Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

CECAFA, AFICON, FIFA waanzishe kombe la UFISADI tuwaonyeshe cha mtema kuni... teh....teh.
 
Mechi 4 mfululizo tumepigwa bila kuscore hata goli moja, na huku kibabu sijui Malinzi ana agenda gani na huyu babu
 
Unajua unaweza kuwa nje ya jambo ukaona walioko ndani wanakosea ukiingia unapewa za uso mpaka unachanganyikiwa kama hivi sasa hujui ushika wapi urekebishe nini
 
All the best to our Football National Team

Huu ni mwaka wa mabadiliko nasi tumeanza kuyaona kwani mafanikio yanaanza kuonekana
 
Vitabu vya dini vinasema kukata tamaa ni dhambi mimi binafsi sijawahi kuwa nafuraha na hizi timu zetu tangu nijitambue pindi pale zinaposhiriki nje ya mipaka ya afrika mashariki huwa ni kawaida yao kuboronga na naamini watanzania wengi huwa hawana imani na hizi timu zetu hata ukikuta mtu anasema kwa kujiamini kwamba tutashinda mbele za watu, ila kwenye nafsi yake anaamini hicho kitu hakiwezekani ivyo anafanya tu kwa tiba saikoloji ya maumivu kiukweli huwa inaumiza sana.

Mimi naona serikali huwa inajaribu kujitutumua lakini tatizo hasa kujulikana ni kitendawili huwatuna mashindano ya copa coka cola lakini madudu ya kule usiseme vijana wanaofanya vizuri kwenye wilaya zao wanaachwa wanachukuliwa ndugu, jamaa na watoto wa viongozi wa benchi la ufundi na makocha kuwakilisha ngazi ya mkoa hapo tena mkoani wale wenye nguvu huendelea kupitisha magwese ngazi ya taifa huko ngazi ya taifa utaona robo tatu yao watakao fanikiwa hata kuonwa na vilabu au kuchukuliwa na timu ya taifa ya vijana wote wanatoka DAR! Hivi unatarajia mabadiliko gani?

Timu inakuwa na kamati zaidi ya kumi kweli huo sio mradi wa watu jamani?Hii inatokea kwa tanzania tu!!lawama kila siku zinaenda kwa makocha bila kuangalia mfumo wa TFF namna unavyoendeshwa na watu wa hovyo kuanzia kwenye ngazi za kuibua vipaji, ligi mpaka uundaji wa timu ya taifa ambayo mara nyingi huundwa na Simba na Yanga na kwa mbali sasahivi Azam.Watu wanakaa wanajifariji eti hata brazil ilifungwa saba, huku wanajisahau kwamba Brazil inamafanikio gani kisoka na Taifa Stars inamafanikio gani?

NB: NDUGU WATANZANIA MABADILIKO HUANZA NA WEWE JE KWA UPANDE WAKO WEWE UNGEPENDA NINI KIFANYIKE ILI KUINUA SOKA LETU AMBALO LIMEPOTEZA DILA KABISA
 
Timu yetu ya taifa leo imefundishwa mpira na Algeria kuwa kuipgwa 7-0! Hii ni rekodi.Sijawahi ktk akili zangu timamu kuwahi kusikia Tz ikipata kisago cha aina hii. Sote tunawajibika lakni wewe ni zaidi.

Kwa mtazamo wangu wewe mwalimu wetu, pamoja na ubora wa Algeria, umeonesha udhaifu mkubwa sana ktk michezo yote miwili. Kama ungekuwa makini zaidi tungeweza kupunguza aibu hii ya milenia kwa mchi yetu.

Udhaifu wako mkubwa unatokana na kuendana na matakwa ya mashabiki hasa wanaoendekeza unazi wa Simba na Yanga. Ukiendelea kufanya hivi utaipoteza timu haraka na utajikuta unakalia kiti cha moto.

Udhaifu wako pamoja na benchi lako la ufundi unatokana na kile ulichodai kuwa sub ulizofanya taifa ndio ziliigharimu timu kitu ambacho si kweli. Ulifanya hivi kuwarishisha watu fulani ili kuficha udhaifu wa kweli wa timu ambao ni kupoteza umakini kwa defence yetu(loss of concentration). Unajua kuwa magoli yalirudishwa sio kutokana na timu yetu kuzidiwa na mashambulizi, la hasha! Ilitokana na ukosefu wa umakini wa walinzi wetu hususani Ngwali na Cannavaro. Unajua goli la kwanza lilifungwa wakati walinzi wetu wakimiliki mpira na kupigiana pasi za hapa na pale na walipopokonywa goli likafungwa. Unajua pia kuwa morali ya timu ilishuka sana baada ya goli hilo kiasi cha kurudia makosa yale yale yaliyopelekea goli la pili. Wewe ni shahidi kuwa Algeria walikuwa wameshapoteana kabisa baada ya kufungwa magoli 2, na kwamba magoli yao ilikuwa ni sawa na kuokota embe jangwani. Narudia tena, pamoja na sub zetu Ndemla na Ngassa kushindwa kufanya jipya ktk timu, lakini Mkwasa na benchi lako mnajua magoli waliyopata Algeria hayakutokana na pressure yao kuwa kubwa kwenye lango letu, laa bali udhaifu wa ulinzi na utumiaji wao bora wa nafasi.

Hapa ulijiweka ktk mtego wa kujiaminisha kuwa timu ile ya kwanza iliyoanza Taifa ndio ilikuwa bora zaidi na kwa maana nyongine ulitaka icheze hiyohiyo tu, nadhani tena bila sub!!!!! Inaweza kuwa kweli lkn hukupaswa kukariri. Hukupaswa kuwaza kishabiki, wewe ulitakiwa kuzingatia weledi wako kuelewa tatizo ilikuwa nini kiufundi. Ulipaswa kuangalia mazingira ya mechi.

Na ni kosa hili tena ndio limepelekea timu kupigwa kipigo cha milenia leo huko mjini Blida, Algeria. Tatizo sio kuwa kikosi chetu ni wabaya, hapana, tatizo ni kukariri na mazoea bila kujali mazingira ya mechi.Ulishindwaje kujua kuwa ni makosa kuanza na fowadi watatu hadi wanne ugenini kupishana na timu kama Algeria? Hebu fikiria wao walipokuja taifa pamoja na ubora wao lkn waliweka washambuliaji wawili tu na wakati mwingine akawa anabaki 1. Lkn wewe kwa sifa za Dar ukaona uweke 3!!!

Kutokana na ubora wa Algeria lkn ulipaswa kubadilisha mbinu kidogo tu ili kuwachanganya ambapo ktk nafasi ya Maguli, ungemwanzisha Malimi Busungu, kucheza kama winga mwongo wa kulia lkn mwenye majukumu makubwa ya ukabaji na kumsaidia Kapombe na hapo hapo kutengeneza nafasi kutokea winga ya kulia.

Samatta alipaswa kuanzia kushoto kwenye nafasi ya kijana Farid Mussa na mshambuliaji wa kati angekuwa Thomas Ulimwengu wakati kiungo cha ukabaji wangecheza Mkude na Himid Mao huku ukimpunguzia kazi ya ukabaji kijana mdogo Mudathir Yahya ambaye angeweza kusaidia kulainisha mipira na kuipandisha timu.

Kutokana na tamaa ya kushambulia, umewapa kazi sana Himid Mao na Mudathiri kuwakaba Algeria kiasi cha kusababisha timu kufa katikati, huku muda wote mipira ikiwa miguuni mwa Algeria na kuwapa wakati mgumu sana walinzi wetu. Narudia tena pamoja na ubora Algeria lkn Mkwasa nabenchi lako umewarahishia sana kazi.
 
Timu yetu ya taifa leo imefundishwa mpira na Algeria kuwa kuipgwa 7-0! Hii ni rekodi.Sijawahi ktk akili zangu timamu kuwahi kusikia Tz ikipata kisago cha aina hii. Sote tunawajibika lakni wewe ni zaidi.

Kwa mtazamo wangu wewe mwalimu wetu, .

usiendekeze tabia ya kulaumulaumu, elewa mleta mada anataka nini ndo uanze kutoa maoni
 
Tutafute madogo 50 under 17 tuwalipie ada huko ulaya kwenye soccer academy!!
Kati ya hao 50 ,ndani ya miaka 4 hatuwezi kukosa wachezaji 11 wa maana.
 
Hoja hapa kwanza tuwekeze kwa kuzalisha makocha bora, kisha tume kuwekeze kwa watoto vijana. Watu wengi wanasema tuwekeze kwa vijana, swali kwa makocha gani? Hawa wanaoshindwa kwenda kufundisha hata Comoro?
 
Afadhali hakuna mchezaji wa Simba aliyecheza. Kwa ufupi, ukuta wa timu ya Kimataifa ndio ulioleta aibu hii. Mbona Jenny Muro hajitokezi kuwapongeza Wakimataifa?
 
Mimi wala sikupata shida ya kuangalia mechi ya jana. nilijua tutafungwa ingawa hayo magoli saba sikutarajia. Hata hivyo haya ni matokeo ya mfumo wetu wa kijamii, kiuchumi na kisiasa. Suala la soka la Tanzania ni mjadala mzito. Tatizo lililopo siyo kwenye soka tu bali ni mfumo mzima wa maisha katika nchi yetu. Uozo upo kila mahali. wapi Tanzania tumefanya vizuri? Kwa upande wa soka uozo umeanzia kwanza kwenye uongozi wenyewe ambao unaingia madarakani kwa rushwa. wachezeshaji nao wanachezesha, kwa maana ya marefarii, kwa rushwa. Watu wanafanya lobbying waingizwe kwenye kamati kwa lengo tu la kutangazwa. hivi mnafahamu chini ya tff ya sasa kuna kamati ngapi? kamati nyingine hazijawahi hata kukutana. watu wanafanya lobbying ili wawemo kwenye kamati kwa ajili ya sifa kwamba nao wako kwenye kamati. michezo mingi ya ligi kuu matokeo yake yameshaamuliwa hata mchezo haujaanza. Refarii anakupigia simu wewee kiongozi kuwa nimefikia mahali Fulani maana yake nini. kama marefarii ni wala rushwa ina maana wachezaji wetu ni shida kucheza mechi za kimataifa kwani watapata kadi nyekundu kwa rafu ambazo kwa refarii wa kwetu asingetoa red card. Wachezaji wenyewe wa kwetu wana vipaji lakini tabia na akili yao ni ya kitanzania, hawajitumi, wapenda sifa, hawafanyi mazoezi, hawana nidhamu ya mhcezo wala maisha. ni walalamishi kwa kila kitu kama ilivyo tabia ya mtanzania. Hivi mnajua kuwa ukisafiri na timu ya Tanzania upo wakati wewe kiongozi unalzimika upite kila chumba cha mchezaji kuwaamsha kuwa saa ya mazoezi imefika? Niliwahi kuongea na mchezaji mmoja maarufu ambaye alikwenda ufaransa na uswizi kufanya majaribio. alinieleza kuwa wakati mchezaji wa Tanzania anafika uwanjani kwa majaribio anakuta wachezaji wa Nigeria na nchi nyingine za afrika magharibi wameshafika saa mbili kabla ya muda wa kawaida na taayari wameshajifua kivyao kivyao....
 
Tutafute madogo 50 under 17 tuwalipie ada huko ulaya kwenye soccer academy!!
Kati ya hao 50 ,ndani ya miaka 4 hatuwezi kukosa wachezaji 11 wa maana.

Wazo zuri sana ,Hivi si ndo kuna mpango huo kwa kushirikiana na club ya RM chini ya mpango wa NSSF ? Au huu ukoje?
 
Back
Top Bottom