Kwa kweli inasikitisha sana nchi kukosa mwelekeo na mipango madhubuti, inaudhi sana kwakweliWajerumani walikuja ku bid na ramani ya 1905.Kama serikali ingeshirikiana na ya ujerumani, US,Canada au UK tusingefika hapa mahali pa kusaini contract halafu tunalipa deni la kusaini contract c'mon!
Tulihoji RITES wanasifa gani, tukababaishwa baibashwa na serikali kwa vile 10% walishakula.
Futa bid ni uchafu, tuombe wenye akili watusaidie.period.
Pitia bajeti ya miundombinu kama utaweza kuamini kuna uwekezaji wowote kwenye miundo mbinu kama reli. Iliyojaa ni siasa na haditihi tu hakuna chochote cha leo au miaka 10 ijayo. InasikitishaKwa kweli inasikitisha sana nchi kukosa mwelekeo na mipango madhubuti, inaudhi sana kwakweli
And who signed the deal?
Andrew chenge.....
Bila kubinafsiha na kuwa na kampuni za reli "independent" hata wawekeze trillioni kumi, zitakufa tu. Hakuna kitu kiitwacho mali ya umma kikaendelea Tanzania hii.
mwanzoni nilikuwa naamini kuwa mambo tunayowaambia CCM na serikali ni mambo mageni kiasi kwamba wanaweza kuyafanyia kazi. Baadaye nikaja kuguundua kuwa yote tunayoyasema yameshasemwa sana na kujadiliwa. Tatizo ni kuwa yakitekelezwa yataondoa mianya ya ulaji. Ndio maana UDA imeuzwa, ATCL, na upuuzi mwingine wote tunaoujua.
Fikiria kwa mfano, hakuna mahali pazuri pa kuanzia treni za kasi kama Moro - DAR na Dar - Tanga. Maeneo hayo kwa treni iendayo kasi yanafikika chini ya dakika 45. Moro iko karibu 120Miles, wakati Tanga iko 223Miles kutoka Dar. Sasa tatizo kubwa la kwetu litakuwa bado ni umeme! Iwe kwenye Maglev trains au conventional trains. Lakini kabla ya kwenda huko tungeimprove hizi hizi conventional kama tulivyokuwa tunafanya (nadhani bado) kwenye TAZARA ambako tulikuwa na ile express na ordinary trains. Watu wangeweza kujenga na kuishi Tanga au Moro wanakuja asubuhi kufanya shughuli zao na kugeuza jioni na wengine wangeweza kufungua biashara huko kwingine na kuishi Dar.. miji yote miwili ingeweza kabisa kuabsorb the growing population ya Dar na hata Zanzibar.
Tukumbuke kwamba kwetu tatizo si fedha, siyo teknolojia wala siyo uwezo au haja. Vyote hivyo vipo. Tatizo ni uongozi. Ninaangalia hapa jitihada za Nyerere kuunganisha sehemu nyingine za Tanzania na Reli ya Kati - nimeshangaa juhudi zake hizo. Najiuliza TAZARA ilijengwaje wakati ule? Sasaa hivi TAZARA ingeweza pia kuwa na express hasa tukidandia utaalamu wa Wachina ambao waliijenga.. ingefungua pia barabara ya kwenda kusini zaidi..kama watu wanaweza kufika Mbeya mapema kuliko kwa njia ya basi well.. kwanini wapanda mabasi? barabara zingedumu zaidi n.k its all about leadership my dear friends.
Pitia bajeti ya miundombinu kama utaweza kuamini kuna uwekezaji wowote kwenye miundo mbinu kama reli. Iliyojaa ni siasa na haditihi tu hakuna chochote cha leo au miaka 10 ijayo. Inasikitisha
Aliimarisha reli aliyoacha Mjerumani, halafu akajenga nyingine. Awamu zote zilizofuata kwa pamoja hawajaweza kufanya uwekezaji aliofanya Nyerere.Jitihada gani za Nyerere, yeye ndiye alyeuwa kila kitu Tanzania, usituchafuwe saa hizi.
Kwa mara ya kwanza tunaona treni ikipakia abiria mjini, kwa mara ya kwanza tunasikia treni ikiboreshwa. Nyerere alikuta treni toka Mjerumani, aliifanya nini badala ya kuiuwa na kuwa nyang'anyag'a.
Aliimarisha reli aliyoacha Mjerumani, halafu akajenga nyingine. Awamu zote zilizofuata kwa pamoja hawajaweza kufanya uwekezaji aliofanya Nyerere.
Zomba angalia kumbu kumbu au kama huna basi omba tukupe.
nyerere hakujenga reli, aliyejenga mchina kwa kutaka shaba za zambia, ustake kuchekesha watu.
Angeiimarisha hiyo reli ya kati si ungeiona inafanya kazi. Tuulize sisi tuliyoipanda wakati tunachukuwa uhuru hiyo treni ilikuwaje na miaka 10 baadae ilikuwaje, kwa ufupi; nyang'anyang'a.
pumba...vuuuu!
Na kama ni kweli watu 10 wanakufa kila siku kwa ajali za barabarani, then usafiri wa treni unaweza pia kupunguza hii idadi.
Reli ya Tanga-Dar alijenga nani?Nyerere hakujenga reli, aliyejenga mchina kwa kutaka shaba za Zambia, ustake kuchekesha watu.
Angeiimarisha hiyo reli ya kati si ungeiona inafanya kazi. Tuulize sisi tuliyoipanda wakati tunachukuwa uhuru hiyo treni ilikuwaje na miaka 10 baadae ilikuwaje, kwa ufupi; Nyang'anyang'a.
Reli ya Tanga-Dar alijenga nani?
Nionyeshe reli iliyojengwa na Mwinyi, Mkapa na JK inayolingana na hiyo.
Ninasema kuwa mpaka Nyerere anaondoka madarakani reli zote zilikuwa zinafanya kazi.
Niambie reli ya kaskazini inapita behewa gani? Umetembelea ukaona reli ilivyo kichakani?
Narudia tena maana naona ulipanda treni za Congo, Nyerere akiondoka Madarakani reli ilikuwa inafanya kazi.
Unakumbuka ajali ya Kilosa ikitokea Nyerere hakuwa madarakani.
Narudia tena na tena maana uelewa wako unatia shaka sana, Nyerere akiondoka reli zote zinafanya kazi.OK?
Sasa endelea kubisha kadri uwezavyo, sina uwezo wa kukuzuia kuvua nguo hadharani. Ninachoweza kukuambia ni kuwa unavua nguo.
Zomba kuna maradhi mengi dunia lakini ya chuki ni hatari maana yanaathiri mfumo mzima wa fahamu.
Nionyeshe reli iliyojengwa na Mwinyi/Mkapa/ Kikwete kwa pamoja.
Kama huna jibu kaa kimya au endelea kuvua nguo mbele ya kadamnasi sina jinsi ya kukusadia tena
Jibu swali muungwana! Ile reli ya Tanga-Dar nani aliijenga? Nionyeshe kipande cha reli kama ya Tanga-Dar kilichojengwa na Mwinyi/Mkapa/Kikwete.Mkiambiwa mmejazwa Ubaguzi wa Ujinga mnakataa, kufanya kazi unakujuwa wewe au unasema tu? Ulisikia kabla ya ujio wake treni imezimika njiani inangoja diesel?