumbuka tu kitu kimoja pamoja na tofauti zetu - once devided we both fail!
Huu ndio usanii mtupu unanikumbusha Lowassa alipokuja huku alikataa kukutana na Watanzania lakini akahudhuria dinner party iliyoandaliwa na wahindi ambayo kushiriki walitoza ada ya mlangoni dollar 50.....
Hii conference haina mpango hata kidogo hasa ukizingatia kwamba hizi kampuni zinazo sponsor ni vyombo ambavyo vinahitaji zaidi deregulation, less taxes na uwezo wa kumiliki ardhi...
Kifupi ni mkutano ambao unatakiwa kupigwa vita, ningependekeza zaidi kama mkutano huu ungejengwa zaidi na wachumi wetu wa ndani na nje kupitia, soko letu la DSE na jinsi ya kujenga soko hilo..

Mkuu Zitto,
Sidhani kama unajenga unapopongeza conference kama hii wakati hufahamu kabisa malengo yake zaidi ya kichwa cha habari kilichofunika moto!..Swali kubwa umelisema wewe mwenyewe!
Kwa nini hukualikwa ama vichwa vyetu vya uchumi wamewekwa nje?....
 
Mkandara,

Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja, leo nimeshangaa kukugundua kwamba Wa Canada hawawapendi kabisa Wa Marekani kwa kuwa waliwaingiza kwenye mkataba wa kitapeli miaka mingi iliyopita. Yaani Canada wana mafuta mengi lakini wa sasa hawafaidiki na kupanda kwa bei ya mafuta duniani kwa kuwa walisaini mkataba wa kuuza cruide oil kwa USA miaka mingi sana iliyopita. Canada kwa sasa wangeweza kufanya "refinery" na kuuza mafuta yao kwa bei ya juu zaidi lakini mkataba wao na USA inawabana kufanya kufanya hivyo.

Sasa hebu fikiria nchi kama Canada inaweza kuingizwa mkenge na wajanja wa CIA, sembuse Tanzania na viongozi wetu hohe hahe!!!!!
 
Masaki,
Mbali na hayo ya mafuta, Canada hawaruhusiwi kutengeneza magari madogo hata kama teknologia hiyo wanayo isipokuwa mashirika ya US tu ndiyo yanaweza kuweka viwanda vyake Canada!...
 
Masaki,
Mbali na hayo ya mafuta, Canada hawaruhusiwi kutengeneza magari madogo hata kama teknologia hiyo wanayo isipokuwa mashirika ya US tu ndiyo yanaweza kuweka viwanda vyake Canada!...

Duh! Kweli CIA ni noma! Naomba mwenye applications forms za kujiunga na CIA anirushie hapa mtandaoni! Maana nimechoka kupiga kelele za kuitaka Tanzania na Watanzania kubadilika!!!!
 
mimi niliwadokeza wanajamii kuhusu mkutano huu
mwezi juni na link nikawawekea lakini naona
tulibanwa navipau mbele vingine wakati huo
hebu ona

https://www.jamiiforums.com/habari-hoja-mchanganyiko/14328-mkutano-mwengine-huo.html

Mwezi June kulikuwa na Bunge la bajeti, ndio maana hukupata sapoti ya kutosha. Pole sana. Ila wana JF naomba ridhaa yenu niwe fisasi...Maana naona mafisadi Tanzania ni kama fasheni vile, yaani ndio ujanja! Unaiba, unatangazwa kwamba umeiba, unajadiliwa Bungeni, kisha hufanywi lolote~!!!! Sana sana hukumu yako ni kupewa muda wa kurudisha vijisenti ulivyoiba!

Nani hataki biashara nzuri na yenye tija kama hiyo?
 
Nilipata mtu mmoja aliyeniambia kuwa Manji ni product kali ya Havard University yeye pamoja na Rostam Aziz. Hawa wamefundishwa entrepreneurship ya hali ya juu. Kwa hiyo kwa macho yao wanaona jinsi watanzania kwa upamoja wao walivyolala. Kwa elimu waliyopata wanaona fursa nyingi mno hapa Tanzania.

Lakini kwangu mimi ninasikitika tu kuwa hawa watu hawana hata chembe moja ya nia ya kutumia ujuzi na elimu yao kwa ajili ya nchi wanayoiita yao. ELIMU ni nini kama huitumii kwa ajili ya jamii yako??

Shame on them!!!!!!!!!!!!!!

Kwamba Manji anaoneka atashepu uchumi wa nchi na kwamba yeye ni role model mimi napinga kabisa na siko tayari kubadilishwa imani yangu.


Kamende,

Katika nadharia ya uchumi wa kibepari, unatakiwa kutumia kila nafasi uliyonayo kujipatia faida. Kama Watanzania wamelala, na una nafasi ya kutengeneza faida kubwa kutokana na kulala kwao, tena faida hiyo itokane na njia halali, basi ni haki yako kutengeneza faida hiyo.

But, I beg your pardon, did Manji go to Havard University?
 
Fisadi Manji ajiengua

Date::9/24/2008
Mfanyabiashara maarufu ajitoa kuwakilishi Tanzania mkutanoni Ulaya
Na Mwandishi Wetu
Mwananchi

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Yusuf Manji, amejitoa katika nafasi ya kuwa mmoja wa wawakilisha wa Tanzania katika mkutano wa wafanyabiashara wenye mchango kiuchumi katika nchi zao kutoka Afrika na wengine wa nchi za Ulaya.

Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya nafasi hiyo ya Manji kuibua mjadala, huku baadhi ya watu wakihoji sababu za mfanyabiashara huyo kupewa nafasi hiyo kubwa ya kuwa mmoja wa wawakilisha wa nchi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Manji alisema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona amekuwa akichafuliwa jina lake na baadhi ya watu na vyombo vya habari nchini.

Manji ambaye alitajwa na kusifiwa na gazeti la The Economist kama mfanyabiashara maarufu ambaye ana mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania, alisambaza nakala ya barua ya uamuzi huo kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete na waandaji, mjini Vienna, Austria.

Alisema uamuzi huo unatokana na taarifa za kumchafua ambazo zimekuwa zikiandikwa na magazeti matatu ya kila siku.

"Baada ya kupitia matukio ya hivi karibuni kwa kina, kwa heshima na taadhima nimeamua kutoa jina langu katika orodha. Uamuzi huo nimeufikia mwenyewe baada ya kuona nashutumiwa sana."

Manji alisisitiza kuwa kuingizwa kwake katika orodha hiyo kulitokana na uzoefu na mchango wake wa kuimarisha sekta binafsi kwa kuunganisha sekta ndogo na kubwa.
 
Kamende,

Katika nadharia ya uchumi wa kibepari, unatakiwa kutumia kila nafasi uliyonayo kujipatia faida. Kama Watanzania wamelala, na una nafasi ya kutengeneza faida kubwa kutokana na kulala kwao, tena faida hiyo itokane na njia halali, basi ni haki yako kutengeneza faida hiyo.

But, I beg your pardon, did Manji go to Havard University?


Kuna ukweli kwenye hili?
 
heshima mbele wakuu, hapa sasa naona kweli sauti ya watu nguvu ya ajabu.... Aluta continua....
 
heshima mbele wakuu, hapa sasa naona kweli sauti ya watu nguvu ya ajabu.... Aluta continua....

Hapo ndio wajue fedha zao haziwezi kununua watu wote, siku zote na kwa kila kitu na wajue pia Watanzania wa leo si wale wa mwaka 47 na kwamba hawatakubali kuendelea kuzugwa kila siku. Iko siku mambo yataharibika
 
nilipata mtu mmoja aliyeniambia kuwa manji ni product kali ya havard university yeye pamoja na rostam aziz. Hawa wamefundishwa entrepreneurship ya hali ya juu. Kwa hiyo kwa macho yao wanaona jinsi watanzania kwa upamoja wao walivyolala. Kwa elimu waliyopata wanaona fursa nyingi mno hapa tanzania.

Lakini kwangu mimi ninasikitika tu kuwa hawa watu hawana hata chembe moja ya nia ya kutumia ujuzi na elimu yao kwa ajili ya nchi wanayoiita yao. Elimu ni nini kama huitumii kwa ajili ya jamii yako??

shame on them!!!!!!!!!!!!!!

kwamba manji anaoneka atashepu uchumi wa nchi na kwamba yeye ni role model mimi napinga kabisa na siko tayari kubadilishwa imani yangu.


shame shem shame shame ............ Look at them!!!!!!!!
 
Siku zote huwa nawshangaa nyie watu wa JF hayo matendo ya Manji na RA ni matokeo. TAFUTENI CHANZO.

Kwani huyo handsome wenu wakati anachukuwa mamiliono ya kampeni hakujua kuwa fedha zetu wananchi ndio zinatumika? Ubavu wa manji RA na wahindi wote wezi kuchota hela zetu wangeupata wapi kama sio MIATANZANIA MIENZETU inayotusaliti?

Mijitu iafurahia kupata billion moja kwenye deal ya mhindi anayechota mabilion?

Mwl Nyerere aliwahi kutofautisha rushwa za ughaibuni na za kiafrica, ulaya mtu anapendelewa mtoto wa waizri anapewa kazi anaifanya kwa kiwango cha kurifdhisa africa anapewa tenda mdogo wa hawara yake waziri kazi anavurunda TUTAFIKA KWELI.

Tusipoacha tamaa hawa tunawalaumu kuwa WAHINDI WABAYA wataendelea kututafuna mpaka BETWEEN OUR LEGS

uwe unapanga maandishi vizuri ili yasomeke,mbuzi wee
 
Because Your/Our President is in Manji's payroll therefore: Tanzania`s future in Manji`s hands. The current Presidency of URT is under the influence of the pimps; and these pimps dictate terms: Money Terms!
 
Nilipata mtu mmoja aliyeniambia kuwa Manji ni product kali ya Havard University yeye pamoja na Rostam Aziz. Hawa wamefundishwa entrepreneurship ya hali ya juu. Kwa hiyo kwa macho yao wanaona jinsi watanzania kwa upamoja wao walivyolala. Kwa elimu waliyopata wanaona fursa nyingi mno hapa Tanzania.

Lakini kwangu mimi ninasikitika tu kuwa hawa watu hawana hata chembe moja ya nia ya kutumia ujuzi na elimu yao kwa ajili ya nchi wanayoiita yao. ELIMU ni nini kama huitumii kwa ajili ya jamii yako??

Shame on them!!!!!!!!!!!!!!

Kwamba Manji anaoneka atashepu uchumi wa nchi na kwamba yeye ni role model mimi napinga kabisa na siko tayari kubadilishwa imani yangu.

Kamende,
usiwe mjinga kusadikishwa upumbavu!!! simple minds can easily be fooled!!
Lini rostam alisoma Havard!! hizo sifa anazo?? usishushe hadhi ya chuo kwa ujinga na kutokuwa mpevu wa mambo wewe!
 
Back
Top Bottom