The Quonquerer
JF-Expert Member
- May 14, 2009
- 777
- 111
But also, sijaliona kama suala la woga kwa Tanzania. Kwa Muungano si suala la hiari? Sisi tulichelewa na kuahirisha maendeleo yetu, tulijotoa mhanga, muda na mali zetu kukomboa nchi za kusini mwa afrika na nyingine zilizokuwa zinakandamizwa. Wakati sisi tukigoma kufanya biashara na makaburu, na wengine kama wao, Kenya walifanya mchana kweupe! Hawa wali-support ubaguzi wa rangi dhidi ya waafrika kama wao. Je ni watu wa kuamini na kuishi nao hawa. Kwanza utamaduni wetu hauko compatible! Baada ya miaka yote hiyo ya hasara, je tunalazimika kupelekwa mbio na watu ambao tulikuwa tuko milengo miwili tofauti. Nadhani si suala la biashara peke yake, kuna zaidi! Smatta, uache watu watoe maduku duku yao, siyo kusema unachukiwa. Lugha huwa ina vionjo pia, kwa hiyo take it easy, watu wakupe vidonge, ukishindwa kumeza viteme. Isn't this a forum where we dare to talk openly! Mi umenitukana ila sijali, cha msingi ni kile ninachosimamia! Hivyo ni vionjo tu.