Tanzania na siasa ya uchumi na uchumi wa siasa

The Planner

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
357
118
Wanazuoni mbalimbali katika fani ya maendeleo na uchumi wamewahi kuja na theories mbalimbali katika kujaribu kueleza dhana ya kutokuendelea kwa nchi za dunia ya tatu, pia wamejaribu kutoa hatua ambazo wanadhani nchi zilizoendelea zilifuata, Ukimuangalia Marx kwa mfano na watu mbalimbali waliochangia katika Marx theories of social development wanatoa hatua zifuatazo ili kuweza kuendelea,
1. Primitive communalism 2. Feudalism 3. Capitalism 4. Socialism na 5. Communism/Communalism
Tukija kwa economist Rostow, yeye anatupa pia hatua tano ambazo hazina budi kupitiwa katika economic growth
1. Traditional Society 2. Pre-conditions for take off 3. Take-off 4. Drive to maturity and 5. Age of high mass consumption
Ukijaribu kuangalia hizi stages, tunaweza kuzichambua katika msingi wa vitu vitatu yaani:
Stage ya 1. Uchumi unaotegemea kilimo 2. Uchumi unaotegemea viwanda na 3. Uchumi unaotegemea huduma na technolojia

Kwamba ili kuweza kujikomboa hatuna budi kutoka stage moja kwenda nyingine, hapa ndipo tunapokuja kuona mkanganyiko ukilinganisha na hali yetu sisi watanzania. Katika critism za hizi stages zote ukulinganisha na hali ya nchi za Afrika kama Tanzania, hatuoni sisi tuko katika stage ipi. hapa ndipo msingi wa mada yangu unapojengeka kwamba katika hizi stage zote sisi uchumi wetu haujengwi kwa msingi wa kilimo, viwanda au huduma rather tunaweza sema uchumi wetu unajengwa katika kutegemea siasa. Mpaka pale tutakapotoka katika political economy na kujua kitu gani kinachojenga uchumi wetu na kuelekeza resources zetu na commitment zetu huko tutajikomboa, vinginevyo tutazidi kutopea katika ufisadi maana ni hatua mojawapo endelevu katika uchumi uliojaa sanaa za kisiasa
 
mkuu wewe ni bingwa wa DS ..... summary basi bana.... wengine ngwini lilitushinda
 
Back
Top Bottom