Hivi kuna tofauti yoyote kati ya Zimbabwe na kinachoendelea Zanzibar tangu mwaka 1995?
Hii safi kabisa kwani ndio tunataka tuelekee kwenye siasa ambazo hakuna kuzulumu na muelekeo anaoupeleka Mheshimiwa sio mbaya kwani naona ameanza kufahamu kuwa ubabe wa kutumia maguvu kwenye uchaguzi sio jambo la busara ,hivyo akumbuke yale mambo ya kupeleka vifaru na marocket loncha kule Unguja na kwenda kuwahanisisha watu na familia zao kule Pemba si mambo ambayo yanawanyima uhuru wa kuchagua serikali yao wazanzibari bali ni siasa za ukandamizaji na unyanyasaji ,zikichangiwa na tabia za kinyama maana ubinadamu huondoka na kuingia tabia za unyama na hilo Muungwana analifahamu kwani katika Uislamu tabia ya binadamu ina kiwango na hutokea ikawa mnyama ni bora kuliko binadamu.
Kwa mujibu wa ile taarifa ya thread, jeshi letu ni kubwa zaidi ya mara mbili ya lile la Zimbabwe. Sasa, I hope Rashid Othman kampa Kikwete better Intelligence Estimates, than simply relative military sizes. Wanaweza kuwa wana nondo kali zaidi yetu ( juzi Mchina Mwekundu kashusha shehena za ammo kwa Mugabe hapo).
Tusije tukaenda kichwa kichwa tukatembezewa mkong'oto. Wenye "dataz" za Nuclear Stockpiles za Mugabe mpo?
Kitu ambacho nadhani wengi tumekisahau au kushindwa kuconnect dots ni kile kile kilichotokea kwa upande wa Kenya. Kweli JK anatumiwa kupitisha ujumbe kwa Mugabe. Hilo ndilo jambo ambalo binafsi linanikera sana na niliandika kwenye barua kwa JK. Hatuwezi kusubiri wazungu watuambie kuwa Zimbabwe hali ni mbaya.
Kuhusu matumizi ya nguvu inasikitisha kuona kuwa JK ananukuliwa kusema haya siku moja baada ya wabunge wa Uingereza kutoa mawazo ya kutumia jeshi kuingilia Zimbabwe. Na sitoshangaa US nao wakasema wako tayari kutoa financial and logistical support kwa ajili ya jeshi hilo. Tofauti na AU Marekani na Uingereza wanazo fedha za kufanikisha hilo kama wakitaka.
Ni kwa sababu hiyo siamini kuwa JWTZ inaweza kushiriki moja kwa moja kwenye uvamizi ikibidi, ila sitoshangaa tukatakiwa kutoa viwanja na staging area ya Operation ya kijeshi. Hivyo manowari na meli za kivita za Uingereza na hata Ufaransa zinaweza kusogea katika pwani yetu na kuwa staging area. Tunaweza tusitakiwe kutoa hata askari mmoja lakini tukatakiwa kutoa ruhusa ya kutumia anga letu kwa ndege zao za kivita. Hayo yote yanawezekana and me being a military analyst pia naweza kusema kwamba uwezekano wa kutumia jeshi letu moja kwa moja ni mdogo lakini tunaweza kutumika kama ilivyotumika Saudi Arabia au Qatar au Kazikstan katika vita vya Iraq.
Ni kwa sababu hiyo naamini the best approach for Kikwete is not the "war talk" bali kusimama na kuitisha mkutano wa ufumbuzi wa suala la Zimbabwe mojawapo ni kuhakikisha kuwa Mugabe anaanchia ngazi na analindwa asishtakiwe na wakati huo huo kuandaa uchaguzi mpya na huru. Hata hiyo mazungumzo haya ya vita yana lengo moja tu, nalo ni kuweka pressure kwa Mugabe.
Itakuwa ni aibu sana kwa Afrika endapo Mugabe ataondolewa madarakani kwa nguvu.
Wakuu,
Naona tunasahau jambo moja kubwa hapa kuhusu Zimbabwe.
Matatizo yanayoikabili Zimbabwe ni global na wale political elite wote Kikwete sasa akiwa mmojawapo wanajaribu kutaka kuidhibiti Zimbabwe kwenye suala la global financial interests.
Huko nyuma kulikuwa na nchi kama za Angola, Msumbiji, DRC na Sudan ambayo bado ina matatizo kule Darfur. Lakini hii kitu global financial markets inakuwa siku zote subsidised na rasilimali kutoka Afrika na Zimbabwe ilikuwa na mazao ya biashara na madini ambavyo kwa sasa havina soko.
Inajulikana sasa kwamba hizi financial interests zinakabiliwa na credit crunch, high inflation na pia the rise of commodity prices hasa mafuta na chakula.
Pia Mugabe pamoja na kusema kwamba Tsvangirai ni puppet wa mabepari lakini ni ukweli usiofichika kwamba ni lazima mabepari hawa watafanikiwa katika azma yao.
Kwa hio mimi naona kwamba kama kweli Kikwete ametoa wazo hili ni katika kujaribu kuona kwamba litakuwa digested vipi na hadhira kabla ya kufanya hivyo na baadae kusaidiwa na mabepari wenzie chini ya mwavuli wa UN resolutions zisizo na kichwa wala mkia.
By the way Mugabe alipewa nchi pale Lancaster House, lakini kwa kutaka sifa kupitia mgongo wa wakoloni wa zamani sasa anachemsha na wao hawako tayari kumuona anafanya hivyo.
Hivi kuna tofauti yoyote kati ya Zimbabwe na kinachoendelea Zanzibar tangu mwaka 1995?