Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,453
- 113,461
Wanabodi,
Hii nimeitoa kwa Mwandishi wa Waziri Mkuu.
Kwa: Whariri Wote;
SERIKALI inakamilisha uanzishaji wa Kituo Maalum (China Tanzania Logistic Centre) kwa ajili ya kuzipatia nchi za Afrika Mashariki na Kati bidhaa zenye ubora wa kiwango cha juu kutoka China badala ya wafanyabiashara wa nchi hizo kuzifuata huko.
Hayo yalitangazwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Cyril Chami wakati akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuzindua Bodi mpya ya Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) jijini Dar es Salaam Jumanne iliyopita.
Ili kuepukana na hatari ya kuupoteza mradi huu muhimu ambao tayari unanyemelewa na baadhi ya nchi hapa Afrika tunajitahidi kupata fedha hizi kutoka Bajeti ya serikali au kupata mkopo kutoka TIB (Tanzania Invstment Bank, Dkt. Chami alisema.
Fedha zinazohitajika ni Sh. Bilioni 60 kulipia fidia ya kuwaondoa watu waliojenga kwenye makazi yasiyo rasmi eneo la ekari 60 Kurasini jijini Dar es Salaam, ambalo wawekezaji hao wanalipendelea badala ya eneo la Uwekezaji la Bagamoyo.
Mradi huo utakuwa wa awamu mbili ya kwanza ni ujenzi wa kituo hicho na ya pili ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, maeneo ya biashara, masoko ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali, majumba ya maonyesho na mikutano na maofisi, huko Bagamoyo.
Dkt. Chami alisema makubaliano yaliyofikiwa na Serikali ya China ni kujenga kituo hicho kwa mfumo wa ubia ambapo Serikali ya China itatoa fedha zote za ujenzi wa miundombinu na mtaji wa kuanzia na Serikali ya Tanzania itatoa eneo la ujenzi.
Serikali ya China itawakilishwa na Ushirika wa Yiwu Pan-Africa International Investment Corporation na Serikali ya Tanzania itawakilishwa na Mamlaka ya EPZA.
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, inaielekeza Wizaraya Viwanda na Biashara kuhamasisha uanzishwaji wa EPZ na Maeneo Maalum ya Uwekezaji (SEZ).
Katika miaka mitano iliyopita Bodi ya EPZA ilisajili Makampuni 63 yanayozalisha chini ya mfumo wa EPZ na kutengeneza ajira 14,000 za moja na 60,000 zisizo za moja kwa moja na Dola za Marekani Milioni 712 zimewekezwa na nyingine Milioni 390 zimeingizwa kutokana na mauzo ya bidhaa nje. (mwisho)Imetolewa na: Ofisi ya Waziri Mkuu, S.L.P. 3021, DAR ES SALAAMJumapili Machi 10, 2012
My Take:
Jee mradi huu ni ukombozi wa kweli kwa wafanya biashara wanaofuata bidhaa mbalimbali nchini China, hivyo kuzipatia humu humu nchini kwa urahisi, na kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa mazagazaga yote?!.Jee ujio huu sio tuu utaleta zile cheap products na mazagazaga yote kutoka China kwa kuihamishia Ghwanzou hapo Kurasini, ambayo ni maarufu duniani kwa kufyatua fake na couterfate products?!. Japo at initio stage unaonyeshwa ni mradi wa ubia kati ya Tanzania na China, ukweli ni kuwa sisi baada ya kuwapa eneo, 100% investment ni ya Mchina japo kila kitakacho tengenezwa kitakuwa made in Tanzania with Chinese brand names kwenye kila kitu kitakachoundwa hapo! What will become with ile ndoto yetu ya Tanzania kufufua viwanda vyetu ili tutawale soko la Afrika Mashariki?. Jee ujio huu unaweza kuwa ndio kiashiria cha mwisho wa utawala wa Wahindi kwenye biashara zote?. Jee vile viwanda vyetu vidogo vigo na ulupuaji wetu, tutaweza kustahili ushindani na Mchina?. Tumemkaribisha wenyewe Mchina ili kutuletea neema, jee hii itakuwa ni neema ya kweli, au ni "A Blessing In Disguise?!.
Welcome to "New China Town Kurasini!,
Pasco.
Hii nimeitoa kwa Mwandishi wa Waziri Mkuu.
Kwa: Whariri Wote;
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI