Tanzania na Utamaduni wa ``Amtaka. Aagiza``

zeus

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
213
55
wana JF kama unafuatlilia kauli za viongozi wetu kuhusu mambo ya msingi ya nchi yetu,
kama vile msimamo wa serikali juu ya rushwa, ufisadi, ajali za barabarani, mafuta, serikali za mitaa, n.k......
utakubaliana na mimi kuwa hawana dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko au hawaamini katika kile wanachosema

mara nyingi utasikia:

Pinda awataka wakurugenzi kuacha ufisadi.......
Waziri awataka wafanyabiaashara kutouza mahindi njee ya nchi
Waziri aagiza majangili waache kuvuna pembe za ndovu.......
Sumatra yawataka wauza mafuta kuacha uchakachuaji......
Igp aagiza madereva daladala kuzingatia sheria.......
Kikwete aapa kuwatoa kafara wala rushwa
...JK aapa kuwatoa kafara wala rushwa
Tamisemi yaagiza kuacha ujenzi holela....HabariLeo | TAMISEMI yaagiza ujenzi holela ukome
hivi kwa nini wasiwachukulie hatua hao wanawaojua kukiuka sheria na taratibu badala ya kuwataka. kwa sababu wanawajua wapo kwa nini wasiwachunguze na kuwachukulia hatua mara moja badala ya kuanza matisho,.Bora tungekuwa tunasikia Pinda wadaka mafisadi, jk aagiza xx achunguzwe au akamatwe kwa rushwa. sumatra yafuta leseni za dalaladala korofi, .....

Very good...dhana ya wao kutumia kauli hizi its a two way traffic; kwa upande mmoja ni kwa kuamini kuwa nchi yetu inaongozwa kwa utawala wa sheria ambapo vitu kama ustaarabu na busara katika kufanya maamuzi vvinapewa nafasi (ingawa kwa sasa ni changamoto),kwa Kuzingatia hilo matamko hayo hutollewa kwa luamini kuwa walengwa watachukua hatua stahili bila kuamrishwa kwa kuzingatia kuwa mkubwa akitoa agizo ni kutekeleza...(orders are not supposed to be discussed) KINYUME chake kwa kipindi hiki kuna watendaji ambao hawajali hayo hivyo kauli za aina hiyo wapewazo na wakuu wao HAWAZITEKELEZI na watoa maagizo HAWAFUATILII kama yametekelezwa. Kwa upande mwingine wa shilingi haya ni matokeo ya mfumo wa 'kuleana" maana unapotoa kauli haitekelezwi lazima umuwajibishe mhusika..kwa mantiki hii kwa sasa mfumo unaofaa ni wa "kuagiza mara moja...kutoa masaa 24 etc ingawa watu wa utawala bora wasema neno) mfano'waziri wa barabara anatoa miezi mitatu barabara fulani iwe imekabidhiwa ikiwa na viwango stahiki..pia anafuatilia kuhakikisha kauli imetekelezwa.Kwa waliokuwepo enzi za mwalimu wanajua wezi wa mali za umma walikuwa wnafanywaje....kufilisiwa maramoja ukibainika,kwa hivo aina hizi za kauli kwa upande mmoja ndo mfumo wa utawala wa kufuata taratibu na haki lakini kwetu sisi ustaarabu huu unakuwa 'mis used' manake watu hawajibiki na viongozi wengi hawathubutu kuuliza chanzo ni "yule kawekwa na nani pale,kimemo etc"
 
Back
Top Bottom