Tanzania nani wakulaumiwa kuhusu ufisadi

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Me maoni yangu nadhani watz sisi wenyewe ndo tunao uwezo wa kuamua kama jirani zetu RWANDA WALIVYOBAILIKA ingawa kwa nchi kama Tz, wanajamii wengi upeo na uelewa ni mdogo sana. Mfano wanafunzi kukaa kwenye ndoo hizi shule za kata?? Ni kweli pesa ya kutengeneza dawati hamna kweli?/Pia sasa tumekopeshwa Dola billion 400 na IMF jana TBC wamenena?? je hizi pesa kwa haraka haraka zikitumika ipasavyo si Tz tuaenda mbele au ndo maandaliza ya UCHAGUZI 2010.

Pia Wapinzani wenzangu tuungane ili iwe dawa kwa nchi yetu otherwise itakuwa ngumu maana watz wetu wengi hawana upeo kama nchi za Uganda, Kenya na Nyingine nyingi.

Nani anasoma vyombo vya habari?? Nadhani hakuna?? Nani anajua kama chadema walipata kula nyingi mjini huko BUSANDA je tatizo ni vijijin?? Pia TV zetu mbona Kituo kimoja tu ndo kinakemea haya ya wizi wa pesa za UMMA??
Wengine wanahofia ajira zao au wanaogopa kufungiwa???
Mfana ITV wanajitahd kwa kweli, TBC hoi, Ch10 ndo ovyo??, Star tv hawana jipya?? wengine hawapo ni bongo fleva tu?? TV zetu zikielemisha na kutumia muda mwingi kusema watu wanaokinzana na uroho wa pesa za UMMA??

FISADI ni nani?? wewe sio fisadi?? Wangapi wamefanikiwa bila ufisadi?? Wangapi wanataka utajiri wa muda mfupi??

TUISHUKURU ITV na MAGAZETI YA WADAU WANAOUNGA MKONO??
Serikali ilianzisha website ya kutoa maoni Wtz, Je inatumika??
Iligharimu kiasi gani?? Na wangapi wanaijua??

Ukilipwa milion 7 kwa mwezi na ukaanzisha biashara yako ya kwaida tu na ukaweza kuendelee kimaisha na jamaa zako?? Kuna haja ya kuiba tena au kupata rushwa??

JIULIZE???
TOA MAONI YAKO???
 
suala si tuu kupinga ufisadi kwa majabizao kwenye magazeti na television!!! suala ni uwajibikaji wa mtuu mmoja mmojaa...hili linawezekana tukianza mimi na wewe..

kwa nn watoto wakalie ndoo wakati nachangia harusi tshs 50,000 na kuendelea??? kwa nn kijiji changu zahanati haina kifaa cha kuhifadhia maiti wakati nachangia tshs 50,000 kwa harusi ya siku mojaaaaa....TAFAKARIIIIIIIIIIIIIIII...

Pili mimi kama mtumishi wa umma/binafsi nawajibika kiasi gani katika kutoa huduma inayoleta mabadilikoo katika jamii yanguuu?? mathalani maafisa mikopo benki kuwaeleimisha wakopaji matumizi ya mkopo badala ya kudai asante ya hela, watumishi wa umma katika halmashauri, wizara na taasisi katika kuhudumia kwa wakati na haki???? viongozi katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleoo badala ya kuhamasisha posho za vikao na kupewa rushwa kutoa tenda zisizokamilikaaa....???

viongozi kula michango ya wananchi ya maendeleo kama vile ujenzi wa shule, maji, barabara, hospitali, soko, umeme, kanisa, msikiti, gari la ushirika, kudidimiza na hatimaye kuua vyama vya ushirika, wizi wa mbole ya ruzuku, madawa ya mifugo kuuzwa kwa ajili ya ulanguzi, ..........KUTOKUPENDA KUFANYA KAZI NA KUWA MLALAMIKAJI
 
Tatizo sie ni jamii ya "rent seekers" (rushwa, hongo, msaada, mchango, takrima, nk). Ni wachache mno wanaofikiria kuzalisha na kuongeza thamani.

Tukianza kufikiria uzalishaji na kuongeza thamani kwa rasilimali, tutajikuta tunalazimika kuwashinikiza watawala wetu watuwekee mazingira ya kutuwezesha kuzalisha "competitively" ili tuweze kushindana kwenye soko la dunia. Tukifikia hapo, watu wataanza kuwajibika na rushwa itapungua sana.

Hakuna neema itapatikana kwa watu wasiozalisha, kuongeza thamani na kuuza nje. Tutaendelea kubomoana tu kwa rushwa, hongo na ujinga mwingine kama huo (mara nyingi bila kujijua).
 
kwa nn watoto wakalie ndoo wakati nachangia harusi tshs 50,000 na kuendelea??? kwa nn kijiji changu zahanati haina kifaa cha kuhifadhia maiti wakati nachangia tshs 50,000 kwa harusi ya siku mojaaaaa....TAFAKARIIIIIIIIIIIIIIII...

na kwanini nisichangie harusi iwapo kama nilichangiwa katika siku yangu na kwanini nisimchangie mtu wangu akaikumbuka siku yake ya harusi milele we vipi. unazungumza kuhusu hela yangu nilioitolea jasho niitumie vipi wakati kuna serakali ambayo inapata kodi, misaada, na ina miradi mingi mikubwa na kwanini wasitimize huo ndio wajibu. sio warithi wa nchi yetu ni viongozi wetu tulio wachagua kwa kura lakini hawafanyi maadili ya kazi zao na wala hawaya piganii majimbo yao wengi uonekana kwenye kuitajika kura tu na hawajali mwanao anakalia nini.

hivi unadhani jukumu la kujenga taifa ni la nani mbona usiseme unaenda kununua rada wakati watoto wanakalia ndoo, unaenda kununua ndege sijui hela copter wakati atuna adui kwa sasa zinapaki wakati zahanati azina vifaa vya kuifadhia maiti. embu elewa kwenza ni viongozi tuliowachagua waoneshe mifano ndio na sisi tufuatie inapobidi.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Juma,

natumai hukunielewa naamanisha zaidi ulivyoelewaa..na hapo ndipo tunapokosa njia sahihi ya kuwawajibisha viongozi wetu..

nimetumi mifano hai inayonihusu mimi na wewe ili kujenga hamasa ya uwajibikaji miongozi mwetu na kwa jinsi gani tuisimamie serikali..kasema nani wajibu wa serikali ni kuleta maendeleo.. wajibu ni kusimamia maendeleo..

mimi na wewe ndi waleta maendeleo ila twahitaji tuu mipango..kwa kuwa serikali inakosea kwenye kupanga na kusimamia mipango hiyo sisi tuiwajibishe vipi kwa vitendo?? ni kutenda kwa kuleta maendeleo ili tudai usimamizii..huwezi kuchangia zahanati leo halafu viongozi wakaiba vifaa vya ujenzi ukakaa kimya!!! utashi utakusukuma kufanya jambo wewe na wale wote mtakaoguswaa...

WALIPA KODI WAJAPANI WANAGUSWA NA MATATIZO YETU NA KUSAIDIA UJENZI WA BARABARA ZETU AMABAZO HAWAZITUMIIII....TAFAKARIII
 
wakalaumiwa fisadi wenyewe waliojaa serikalini.haiwezekani hela ya kununua madawati kwa wanafunzi haipo lakini hela ya kuibiwa na mafisadi hiwepo.hili swala la ufisadi lilikuwepo na linaendelea kwa kasi kubwa tofauti na wakati wa nyerere kwa vile nyerere alikuwa mkali sana.sema sasa hivi sasa wauni wote wamejikusanya pamoja wamekuwa kundi moja na kuishambulia mali mpaka misaada ya tanzania kwa kasi kubwa sana.swala la ufisadi halitoisha kwa vile serikali inatumia nguvu yake kuwatisha watu amabao wanapinga hili swala.
 
nimetumi mifano hai inayonihusu mimi na wewe ili kujenga hamasa ya uwajibikaji miongozi mwetu na kwa jinsi gani tuisimamie serikali..kasema nani wajibu wa serikali ni kuleta maendeleo.. wajibu ni kusimamia maendeleo..

mkuu mbona unataka kuniacha njia panda basi hou mkopo unaokuja ugawanye mapema, kodi waliokusanya waigawe mapema na faida zote walizonazo wapeleke kwenye majimbo na Taasisi za wilaya watu tuanze kazi kama ni wajibu wetu kwa sababu tuna itaji hela ya taifa na sio mfuko wangu wa jasho langu kupeleka madawati ama nikifanya hivyo ntaumia. wao wakae pembeni wasimamie maendeleo kwani si wajibu wao. au unadhani Bajeti ya bunge ni mchezo kuigiza jamani.

hili ndio tatizo wengi hatujui who is responsible for what but it rarely happens in JF.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Juma,

WALIPA KODI WAJAPANI WANAGUSWA NA MATATIZO YETU NA KUSAIDIA UJENZI WA BARABARA ZETU AMABAZO HAWAZITUMIIII....TAFAKARIII

Gharama kwa Wajapani za kutujengea barabara za msaada ni kiduchu tu ya pato lao la KUTUUZIA magari mtumba.

There's no such thing as a free lunch (msaada).
 
Back
Top Bottom