Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

Mpira fitna siku hizi...Tff wapo kimaslahi zaidi fitna hawazijui hata kama wanazijua basi wabahili kufanya hivyo.Maana Tanzania tukiwa nyumban hakuna tofauti na tukiwa ugenini.Tusipofanya fitna tutaishia kusindikiza wwnzetu tu miaka yote.
 
Nashangaa ni rais tu anapata ma tuzo kila mara sijui ya nini lkn raia hawapati.
kule commonwealth tumeboronga. taifa stars tumeboronga. Wakati Kenya kuna kalenda ya michezo huku kwetu watu wa kwenda kushindana na USAIN BOLT wamekaa kambini kwa mazoezi wiki mbili. I ask myself is Mr. Filbert Bayi doing this delibarately or kuna kitu imefichamana. IF YOU DO NOT PLAN. SURELY YOU PLAN TO FAIL.

Hatuna kipya Bongo. Business as usual.
 
PICHA ya Gazeti la Mwananchi iliyopigwa na Mahmoud Zubeiry jana ukurasa wa 32 inamuonyesha beki wa Timu ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars', Shomary Kapombe akilia kwa uchungu baada ya Stars kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Afrika katika kufuzu hatua ya makundi na Msumbiji.

Unajua kwa nini Kapombe ameumia? Sababu ni rahisi tu. Msumbiji wametutoa kwa ushindi mwembamba sana. kwetu tulitoka nao sare ya mabao 2-2. Kwao wametufunga 2-1. Wametutoa kwa jumla ya mabao 4-3.

Kwa hesabu rahisi inaonekana wametutoa kwa urahisi. Kapombe analia. Mbwana Samatta naye anakaa katika nyasi za uwanja anatamani kulia. Timu imefungwa. Tumekosea wapi? Ndiyo swali lao.

Katika miaka ya karibuni, ndani ya utawala wa kocha wa zamani, Marcio Maximo timu ilikuwa inakwenda vizuri. Wachezaji vijana walikuwa wanachipukia ndani ya timu ya wakubwa na katika timu za vijana tukianzia kwa kocha Marcos Tinocco.

Katika timu ya wakubwa tukaanza kushindwa kidogokidogo. Hata pointi zetu katika makundi ya kufuzu kwenda kombe la dunia au Afcon hazikuwa mbaya. Kuna wakati tulimaliza kundi letu na pointi tisa.

Tukamuondoa Maximo akaja babu, Jan Poulsen. Yule naye akaanza kutuliza machozi kama haya ya Kapombe. Mipango yake ilikuwa ya muda mfupi kutokana na umri wake.

Akatuchagulia wachezaji vijeba wa mipango ya muda mfupi. Akatuliza machozi kwelikweli.

Kocha wake wa vijana alikuwa Kim Poulsen, huyu alikuwa anatupeleka vizuri katika soka la vijana, akawafahamu vijana wengi mahiri, akawapika vizuri akina Simon Msuva. Lakini kule juu tukamuona Jan hafai, tukamuondoa, nafasi yake tukampa Kim Poulsen.
Huyu aliturudisha katika zama za Maximo, timu yake ya wakubwa aliwaingiza vijana wake wa chini na ilikuwa wazi kwamba alikuwa na mipango ya muda mrefu.

Kwa ujinga wetu, tukamuondoa Kim eti kwa timu kutofanya vizuri michuano Chalenji. Kumbe wakati huo Kim alikuwa anajaribu kutafuta timu ya baadaye. Kwa ujinga zaidi, Kim akaondolewa kwa siasa za uchaguzi wa TFF kutokana na viongozi walioingia madarakani na jazba za kufagia kila kitu.

Na sasa ameingia Mart Nooij tumeanza upya na tumeanza kwa kulia kama Kapombe alivyotuonyesha. Mbaya zaidi ni kwamba kwa mwendo huu tunaokwenda nao Kapombe anaweza kulia mpaka atakapostaafu soka.

Kwa nini ataendelea kulia? Ni kwa sababu hata huku chini katika timu ya vijana tumevuruga. Umeiona Serengeti Boys? Inaonekana wazi kwamba haina vijana wenye uwezo au haifundishwi na watu wenye uwezo.

Waliopo wamechaguana kienyeji tu. Wachezaji wa leo wa Serengeti ndiyo wachezaji wa baadaye wa timu ya taifa.
Ina maana kilio kitaendelea hivi hivi. Kilio kitakuja kukoma pale tutakapoanza kuwa makini na soka. Kilio kitakoma wakati tutakapoachana na njia za mkato.

Nilikuwa namuona Kim Poulsen alipokuwa anatupeleka. Falsafa yake ilikuwa wazi. Lakini watu wakamfukuza kwa madai ya kwamba alifeli michuano ya Chalenji. Michuano ambayo licha ya kwamba tumechukua mara tatu hatujawahi kuingia katika orodha ya nchi 70 bora katika soka duniani.

Anachokifanya Kapombe ni kutusaidia kulia tu sisi wengine ambao tumekuwa tukilia kwa muda mrefu kutokana na udhaifu wa soka letu. Virakaviraka vya soka letu vitaendelea kutuliza kwa muda mwingi ujao. Acha tuendelee na mipango ya muda mfupi!

Source : MwanaSpoti
 
Nilikuwa namuona Kim Poulsen alipokuwa anatupeleka. Falsafa yake ilikuwa wazi. Lakini watu wakamfukuza kwa madai ya kwamba alifeli michuano ya Chalenji. Michuano ambayo licha ya kwamba tumechukua mara tatu hatujawahi kuingia katika orodha ya nchi 70 bora katika soka duniani.
i

attachment.php

 

Attachments

  • viwango.png
    viwango.png
    17.5 KB · Views: 740
nimeumia sana baada ya rafiki yangu mganda kuniambia "Tanzania national team is worst in east africa''
 
No way out taifa stars inabidi kupumzika mashindano ya kimataifa atleast kwa miaka miwili tukipange.
 
Taifa Stars imejilaza ICU inapumulia mashine

HAUTAIKUTA hospitali yoyote nchini, lakini Taifa Stars inaumwa sana. inahitaji msaada mkubwa. Ina magonjwa mengi ambayo hayawezi kutibika kirahisi, ni tofauti na wengi wanavyofikiri.

Ugonjwa mkubwa wa Stars unaanzia nje ya uwanja. Nani anaitaka Taifa Stars ya sasa? Hakuna. Mashabiki hawaitaki, wachezaji hawaitaki. Nahisi hata Rais Jakaya Mrisho Kikwete naye haitaki Stars ya sasa. Anashindwa kusema tu.

Duniani kote hakuna mchezaji aliyetajirika kwa kupitia timu yake ya taifa. Hii ni timu ya hiyari. Gurudumu lake linaendeshwa kwa mapenzi kati ya wananchi na mashabiki. Wachezaji wanatajirika kupitia klabu zao.

Lakini wachezaji wa Taifa Stars hawaitaki timu kwa sababu mashabiki hawaitaki timu. Mbrazili mmoja alisafiri zaidi ya kilomita 5,000 katikati ya mwaka 2006 kwa ajili ya kuleta muunganiko huu. Marcio Maximo.

Hata hivyo, kile si kitu cha kujivunia sana. Wachezaji na mashabiki wanapaswa kuungana muda wote linapokuja suala la timu ya taifa. Inachekesha, Maximo alipoondoka na uzalendo ukaondoka.

Katika taifa la dunia ya tatu, ambalo lina ligi ya kawaida tu huku likiwa halina wanasoka wanaotamba Ulaya, uzalendo ndio dawa ya kwanza kumfanya adui apate wakati mgumu anapocheza na nyinyi. Lakini hauwezi kuamini, Wajerumani wanaojua sana soka kwa sasa duniani wana uzalendo zaidi kuliko Watanzania wote.

Ugonjwa wa pili mbaya vilevile ni ule wa Kocha, Mart Nooij. Bado kocha hajatusaidia. Tuliambiwa maneno mengi kwamba TFF mpya ingekuja na kocha wa Kidachi kwa madai kwamba ni mafundi sana wa soka. Ilikuwa sehemu ya kampeni na siasa tu za soka la Tanzania.

Nooij haeleweki hata kidogo. Ndani ya uwanja timu ina mapungufu mengi. Hakuna uwiano mzuri kati ya ushambuliaji na ulinzi. Unabaki kujiuliza tu, anawajua vizuri wachezaji wa Kitanzania? Ni kweli wapo katika viwango vya mfumo anaoutaka?
Hata kama tunahitaji mabao, tena tukiwa katika uwanja wa nyumbani, unawezaje kuwapanga kwa pamoja, Mbwana Samatta, John Bocco, Thomas Ulimwengu na John Bocco? Wote hawa si wakabaji wazuri na hawawezi kurudi nyuma kwa haraka wakati wapinzani wana mpira.

Nyuma yao, Nooij anawapanga Erasto Nyoni na Mwinyi Kazimoto. Katika soka la kisasa, mpinzani anajaza viungo wanne hadi watano, wewe unawaweka Mwinyi na Erasto peke yao, unatagemea nini? Ndio maana Msumbiji walituchafua vibaya pale Uwanja wa Taifa.

Ndio maana kupitia mechi za timu ya taifa, sasa hivi tunaanza kuona mapungufu ya Kevin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro' ingawa katika Yanga hayaonekani sana.

Maximo alikuwa mwoga. Alijaza viungo wengi eneo la katikati kwa sababu alijua udhaifu wetu kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja. Katikati ya uwanja angeweza kuwapanga Shaaban Nditi, Henry Joseph, Athuman Idd na mbele yao kidogo angecheza Nizar Khalfan.

lisaidia sana kutokana na aina ya wachezaji tulionao Tanzania kwa sasa. Hawawezi kupishana na Cameroon, Ivory Coast, Ghana hata Msumbiji. Lakini Nooij anaichezesha Stars kama vile ni timu kamilifu.

Kim Poulsen alijua soka la kutandaza, lakini bado alikuwa anaweka viungo watatu hadi wanne pale katikati. Vipi Nooij na wachezaji wake wa sasa. Anadhani wapo katika viwango vya Yaya Toure?

Ugonjwa mwingine ambao ni mbaya zaidi kwa Taifa Stars ni ule wa kukosa mwelekeo na malengo. Tunataka kufuzu michuano gani? Kwa kutumia wachezaji gani? Kocha anafahamu tunachotaka?

Kocha aliyepita, Kim Poulsen alikuwa na malengo yake. Kabla ya kuchukua nafasi ya Jan Poulsen yeye ndiye alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana. Alipopanda kuwa kocha mkuu alishawaelewa wachezaji wa timu ya vijana na uwezo wao. Alishawaelewa vema akina Frank Domayo, Simon Msuva, Atupele Green, Issa Rashid, Manyika Peter na wengineo. Alikuwa anatazama mbali kidogo.

Lakini pia alishajua jinsi ya kuwatumia wachezaji wakubwa wa Kitanzania. Stars ilikuwa inacheza pasi fupi fupi na za haraka. Mwelekeo ulionekana. Mwenyewe alijiwekea lengo la kwenda Morocco lakini watu wakamhukumu kwa matokeo ya michuano ya Chalenji huku tukiambiwa kuwa tutaletewa bonge la kocha.

Siioni Msumbiji ambayo ingemuondoa Kim katika michuano hii. Katika mfumo wa kawaida wa Kim, Msumbiji ingeteseka tu na yule kiungo wao mtembeaji, Elias Pelembe Domingues, asingetembea sana kama alivyofanya katika mechi hizi mbili.

Ugonjwa mbaya zaidi ni kwamba Stars ipo ili mradi ipo. Wachezaji waliopo baadhi yao wameanza kuchoka, lakini nani mbadala halisi? Kizazi cha akina Samatta kilitengenezwa, kizazi kijacho nani anakitengeneza? Walahu Simba walijitahidi kututengenezea akina Ramadhani Singano, lakini wako wachache.

Tunahitaji kuiokoa Stars kwa kutibu magonjwa yote hayo hapo juu. Tulitaka kukosea kwa kuanza kutibu mabadiliko ya jina la timu wakati magonjwa hayo juu yameilaza Stars kitandani kwa sasa.

Source : Taifa Stars imejilaza ICU inapumulia mashine - Soka - mwanaspoti.co.tz
 
hali mbaya ya ebola siara lion nchi ambaye imepakana na benin na nyie mnaing'ang'ania kucheza na nchi hiyo kwa habari za bbc walitaka kufunga mipaka lakini nchi za magharibi zimekataa kwa maana hiyo siarleon wanaingiliana na benin
 
Alivyosema kocha wa benin kabla ya mechi na t/stars leo saa 11 jioni

Taifa Stars yaivaa Benin

Naye kocha wa Benin, Olle Didier Nicolle alisema wamejiandaa vizuri kushinda mchezo huo na anaamini utakuwa mchezo wa amani na ushindani kwani lengo lake ni kuandaa timu itakayoshiriki mashindano ya Afrika mwaka 2017.

“Nimefurahi kuja Tanzania, sisi ni kama nyinyi, tumekuja kucheza mechi ya kawaida ya kirafiki kwani naandaa timu itakayoshiriki mashindano ya Afrika 2017, nina wachezaji wengi vijana chini ya miaka 20.”

Wadau Je sisi Watanania MALENGO yetu yapi???
 
Alivyosema kocha wa benin kabla ya mechi na t/stars leo saa 11 jioni
Taifa Stars yaivaa Benin

Naye kocha wa Benin, Olle Didier Nicolle alisema wamejiandaa vizuri kushinda mchezo huo na anaamini utakuwa mchezo wa amani na ushindani kwani lengo lake ni kuandaa timu itakayoshiriki mashindano ya Afrika mwaka 2017.

“Nimefurahi kuja Tanzania, sisi ni kama nyinyi, tumekuja kucheza mechi ya kawaida ya kirafiki kwani naandaa timu itakayoshiriki mashindano ya Afrika 2017, nina wachezaji wengi vijana chini ya miaka 20.”

Wadau Je sisi Watanania MALENGO yetu yapi???
 
hongereni taifa star mbinu zaidi ziongezwe pamoja na kupata wachezaji walioenda shule kwani possible wakawa na uwezo wa kufikiri mambo kwa haraka wakiwa uwanjani badala ya kuchuku vijiweni tukumbuke mara ya mwisho tumefanya vizuri katika mashindano ya africa tukiwa na wachezaji walau walio na elimu ya juu kina tenga mtemi ramadhani nk
 
Hivi hii timu ya taifa tuna malengo gani? Yani tunajiandaa kwalipi? Hivi hakuna haja ya kuanza kuwekeza kwenye migogoro let's focus CHAN Mwakani na CAN 2017& 2019 hizi mambo za migogoro hatufiki popote
 
Back
Top Bottom