Tanzania na mustakabali wa kizazi kijacho

van helsing

Member
Jan 7, 2011
13
0
pindi niliposoma historia ya shule za msingi niliwacheka na kuwaona wapumbavu sana mababu zetu wa enzi hizo waliporubuniwa kwa vitu vitu vya kijinga na kukubali kunyonywa na wakoloni.mfano walipobadilishana gololi kwa dhahabu au shanga kwa pembe za ndovu,au mfano mzuri mkataba alioingia chifu mangungo na wakoloni wa kijerumani
lakini umri uliposonga mbele nilipunguza kidogo kuwadarau na kuwalaumu kwani kidogo walikuwa hawana uelewa wa mambo mengi yaliyoendelea duniani kwa kipindi hicho, labda niseme ukosefu wa elimu nao ulichangia.
Kwa sasa mambo ni tofauti sana, kwani tuna viongozi na watendaji wenye elimu ya kutosha, weye ufahamu wa kutosha kwa kinachoendelea duniani.kuanzia madaktari hadi wanasheria wenye kuheshimika mbele ya jamii, na tunaraisi ambaye si mbumbumbu [mwenye digrii yake moja na nyingine za kuzawadiwa]
Ila naduwazwa na kushangangazwa pindi niyaonapo na kuyasikia matendo yafanywayo na hawa viongozi na watendaji waliosoma kwa kodi zetu, nakereka kuona jinsi wanavyogawana rasilimali zetu bila huruma kwa kuingia kwenye mikataba ya hovyo inayolandana na ya kina CHIFU MANGUNGO, kuanzia walivyo kodisha mbuga zetu na kuuza madini yetu ardhi
shughuli inakuja pindi nifikiriapo wajukuu zetu miaka 100 ijayo, WATAJIVUNIA NINI KUTOKA KWETU au watarithi nini kutoka kwetu, KWANI NAAMINI KWA HALI ILIVYO SASA NA IKIENDELEA KUWA HIVI HIVI, miaka miamoja[100] ijayo tutaambulia matusi na kejeli na majuto ya wajukuu zetu kuzaliwa nasi.watatamani wangezaliwa mbwa uluya kwani nadhani haya ndiyo yatakuwa maisha yao;
Wanyama pori watakuwa wakiwasoma na kuwaona kwenye vitabu na filamu, kwani mbuga zitakuwa zimeuzwa zote na wanyama pori kutoweka [kwa sasa licha ya utajiri na utitiri wa wanyama pori ni watanzania wangapi wameshawahi kuionja nyamapori? ukidakwa unaozea jela,] Na hivi viwanja vya ndege ndani ya mbuga ni vya nini? kama si hujuma za kusafirisha wanyamapori wetu kwenda ughaibuni? Nadhani miaka 100 ijayo wajukuu wetu kwa wale watakaokuwa na uwezo itawabidi wapande pipa kwenda ughaibuni kuwaangalia hao wanyama kwenye ZOO zao, Nadhani watajiuliza,''SI WALIKUWA WETU HAWA? WAMEFIKA FIKAJE HUKU? nadhani watahitimisha kwa kejeli na matusi kwa sisi babu zao
Madini itabidi wayasome kwenye vitabu tu, kwani sidhani kama hata watayakuta makumbusho, nadhani watayakuta mashimo yakiwatamalaki, Natumaini watakuwa na maswali mengi sana, ''mamadini wameyauza, mbona bado tu masikini wa kutupwa? fedha walizipeleka wapi hawa? watahitimisha kwa matusi na kejeli na majuto ya kuwa kwenye kizazi chetu
Nadhani biashara ya utumwa itajirudia upya, kwani natumai miaka 100 ijayo tutakuwa hatuna rasimali tena [madini, wanyama, samaki nk] za kuwashawishi hawa bwana wakubwa kutupatia masaada au mikopo kama wanavyoiita, kwani mimi naamini hizo fedha ni takrima za kuwawezesha kuchota rasilimali zetu. Miaka hiyo watakuwa wamebakiwa na rasilimali watu pekee, hivyo njia pekee ya kupewa misaada itakuwa ni kutumikishwa na hawa mabwana kwa ujira kiduchu
WACHA NIISHIE HAPA KWANI NASIKIA UCHUNGU SANA PINDI NIWAFIKIRIAPO WAJUKUU ZANGU MIAKA 100 IJAYO
NAHITAJI TUOPUKE MATUSI NA KEJELI KUTOKA KWA WAJUKUU ZETU. NCHI ZA UGHAIBUNI ZINA MAENDELEO LEO HII KWA SABABU BABU ZAO WALIWAWEKEA MISINGI MIZURI
NAWAOMBA WANA JF, KWANI NAAMINI WENGI MLIOKO HUMU MNA MNA UCHUNGU NA MAENDELEO YA HII NCHI.

TUFANYE NINI AU TUWEKE MISINGI GANI KUKINUSURU KIZAZI CHA WAJUKUU ZETU, ILI WAJE NAO KUSEMA ''NAJIVUNIA KUZALIWA NA KUWA MTANZANIA'' AMEN
 
Viongozi wetu wanawatukana wahenga wetu walomwaga damu kuifanya jamii yetu huru tena. Wanawalamba miguu waarabu walowauza babu na bibi zetu kama mbuzi sokoni. Hakika tuko pabaya tusipowazindua wajinga waloshika hatamu za uongozi wetu. Sijui tusema 'UTAMU WA UDOKOZI?'
 
Tunahitaji kuwang'oa waabudu tumbo kutoka madarakani, kisha turejeshe nidhamu ktk ofisi za umma. Kwanza tutubu kama taifa kwa kubadilisha katiba, imetusababishia wote kutenda dhambi ya uongo mbele za Mungu. Tunasema tunajenga uchumi wa ujamaa na kujitegemea ili hali tukitenda mambo kinyume, unategemea nini hapo?
Pili tutumie uelewa wetu kuwaelimisha na wengine, mtaani unapoishi tumia dk 10 kwa siku kugawa elimu ya uraia bure kwa wenzio, msikitini, kanisani etc, raia mwema uchangia kuweka madarakani viongozi wabovu nao hufinya elimu kwa watu wao ili waendelee kuwatafuna mchana kweupeeee. Tizama matokeo ya F4 na wingi wa shule zetu za sec kata bila walimu.
Hapo, miaka 100 haitafika tutakuwa yenye neema. Hatuhitaji kujilaumu, tushiriki kupambana na giza mchango wa mtu mmoja waweza kuligeuza taifa, hivyo ndo historia inavyoandikwa. Nawakirisha
 
Back
Top Bottom