Tanzania na Siasa za kinyumenyume- Tanzania and the Policy of Reverse Governance

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66

  • Badala ya kijenga barabara ili ziweze kupitika, Wananunua magari makubwa (heavy duty vehicles) ili kuwawezesha kupita katika barabara hizo mbovu. Bila kuangalia kuwa kuhudumia magari hayo ni inagharimu kiasi kikubwa sana cha pesa ya wapiga kula. Mfano chukulia gari aina ya Toyota Land Cruiser 4000cc or above, kiasi cha mafuta ambacho gari hili linatumia chukulia mfano kutoka Dar es Salaam mpaka Arusha (One way), kwa safari hiyohiyo mtu atakaye tumia Toyota RAV4 atakwenda na kurudi (round Trip) kwa kiasi kile kile cha mafuta na pengine kubakia na kiasi kidogo cha kuzungukia kilomita kadhaa akishafika. ukiachilia mbali na huduma nyingine kama services za kila mwezi /mwaka za magari haya ambazo nazo zinakwenda kwa karibia uwiano ule ule na gari kama RAV4.


  • Badala ya kusimamia vizuri vyanzo mbali mbali vya mapato na kuhakikisha kuwa zinatumika ipasavyo na katika uwiano unaeleweka, mfano kuboresha huduma za afya, elimu na mishahara na kuhakikisha kunakuwa na uwiano unaokubalika. Hii itasaidia kuboresha maisha ya raia na utawala wa kuheshimu sheria na kwa kiasi kikubwa itasaidia kupunguza uhalifu.


  • Badala yake njia ya kupunguza uhalifu hasa ujambazi, serikali inaona ni kutoa mafunzo na kuajili askari zaidi. Hata uwiano ukiwa askari 1 kwa raia 1 hii kitu haitafanikiwa kupigana dhidi ya uhalifu kama hali ya maisha ya wananchi itandelea kuwa kama ilivyo kwani hata hao askari ni sehemu ya jamii hii pia na machungu ya maisha na wao yanawapata na uozo unaendela wa viongozi na wao wanaona pia. Sana sana itakuwa ni kufunza majambazi zaidi kwani katika matukio ya ujambazi yanatotokea hivi sasa wahusika wakuu ni askari, ukichukua matukio 5 ya uhalifu/ujambazi wa kutumia silaha matukio 3 kati ya hayo askari (ama askari wastaafu) wamehusika moja kwa moja na matukio.

  • Badala ya kurekebisha maisha ya vijijini na kupeleka huduma muhumu ili kupunguza tatizo la vijana wazururaji mijini na wengine kuishia kwenye umachinga badala yake wanaajili mgambo kwa ajili yakukabiliana na wachuuzi hao wa bidhaa ndogondogo na Mama lishe.


  • Badala ya kupima viwanja vingi na kuuza kwa bei ya kawaida kwa raia wote na hatimae watu waweze kununua viwanja hivyo na wajenge kutokana na mipango miji badala yake wanapima vichache na kuviuza kwa bei ya kulinganisha na ile wanayouza watu binafsi. Wanasahau kuwa wao ndio wanatakakiwa wasimamie na kutetea haki ya kila mmoja ya makazi bora yaliyokatika mpangilio badala ya watu wachache tu kusimamia soko hili na kutuwekea bei za ajabu ambazo hauwezi kuziangalia hata mara mbili. Matokea yake kila siku watu wanavamia misitu na kuendelea kujipimia bila mpangilio.


  • Badala ya manispaa kutumia kodi vizuri za wananchi na kubuni namna gani wanaweza kuweka mazingira safi hasa yale ya ufukweni badala yake wanapiga marufuku watu wasitumie maeneo hayo kwa kisingizio kuwa wanayachafua, kuzuia kuogolea ufukweni (beach), ama kuwa maeneo hayo kwa ajili kupunga upepo.


  • Badala ya kusikiliza malalamiko ya wanafunzi hasa wale wa vyuo vya elimu ya juu na kuyafanyia kazi wanapuuzia na wanafunzi wakigoma kudai maslahi hayo, wanaishia kuitiwa polisi na kufukuzwa vyuoni na kisha kupewa masharti ya ajabu ajabu kama kuandika barua ya kujieleza na kuorodhesha majina ya waanzilishi wa mgomo wanasahau madai ya mgomo huo ambao ndio mzizi.


  • Badala ya kufidia wananchi wanaoathirika kutokana na afya zao na maeneo yao kuharibiwa vibaya hasa yale yaliyo katika migodi na wengine kupoteza kazi zao ama kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu, badala yake wanafikiria namna ya kuwalipa fidia watu wachache mabilioni ya shilingi (wawekezaji feki wa migodi hiyo. Mfano KIWIRA).

Kuna mambo mengi sana hawa jamaa wanafanya kinyume na hali halisi.. mnaweza kutoa michango yenu na kuendeleza hiyo list ya REVERSE GOVERNANCE ya serikali yetu...
 
Inasikitisha sana kuendelea kuongozwa na hawa jamaa waliokaa kama mapazia pamoja na kuwa wengine wanaelimu ya hali ya juu, sasa hata umuhimu wa elimu unakuwa ni kama bure kabisa..
 
Back
Top Bottom