Tanzania Na UK Zatofautiana

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
15
Ni kutokana na Brown kumzuia Mugabe
*Zambia na Ghana nao watoa kauli nzito
*Asipohudhuria mkutano wa marais basi

Na Mobhare Matinyi, New York

TANZANIA kwa mara nyingine imeiunga mkono Zimbabwe ikisema itaungana na Zambia na nchi zingine za Afrika kususia mkutano ujao wa wakuu wa nchi za Ulaya na Afrika utakaoifanyika Desemba nchini Ureno, iwapo Zimbabwe haitaalikwa.

Akizungumza katika mahojiano maalumu wiki iliyopita na mwandishi wa habari hizi jijini hapa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, alisema wazi kuwa kama Zimbabwe haitaalikwa na Tanzania haitahudhuria mkutano huo.

Waziri Membe alikuwa akizungumzia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Zambia, Levy Mwanawasa, kwamba Zambia itasusia mkutano huo iwapo Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe hataalikwa kutokana na mwito wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Gordon Brown.

Bw. Brown hivi karibuni katika kauli yake, alitishia kwamba atasusia mkutano huo Rais Mugabe akihudhuria na kumfanya Rais wa Zambia ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa tamko na msimamo wake hadharani.

"Naamini kwamba kuwapo kwa Rais Mugabe kutaudhalilisha mkutano huo na kusababisha masuala muhimu yaliyopangwa kujadiliwa yasishughulikiwe. Katika mazingira hayo, kuhudhuria kwangu hakutakuwa na maana yoyote," Waziri Mkuu wa Uingereza alikaririwa na gazeti la The Herald la Zimbabwe la Septemba 21 mwaka huu.

Katika kauli yake akikaririwa na vyombo vya habari vya Zambia, Rais Mwanawasa alisema: "Sitakwenda Ureno kama Rais Mugabe hataruhusiwa. Sijui ni viongozi wangapi wa Afrika watakuwa tayari kwenda Ureno bila Mugabe."

Waziri Membe ambaye alifuatana na Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alisema alishitushwa sana kusikia, kwamba kuna tamko limetolewa la kumzuia Rais Mugabe kuhudhuria mkutano huo, huku msimamo ukifahamika siku zote kuwa mkutano huo wa EU-AU hushirikisha viongozi wote wa Afrika bila masharti.

"Tayari tumeiambia Jumuiya ya Kimataifa, kwamba kuitenga Zimbabwe si suluhisho kabisa," alisema Waziri Membe na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kushikilia na kuheshimu Azimio la Accra, lililofikiwa mbale ya marais wa EU, kwamba nchi zote za Afrika hazina budi kuhudhuria mkutano wa Ureno na si vinginevyo.

Waziri alisema nchi wanachama wa SADC watashikilia msimamo aliouonesha Mwenyekiti wao, Rais Mwanawasa na kusema, kwamba SADC inajulikana kwa mshikamano wake kila unapotokea mvutano wa kidiplomasia kama huu.

Akizungumzia kauli ya Bw. Gordon, Waziri Membe alisema: "Wazo kuwa kuwapo kwa Rais Mugabe kutasababisha masuala muhimu yasijadiliwe, halina maana, kwa kweli kutokuwapo kwake kunaweza kukavunja mkutano huo," alisema na kumtaka Waziri Mkuu huyo kumruhusu Rais Mugabe ahudhurie mkutano huo.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) nchi ya Ghana, alimuunga mkono Rais Mugabe, akisema lazima aalikwe kuhudhuria mkutano huo kama kiongozi mwingine yeyote wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Akwasi Osei Adjei, alikaririwa na shirika la habari la kimataifa, akisema: "Naamini tutahudhuria na viongozi wetu wote wa nchi za AU."

Mwenyeji wa mkutano huo hata hivyo alishauponda mwito wa Bw. Brown akisema hauna maana na uliogubikwa na unafiki na kutuma ujumbe kuwa jaribio lolote la kumzuia Rais Mugabe kuhudhuria mkutano huo litapingwa kwa nguvu zote.

Mjumbe wa Ureno katika Bunge la Ulaya, Paolo Casaca, aikaririwa na vyombo vya habari vya Ulaya akimpinga Waziri Mkuu wa Uingereza, kwa kushikilia madai ya uvunjaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe, huku akiwa haoni nchi zingine ambako kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika wazi, tena kila siku.

Mkutano huu wa Desemba ukifanyika utakuwa wa kwanza katika miaka saba kutokana na mingine mingi ya aina hiyo kushindikana, kutokana na Uingereza kukataa kumwalika Rais Mugabe na kusababisha vingozi wengine wa Afrika kuweka msimamo wa pamoja.
 
Waziri Membe alikuwa akizungumzia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Zambia, Levy Mwanawasa, kwamba Zambia itasusia mkutano huo iwapo Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe hataalikwa kutokana na mwito wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Bw. Gordon Brown.

Bw. Brown hivi karibuni katika kauli yake, alitishia kwamba atasusia mkutano huo Rais Mugabe akihudhuria na kumfanya Rais wa Zambia ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutoa tamko na msimamo wake hadharani.

"Naamini kwamba kuwapo kwa Rais Mugabe kutaudhalilisha mkutano huo na kusababisha masuala muhimu yaliyopangwa kujadiliwa yasishughulikiwe. Katika mazingira hayo, kuhudhuria kwangu hakutakuwa na maana yoyote," Waziri Mkuu wa Uingereza alikaririwa na gazeti la The Herald la Zimbabwe la Septemba 21 mwaka huu.

Kwani Mugabe, anatofautiana kipi na viongozi wengi wa Afrika ambao Uingereza inawakumbatia? Halafu yeye ni nani kutuamulia wa-Afrika tukutane na nani na nani tusikutane naye? Huyu kumbe naye hamnazo kama ndugu yake GWB?
 
..Mimi nilifikiri Gordon Brown atakuwa mjanja ktk "kumshughulikia" Mugabe.

..Namna hii Mugabe amepata hoja kwamba Brown anataka kurudisha ukoloni Zimbabwe!
 
Back
Top Bottom