MJINI CHAI
JF-Expert Member
- Dec 12, 2010
- 2,198
- 1,226
kwa kuwa umesema Tanzania ni mali...........Basi ni mali ya kuokota ambayo aliyeipoteza bado hajajua kuwa ameipoteza......ngoja siku akitambua......
Nchi ni nchi, na mali ni mali. Kusema nchi ni mali huo ni ujinga tena wa wazi wazi. Kama nchi ni mali haya itumie basi Tanzania. Mie nakupa Tanzania yote yako chukuwa wewe, pata wewe, haya umeshakuwa na mali. Hata wewe binafsi yako sio mali, haya jiuze basi kama wewe mali.
Huna hoja, una viroja.
Ni mali yetu sote mkuu ila ndo hivyo, sijui dunia inataka kufikia kiama?Wakuu,
Tunapoendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mambo ya kitaifa yaliyoko mbele yetu, hususan mchakato wa kuandikwa kwa katika mpya, naomba kuuliza swali. Nahisi pamoja na mambo mengine, katiba mpya itatakiwa kuwa na ibara inayolitaja taifa letu Tanzania. Katika kufikiria hayo nimepata swali ambalo pengine laweza kuonekana jepesi lakini kumbe gumu. Hivi; Tanzania ni mali ya nani? Naomba mtazamo wenu kisha tujadiliane
hawa ni wale wanaoambiwa kuwa Dhahabu iliyopo kahama,almasi iliyopo Mwadui,kahawa iliyopo kagera, korosho zilizopo mtwara, mbuga za wanyama zote na pesa zilizopo hazina/ BOT ni mali yetu wanaitikia kuwa ni kweli zao......Chako ni kile ulichonacho na unauwezo wa kukitolea maamuzi....
MY WORD IS MY BOND...
mungu..
Tanzania ni mali ya Watanzania wote.
Swali: je, Mtanzania ni nani?
Jibu: Mtanzania ni yule mwenye maisha bora hadi sasa. Hii ni kwa sababu kila aliye Mtanzania ali ahidiwa maisha bora. Kwa maana hiyo kama huna maisha bora hadi leo hii basi wewe sio Mtanzania na Tanzania utaiona ngumu. Tanzania in wenyewe...na wenyewe ndio Watanzania.
Maisha bora kuyangoja JF? Sahau. Hapa tuwachieni sisi semi retired, vijana mkachakarike at least 14 hours every day. Hii ni kwa vijana wote wa miaka 18 mpaka 50. Nakuhakikishia ukijituma inavyotakiwa hutolalamika maisha magumu.
Nimetembea sana duniani, ni nchi chache sana zenye fursa za kujiwezesha haraka haraka kama tulizonazo Tanzania kwa sasa. Amini usiamini huo ndio ukweli. Lakini ikiwa kutwa kucha unajificha kwenye mtandao hutoziona maisha yako.
JF ni sehemu ya kuchakarika. Huwa sipati msukumo wa kuchakarika ninapokuwa mpofu wa habari/taarifa. Taarifa kwangu ni chachu ya kunichakarisha...nikitoka JF huwa naingia kitaa kama mbogo mjeruhiwa. Lakini sijasema kama mimi ni Mtanzania au la! pengine ninge enea katika ujumbe wako moja kwa moja.Maisha bora kuyangoja JF? Sahau. Hapa tuwachieni sisi semi retired, vijana mkachakarike at least 14 hours every day. Hii ni kwa vijana wote wa miaka 18 mpaka 50. Nakuhakikishia ukijituma inavyotakiwa hutolalamika maisha magumu.
Nimetembea sana duniani, ni nchi chache sana zenye fursa za kujiwezesha haraka haraka kama tulizonazo Tanzania kwa sasa. Amini usiamini huo ndio ukweli. Lakini ikiwa kutwa kucha unajificha kwenye mtandao hutoziona maisha yako.
Hao au nyie mnaouliza Tanzania mali ya nani?
Mali huwezi kuipata kw kukaa na kuuliza eti nchi na mali ya nani? huo ni upunguani wa hali ya juu. Wewe unaeojioan kuwa una mali, mbona huna? ungekuwa na mali ungejuwa mali ni nini na usingefikiria kuwa nchi ni mali.
Huo ujanja umeupata lini hata leo ujidai Tanzania ni mali ya nani? nani alikuambia Tanzania mali? Mali iko huko magharabi.
Nyie ni mapunguani msiojuwa mali ni nini. Hiyo tanzania kaa uitazame jina tu. Kama unataka kujua Tanzania mali ya nani basi ni ya Muhindi wa Tanga aliyoipa jina Tanzania. Haya unalo?
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete = Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Mohamed Gharib Bilal = Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Ali Mohamed Shein = Rais Serikali ya Mapinduzi, Zanzibar.
Hao wote ni Raia wa Tanzania. Wewe na mimi ni Raia wa Tanzania.
Mali iko wapi hapo? usituletee akili za mbege saa hizi.