Tanzania Presidents: Nyerere, Mwinyi, Mkapa and Kikwete

Wakuu heshima zenu,
Hapa JF pamekuwa mahali penye uchambuzi yakinifu wa masuala yote.

LEO naleta hoja hii wakuu:-

Tuwachambue na kuwatathmini Marais wa awamu zote nne za uongozi hapa Tanzania.


Uchambuzi na tathmini hiyo ifanywe kulingana na mtu apendavyo au aonavyo, kijumla au jambo specific ila kwa heshima na nidhamu kubwa kwa wakuu wetu.

NYERERE,
MWINYI,
MKAPA,
KIKWETE.

Hao ndio reflection ya Watanzania. Roughly 25% ya Watanzania wana tabia za Kinyerere kujiamini kuwa wana uwezo wa kila jambo na kama wakiharibu basi ni kwa sababu ya watu wengine. Robo moja ina tabia za Kimwinyi za kutaka mambo yanyooke bila wao kufanya lolote, na ile sehemu 0.25 wana tabia za Kimkapa za kutaka kila kizuri wakimiliki kwa njia yoyote hata kama itabidi waue mtu ili kukipata. Sasa waliobaki ni wabababishaji tu wakiwa na tabia za Kikikwete za kutembelea majirani wakati wanapojua kuwa huko msosi uko mezani.
 
[COLOR=red said:
Kichuguu[/COLOR];695814]Hao ndio reflection ya Watanzania. Roughly 25% ya Watanzania wana tabia za Kinyerere kujiamini kuwa wana uwezo wa kila jambo na kama wakiharibu basi ni kwa sababu ya watu wengine. Robo moja ina tabia za Kimwinyi za kutaka mambo yanyooke bila wao kufanya lolote, na ile sehemu 0.25 wana tabia za Kimkapa za kutaka kila kizuri wakimiliki kwa njia yoyote hata kama itabidi waue mtu ili kukipata. Sasa waliobaki ni wabababishaji tu wakiwa na tabia za Kikikwete za kutembelea majirani wakati wanapojua kuwa huko msosi uko mezani.

KIChuguu,
Mmoja wa marais hao alisema kuwa Nyerere alikuwa kama MLIMA na yeye ni kama KICHUGUU.
 
KIChuguu,
Mmoja wa marais hao alisema kuwa Nyerere alikuwa kama MLIMA na yeye ni kama KICHUGUU.

Huyu aliona sawa lakini hakujitahidi ili na yeye aweze kuwa kama mlima.Kwa kweli ni rahisi kuwanyooshea vidole hawa Marais waliopita lakini ukweli ni kwamba kuna genge la majambazi walioko CCM ambao wamejipanga na kuhakikisha kuwa Keki hii ya watanzania wanaifaidi wao na watoto zao.

Watanzania tusipofumbua macho na kupambana na huu ukoloni mpya wa kutawaliwa na kunyonywa na watanzania wenzetu hakika vizazi vijavyo vitalaani ni kwa nini kizazi chetu kilikuwepo hapa Tanzania.
 
ningependa niwachambue kwa dira walizojiwekea(nyerere)/kuwekewa(mwinyi,mkapa na kikwete) wenyewe,

1. nyerere - azimio la arusha, kilimo cha kufa na kupona
mwalimu alitimiza maazimio yote ya azimio la arusha kwa kuweka binadamu wote ni sawa (sasa ivi hatuoni tatizo la hili we take it for granted), heshima ya mtanzania kimataifa (kina salim walitengenezwa we also take it for granted), kupigania uhuru ktk bara la africa (afrika kusini,zimbabwe,angola,msumbiji etc), kuondoa matabaka ya matajiri na masikini, elimu bure msingi hadi chuo kikuu bila ubaguzi( free education we used to take it for granted sasa tunaona its not free afterall and how expensive it is), ajira kwa watu wote hata kama ujasoma utajulia kazi kazini, kujitegemea, uanzishwaji wa viwanda na mashirika makubwa na madogo ( mashirika yote yalianzishwa kipindi cha mwalimu ambayo tunayauza). kilimo cha kufa na kupona tulijitosheleza kwa chakula mpaka tukasaza,tuliondoa ujinga kupitia upe,tulivunja ukabila na udini ndio maana ii amani tunayodai watanzania tunayo imetengenezwa kwa mfumo si kweli kwamba watanzania ni wapole kuliko watu wote duniani ni mfumo ndio ulitengeneza amani but we take it for granted.

2. mwinyi - azimio la zanzibar na structural adjacement programme
uchumi holela, kushuka kwa thamani ya shilingi, tabaka la matajiri na maskini kujitokeza, cost sharing, elimu, afya etc that we used to take for granted during nyerere, viwanda na mashirika kufilisika na kuanza kuuzwa, massive job cut, njaa mashamba pembejeo bei juu, uchumi wa udalali(economy with no production and manufacturing just collecting tax this kind of economy has never develop any country in the world), heshima ya mtanzania kushuka kimataifa, nchi kuongozwa na wafanyabiashara bila dira.

3. mkapa -millenium development goals,mkukuta,mkurabita
utumikaji wa rasilimali usiojali(plundering) wala tija, kuuzwa kwa mashirika hata yenye faida kwa bei ya kutupa, uchumi imara lakini hakuna uwiano kulinganisha na tulichopoteza kupata uo uchumi imara, kupotea kwa utanzania, rushwa na ufisadi wa kuumiza nchi ambao haujawai onekana nchini, alijitaidi kudhibiti mfumuko wa bei na kuifanya shilingi kua stable, matumizi mabaya ya ofisi, ubabe na nguvu kudeal na upinzani dhidi ya serikali yake, kurudisha ukoloni mkongwe, kuanza kuvunjika kwa amani that we used to take it for granted, improvement ktk miundominu ingawa kuna maswali ya kujiuliza kwa nini wahisani watulazimishe kujenga barabara badala ya kujenga viwanda

4. kikwete - vision 2025, kilimo kwanza
msanii, hana maamuzi binafsi ni wa kufuatilia upepo unasemaje, kushuka kwa thamani ya shilingi, mfumuko wa bei, hataki kutake risk, anasahau yeye ni rais wa nchi maskini kwa kujichanganya katika majukwaa ya marais tajiri kana kwamba tanzania iko level moja na izo nchi kwa mfanpo safari za marekani na ulaya zisizoisha,kuudhuria mkutano wa kujadili mabadiliko ya hali hewa kana kwamba na sisi tanzania tuna viwanda vya kutoa iyo co2 kwa kiwango cha kuitaji kujadiliwa, hana priority zinazorelate na hali halisi ya tanzania, hana hata mradi mmoja wa maendeleo mkubwa ulionza chini yake na ukaleta ajira au kipato kwa serikali, mdudu mbaya wa udini anakua kwa kasi chini ya utawala wake, hamana hata kimoja ktk vision 2025 alichokianzisha, kilimo kwanza ndio balaa analolite sasa! kiko wapi kilimo cha kufa na kupona? tulitegemea madawa na matrekta kutoka nje? sasa tusikilizie kilio baada ya kilimo kwanza kuanza, improvement ya miundominu iko katika kasi ya konokono, amefanya vizuri ktk kupanua sekta ya mawasiliano
 
I beg to differ,
Mkapa na baraza lake la mawaziri walitaka perfomance kwenye taasisi za kibenki wakataka ushauri kutoka wataalamu WB wakamsahuri hicho alichofanya. note nimesema ana weakness ya kuabudu wazungu akaingizwa mkenge

Mkapa akipelekwa segerea tutaandamana kwasababu makosa mengine ni kibinadamu na tunastahili kwenda mbele siyo kuangalia nyuma...jamaa kwa hulka yake ni mjeuri lakini siyo sababu tosha kumpeleka huko
Tumain,
Kitakachompeleka MKAPA Segerea si makosa ya kibinadamu, ni yale ya JINAI na kwa bahati mbaya tuhuma za makosa hayo zaelekea kuwa nyingi, kiasi yeye mwenyewe anaamua kumwachia Mungu, anashindwa hata kujieleza ni vipi anazuliwa wakati fursa ya kujisafisha anayo.
 
I beg to differ,
Mkapa na baraza lake la mawaziri walitaka perfomance kwenye taasisi za kibenki wakataka ushauri kutoka wataalamu WB wakamsahuri hicho alichofanya. note nimesema ana weakness ya kuabudu wazungu akaingizwa mkenge

Mkapa akipelekwa segerea tutaandamana kwasababu makosa mengine ni kibinadamu na tunastahili kwenda mbele siyo kuangalia nyuma...jamaa kwa hulka yake ni mjeuri lakini siyo sababu tosha kumpeleka huko

Tumaini tafadhali kama huna point za kuandika ni bora ukae kimya kuliko kutuletea utumbo hapa.
 
Nyerere:

Mazuri - Kujenga umoja wa kitaifa, kuweka uchumi mikononi mwa watanzania (azimio la arusha), Kujenga viwanda, Kusimamia mashirika ya umma, elimu bure, tiba bure, rushwa kudhibitiwa, wizi kidogo, kazi ndo msingi wa maendeleo; binafsi alikuwa commited na muda ulithibitisha kuwa alikuwa mwadilifu. Katika kipindi cha 1970 hadi 1978 uchumi ulikuwa imara na uzalishaji wa chakula ulikuwa juu. Mashirika ya umma yalikuwa yanaendeshwa vizuri.

Mabaya - Serikali kuhodhi njia zote za uchumi na kuwazuia watanzania kufanya biashara, kuondoa uhuru wa kujieleza, kujiingiza mno kwenye siasa za kimataifa zilizosababisha matatizo mengi ikiwemo vita (ilitokana na msimamo wa nyerere uliokuwa pro-east zaidi badala ya neutral kama alivyotaka dunia imuone).

Mwinyi:

Mazuri: Alianza na fagio la chuma (kama mnakumbuka vizuri miaka yake mitano ya kwanza). Alitoa ruksa kwa watanzania kufanya biashara, bidhaa zikajaa madukani. Alitoa uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari vikaota kama uyoga. Nchi ilianza kuwa vibrant na watanzania kuanza kujisikia kama watu. kuleta cost sharing.

Mabaya: Alishindwa kusimamia mfumo wa uchumi huria ikawa hakuna udhibiti, serikali ikawa kichaka cha wakwepa kodi na ushuru, tija serikalini ikawa hakuna. Kwa mara ya kwanza misamiati ya kushuka thamani ya shillingi na inflation ikaanza kujulika. Ufisadi serikalini ulianza kujiimarisha kipindi hiki. kushindwa kusimamia vizuri huduma za jamii pamoja na kuwepo cost sharing.

Mkapa:

Mazuri: Alianza na tume ya Warioba, kusimamia vizuri uchumi wa kibepari, kukusanya kodi, kudhibiti mfumko wa bei, kujenga miundo mbinu hasa bara bara, kurejesha nidhamu serikalini, kuendeleza mazuri ya utawala wa awamu ya pili.

Mabaya: Alishindwa kufagia ufisadi ulioanza kuota wakati wa awamu ya pili ukazidi kujikita mizizi zaidi. Ugenishaji wa uchumi. Kugawa raslimali za nchi kwa makampuni ya kigeni. Mikataba na makampuni ya kigeni mengi ikiwa mibovu kutokana na usimamizi mbovu au usiokuwepo kabisa. Tija iliyokuwa imeanza kuonekana serikalini ilisambaratishwa na ufisadi uliojiimarisha zaidi kipindi hiki hasa baada ya kifo cha Nyerere.

Kikwete:

Mazuri: Kujenga chuo kikuu cha Dodoma, kuendeleza miradi ya ujenzi wa barabara iliyoanza wakati wa mkapa (ingawa kwa kasi ndogo zaidi), kujenga matumaini zaidi kwa watanzania kuwa hali itakuwa nzuri.

Mabaya: Mdudu wa ufisadi anazidi kuitafuna nchi. Kutegemea zaidi misaada kutoka nje (explanation ya safari nyingi za nje zisizokoma). Wasi wasi kuwa nchi inaongozwa kwa ubia.

Verdict: Nyerere was far better than any of the rest.
Kikwete anaelekea kuwa rais mbaya kuliko wote.

Mwinyi was better than Mkapa. Ingawa wote walifanya vizuri miaka mitano ya kwanza wakachemsha miaka mitano ya mwisho; Makosa ya mkapa yalikuwa makosa yenye mwelekeo wa kijinai zaidi, kuliko yale ya Mwinyi ambayo mengi yalisababishwa na uwezo mdogo.
 
....Kuhusu baba wa Taifa Nyerere mimi sijui sana, maana kipindi chake wakati anatawala mie sikuwepo.

.......Kipindi cha Mhe; Mwinyi hapa nilikuwepo na kushuhudia utawala wake, hapa mambo yalikuwa poa, watu watu walikuwa huru kufanya kila kitu, huyu aliitwa mzee wa Ruksa.
Kama hukuwepo kipindi cha Nyerere then huwezi uka'comment chochote kuhusu Mwinyi, maana hata kama ungezaliwa siku wanayokabidhiana madaraka, then ungekuwa na hardly miaka 10 siku Mwinyi anapotoka...ambapo pia huwezi kueleza material thing!

Hapa hii mambo itakuwa tamu zaidi kama watapatikana watu walioonja "live" maisha yote ya hawa viongozi wakatusimulia, kuliko kuyapata toka kwa waliosimuliwa au kusoma kwenye vipeperushi!
Thats just my notion.
 
NYERERE
nyerere alikuwa dictator mkubwa katika awamu yake hakuruhusu freedom of speech kama ukitoa maoni kuhusu serikali basi wewe unaonekana ni mhaini ,wananchi walikuwa masikini kupita kiasi kutokana na siasa yake ya ujamaa .nguo za watu zilijaa viraka ,kila kitu madukani ilikuwa kwa foleni mchele ,sukari,unga,sabuni na n.k .watu waliokuwa wanatanuwa katika kipindi chake ni mawaziri peke yao ,mtu wa kawaida ukionekana una mali kidogo basi wewe utaletewa polisi usawa uwo uwo.alijifanya kwamba yeye ni mpigania uhuru lakini kumbe muongo mkubwa kwasababu british ilikuwa uhuru wautoe anyway ,alipiga kelele kuhusu wizi serikalini wakati yeye ni mwizi mkubwa alijilimbikizia mali kibao ,alikuwa silent killer amewaua viongozi kibao ambao walimpinga na siasa zake ,marehemu sokoine,kigoma malima etc na vile nusura amuondoe mwinyi
kwakweli kama bado anaongoza nchi basi huu mtandao tungeuwona kama kituo cha polisi mana sie sote hapa tungekuwa wahaini .nchi ilimshinda akaamua kumtupia mwinyi .
MWINYI
alichukua nchi katika hali mbaya sana lakini alitufunua macho aliondosha kila kitu cha nyerere regime ideology na economically.uchumi ulikuwa,pesa kibao,emplyment zilikuwa nyingi kutokana privatization na free trade ,freedom of speech kwamfano vyombo vya habari binafsi vilianzishwa .hata masikini walianza kumiliki magari na luninga
tatizo la mwinyi alikuwa mpole .
MKAPA
alianza vizuri lakni alimaliza vibaya kwa kuanza kula kwa pupa
JK
sorry sipo nyumbani lakini nasikia anapenda holiday na anashindwa kuwafukuza kazi wala rushwa kwasababu ni rafiki zake.
kama nyerere hakuongoza tz basi hii nchi ingekuwa mbali sana kiuchumi na matatizo mengi kama ya muungano yasingekuwepo ,kitu muhimu tulichojifunza kutoka kwa nyerere ni kwamba ujamaa ni siasa mbovu katika kuendeleza nchi .
 
Nyerere: alitushughulikia kisaikolojia tukamwona Mungu mtu
Mwinyi: Mzee wa ruksa, kila kitu fanyeni
Mkapa:Mbabe
Kikwete: Anajirusha na kuuza sura
 
Kila mtu amekuja na era yake nzuri tu. Hakuna mbaya hata mmoja. Hakuna kigezo chochote cha kusema kuna mbaya. Kama basi ni ubaya basi atakuwa Nyerere aliyepona coup de tats!Wengine wote ni wazuri, hatujawhi kuingia barabarani kuipinga serikali au rais wetu.
Kwa maana nyingine tuwache chokochoko hawa wote ni wazuri. tatizo ni kwamba hatuangalii vitu kwa undani wake na wakati wake. Kila mtu aangaliwe ni wakati gani (era) alishika madaraka na hali ilikuwaje? Kivingine "none of the is an angel, hence they all have their deficenices"!!!!
 
Kila mtu amekuja na era yake nzuri tu. Hakuna mbaya hata mmoja. Hakuna kigezo chochote cha kusema kuna mbaya. Kama basi ni ubaya basi atakuwa Nyerere aliyepona coup de tats!Wengine wote ni wazuri, hatujawhi kuingia barabarani kuipinga serikali au rais wetu.
Kwa maana nyingine tuwache chokochoko hawa wote ni wazuri. tatizo ni kwamba hatuangalii vitu kwa undani wake na wakati wake. Kila mtu aangaliwe ni wakati gani (era) alishika madaraka na hali ilikuwaje? Kivingine "none of the is an angel, hence they all have their deficenices"!!!!
NANU,
Mtazamo wako ni mzuri sana.
Kila mtu anathamani yake kulingana na wakati siyo?
 
awamu ya nne bwana; daaaaaaaaaaaaaaaahh..mambo yote yamekwenda mrama sasa, almost hamna raisi hapa; mtu hata hajui ni kwa nini TZ ni maskini? imagine that! raisi hajui ni kwa nini nchi yake ni maskini..unategemea atafanya mikakati endelevu ya kuondoa umaskini nchini..ni raisi muuza sura kuliko maraisi wote waliowahi kutokea in the history of this nation!!!!!! ever
 
Nyerere:The best president ever
Mwinyi:Aliuza madawa ya kulevya na wife wake,ni kilaza tuu,alitaka kuifanya tanzania iwe uNITED iSLAMIC rEPUBLIC oF tANZANIA,hana vision,kauza loliondo kwa waarabu mashemejize,aliua azimio la arusha akiwa zanzibar,alikuwa kivuli cha rais,hana sifa za kuwa rais
Mkapa:Ni fisadi period baada ya Nyerere kufa
Kikwete:ni kiazi kama babu yake mwinyi,ni mmiliki wa IPTL,anamiliki mtandao wa kidini wa kigaidi ulioko wenye makao maku yake lamu,anaongozwa na mafisadi,...
 
Nyerere:The best president ever
Mwinyi:Aliuza madawa ya kulevya na wife wake,ni kilaza tuu,alitaka kuifanya tanzania iwe uNITED iSLAMIC rEPUBLIC oF tANZANIA,hana vision,kauza loliondo kwa waarabu mashemejize,aliua azimio la arusha akiwa zanzibar,alikuwa kivuli cha rais,hana sifa za kuwa rais
Mkapa:Ni fisadi period baada ya Nyerere kufa
Kikwete:ni kiazi kama babu yake mwinyi,ni mmiliki wa IPTL,anamiliki mtandao wa kidini wa kigaidi ulioko wenye makao maku yake lamu,anaongozwa na mafisadi,...[/QUOTE]


ebu dadavua hiyo habari
 
Mtoa hoja ni mchanga wa historia ya nchi hii.Tanzania kabla ya vita na Uganda tuliishi kwa shibe na amani. Ni baada ya 1980 ndo dhiki ilianza. Nchi haikuwa na wataalam wa kutosha wala teknolojia iliyo juu kama ya sasa. Benchmarking inaangalia timeframe, industry na aina ya firm.Mtoa mada kalewa na unafiki wa kibepali, huko aliko anafanya kazi kama Punda na bado saving yake ni kiduchu. Kwa kifupi viongozi wetu ni safi ila wameongoza kwa vipindi tofauti ndani ya maendeleo yenye nyanja tofauti. Muunguja amekuwa mvivu wa kufikiria.
 
Back
Top Bottom