Tanzania na Misaada: Tujadili hili...

Naona walio wengi wamekubali kuwa inawezekana Tanzania kuendelea bila misaada. Aidha, waliowengi wanalaumu mfumo wa uongozi wa nchi kuwa ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Tanzania hasa ukizingatia kuwa tunarasilimali za kutosha.

Ni vizuri pia tukatofautisha misaada ya mikopo, sidhani kama kukopa ni tatizo maana kila nchi zinakopa ila tu suala kubwa ni kuwa mkopo huo ni wa nini na unatumika katika nyanya gani.

Hata hivyo imefika wakati sasa watanzania tubadilike kifikra, siyo kweli kwamba maendeleo ya Tanzania yataletwa na serikali, kama tutaendelea kuangalia kwa mtazamo huo nashawishika kusema kuwa bado tutakuwa tunafikiria kijamaa na kuishi kibepari. Mimi ni moja ya wale wanaoamini mabadiliko yanaanzia chini kwa kila mmoja wetu. Kila moja kwa nafasi yake at the micro level aangalie nini anachangia katika maendelo ya nchi, kama ni mkulima, mfugaji, mfanyabishara, fundi n.k fanya self eveluation kuona kama unatumia fursa ulizopewa na mwenyezi Mungu kwa kiwango stahiki.

Ni wakati wa kuacha ushabiki wa kuamka asubuhi na kuanza kwenda kijiweni kuhesabu watu na kuangalia nani katoka na nani au na gari gani au yule ndiye mwenye ile hotel blabla nyingi tu. Bila kuwa na mipango ya kila siku, wiki, mwezi, mwaka etc na kila baada ya muda kuangalia unavyoendelea ni vigumu kujitegemea kwa kuwa kama sisi wananchi tumeshindwa kujitegemea ni dhahiri serikali yetu haiwezi kujitegemea kwa kuwa serikali hiyo inawezeshwa na sisi wenyewe. Ni ukweli uliowazi asilimia kubwa ya wazalendo ambao wamefanikiwa walitumia kila walichonacho kufika hapo walipo, hata kama hawajafanikiwa sana, wapo waliofikia hatua nzuri siyo kwa kuwa uongozi kwao ulikuwa mzuri bali kwa sababu ya kujituma.

Fursa tunazoziona tuzitumie kwa kadri ya uwezo wetu bila kusubiri kuelezwa au kusimamiwa.

Nakubali tunatatizo la uongozi hasa katika ngazi ambazo zinatakiwa kuwa chemchem ya mawazo positive kwa vijana huko kwenye grassroots, viongozi wengi ni watawala hivyo kutumia mabavu muda wote. Tunahitaji viongozi ambao watakaa na vijana na kuwafumbua macho namna ya kutumia hizo fursa zilizopo mbele yao. Ukienda nchi zilizoendelea kiongozi anafurahi kuongoza kijiji/mtaa/ kata/wilaya mabayo ina watu wanaoweza kutumia fursa na kufanya eneo lake kuwa na maendeleo na kila mara watafanya tathmini kuona kila mwaka wako katika nafasi gani au wamechangia kiasi gani katika pato la taifa. Lakini kwetu ni kinyume chake, unakuta watawala wetu huko mikoani, wilayani, tarafa na kata wanakaa madarakani miaka bila kujiuliza katika utawala/uongozi wangu nimefanyia nini wananchi wangu na taifa kwa ujumla.

Kwa hiyo niseme tu micro-level initiatives ndizo zitakazo amua kama Tanzania inaweza kujiendesha biala misaada au la.

Hata hivyo kwa sasa kwa kuwa tumedumazwa na misaada itakuwa ni vigumu katika siku za karibuni kusema tutasimama wenyewe, japokuwa inawezekana ila kutakuwa na machungu ambayo tukiamua hatuhitaji tupiana lawama.

I submit
 
KIla nchi duniani ina mikopo. Kwa kifupi hatuwezi kujiendesha bila mikopo kwakuwa hata Marekani na China wana mikopo.

Mkuu ukiilinganisha Tz na nchi kama China au Marekani unajionyesha ni jinsi gani ulivyo sio mzalendo wa nchi hii ............... ni miaka HAMSINI (50) ya uhuru na hali yenyewe ndio hii ..................... tia maji tia maji, kweli hata mungu hapendi!!!!!!!!
 
Tujaribu kuisoma na kuielewa Mada....
Kukopa sio misaada.. Pia Nchi zilizoendelea zilipiga hatua kwa Mikopo pia,halina ubishi..
Sasa Hapa TZ , kwa Miaka 50 Tumekopa ngapi na tulizokopa zimefanyia nini? na Mikopo mingapi imesha rudishwa?
Ukipata Jibu ,Jilinganishe na hao China na Marekani..
Kama wao wanaendelea kwa Mikopo WHY TZ ISIENDELEE?
Mkuu ukiilinganisha Tz na nchi kama China au Marekani unajionyesha ni jinsi gani ulivyo sio mzalendo wa nchi hii ............... ni miaka HAMSINI (50) ya uhuru na hali yenyewe ndio hii ..................... tia maji tia maji, kweli hata mungu hapendi!!!!!!!!
 
Nafarijika kwa kuilewa hii Mada ,pia unanisaidia kufahamu kua TZ tuna WATU WENYE AKILI TIMAMU NA UELEWA MPANA kama Wewe Mkuu..
Kikubwa ni kwamba, kukosa elimu ya Shule si kukosa elimu ya Maisha na Utambuzi.. Jitoe kuwaelimisha wale walio gizani ambao wanadhani TZ haiwEZI KUJITEGEMEA wakati INAWEZEKANA. Jah Bless u...
Naona walio wengi wamekubali kuwa inawezekana Tanzania kuendelea bila misaada. Aidha, waliowengi wanalaumu mfumo wa uongozi wa nchi kuwa ndiyo kikwazo cha maendeleo ya Tanzania hasa ukizingatia kuwa tunarasilimali za kutosha.

Ni vizuri pia tukatofautisha misaada ya mikopo, sidhani kama kukopa ni tatizo maana kila nchi zinakopa ila tu suala kubwa ni kuwa mkopo huo ni wa nini na unatumika katika nyanya gani.

Hata hivyo imefika wakati sasa watanzania tubadilike kifikra, siyo kweli kwamba maendeleo ya Tanzania yataletwa na serikali, kama tutaendelea kuangalia kwa mtazamo huo nashawishika kusema kuwa bado tutakuwa tunafikiria kijamaa na kuishi kibepari. Mimi ni moja ya wale wanaoamini mabadiliko yanaanzia chini kwa kila mmoja wetu. Kila moja kwa nafasi yake at the micro level aangalie nini anachangia katika maendelo ya nchi, kama ni mkulima, mfugaji, mfanyabishara, fundi n.k fanya self eveluation kuona kama unatumia fursa ulizopewa na mwenyezi Mungu kwa kiwango stahiki.

Ni wakati wa kuacha ushabiki wa kuamka asubuhi na kuanza kwenda kijiweni kuhesabu watu na kuangalia nani katoka na nani au na gari gani au yule ndiye mwenye ile hotel blabla nyingi tu. Bila kuwa na mipango ya kila siku, wiki, mwezi, mwaka etc na kila baada ya muda kuangalia unavyoendelea ni vigumu kujitegemea kwa kuwa kama sisi wananchi tumeshindwa kujitegemea ni dhahiri serikali yetu haiwezi kujitegemea kwa kuwa serikali hiyo inawezeshwa na sisi wenyewe. Ni ukweli uliowazi asilimia kubwa ya wazalendo ambao wamefanikiwa walitumia kila walichonacho kufika hapo walipo, hata kama hawajafanikiwa sana, wapo waliofikia hatua nzuri siyo kwa kuwa uongozi kwao ulikuwa mzuri bali kwa sababu ya kujituma.

Fursa tunazoziona tuzitumie kwa kadri ya uwezo wetu bila kusubiri kuelezwa au kusimamiwa.

Nakubali tunatatizo la uongozi hasa katika ngazi ambazo zinatakiwa kuwa chemchem ya mawazo positive kwa vijana huko kwenye grassroots, viongozi wengi ni watawala hivyo kutumia mabavu muda wote. Tunahitaji viongozi ambao watakaa na vijana na kuwafumbua macho namna ya kutumia hizo fursa zilizopo mbele yao. Ukienda nchi zilizoendelea kiongozi anafurahi kuongoza kijiji/mtaa/ kata/wilaya mabayo ina watu wanaoweza kutumia fursa na kufanya eneo lake kuwa na maendeleo na kila mara watafanya tathmini kuona kila mwaka wako katika nafasi gani au wamechangia kiasi gani katika pato la taifa. Lakini kwetu ni kinyume chake, unakuta watawala wetu huko mikoani, wilayani, tarafa na kata wanakaa madarakani miaka bila kujiuliza katika utawala/uongozi wangu nimefanyia nini wananchi wangu na taifa kwa ujumla.

Kwa hiyo niseme tu micro-level initiatives ndizo zitakazo amua kama Tanzania inaweza kujiendesha biala misaada au la.

Hata hivyo kwa sasa kwa kuwa tumedumazwa na misaada itakuwa ni vigumu katika siku za karibuni kusema tutasimama wenyewe, japokuwa inawezekana ila kutakuwa na machungu ambayo tukiamua hatuhitaji tupiana lawama.

I submit
 
Ukubwa au udogo wa Nchi si tatizo..
Iweje leo tunajilinganisha kwa UKOPAJI na Marekani,Uchina na nchi zingine za Magharibi ambazo ni Kubwa kwa Sq mt za mraba na TZ???
Unataka tujilinganishe na nani kwa Maendeleo tuliyonayo kwa kipindi cha Miaka 50 iliyopita?
Leo Msumbiji iko juu ya Tanzania Kiuchumi na thamani ya Pesa yao iko juu zaidi ya Tshs... Na tambua kwa miaka 15 iliyopita Msumbiji ilikua haitukaribii kabisa..
Sasa kwetu kwanini tuzidi kudidimia na Raslimali tunazo zaidi yao?

upuuzi mtupu hivi ndivyo mnavyodanganywa
 
Tanzania inahitaji tu mabadiliko ya fikra potofu ya utegemezi au kuomba omba kuanzia kwa viongozi hadi raia wa kawaida na kwa muda mfupi mabadiliko yataonekana.
Kajitegemea kunaanzia kwenye mawazo halafu matendo yanafuatia. Kila raia anatakiwa ajue wajibu wake kwake mwenyewe na kwa jamii yake hadi taifa wa kuhakikisha anapambana na vikwazo vinavyomfanya asijitegemee katika mazingira yake, hii ikiwa ni pamoja na kuwajibisha mamlaka dhalimu zinazomkwamisha kwa gharama yoyote ile hata ikigharimu maisha yake kwa faida ya jamii au taifa.
Ni muhimu tuwaelimishe watu wetu, kuanzia watoto kuwa utegemezi siyo mzuri na kwamba mara nyingi unatokana tu na fikra hasi zinazosababisha watu kukosa uthubutu au kuwa waoga na matokeo yake ni umasikini. WOGA NI UMASIKINI.
Mabadiliko ya msingi yanatakiwa katika uwanja wa siasa zaidi kwani utashi wa kisiasa ni muhimu sana katika kubadilisha jamii. Na katika hili la siasa jamii imepotoka kidogo na masahihisho yanatakiwa, kwani tunashuhudia usanii ukichukua nafasi kubwa katika siasa na hii ni hatari kwa jamii na taifa kwa ujumla. Wahenga walisema kuwa Wasanii ni watu wa kutoa burudani kwa jamii na kutokana na saikolojia hawawezi kuwa waamuzi wazuri sana.
Wajibu wa kulinda rasilimali za nchi, kuwatumia wageni kwa faida ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wasitoroshe utajiri wetu kwa kuhakikisha wanaingiza zaidi kuliko kutoa (kuna tuhuma nyingi za watu wenye mamlaka kwenye vyombo vya dola kushirikiana na wageni kutorosha rasilimali), huu ni uasi dhidi ya jamii. tuhuma hizi zinatakiwa kufanyiwa kazi na hatua stahili zichukuliwe haraka.
Kanuni ya msingi ya utajiri ni kulinda mali iliyo ndani, kisha kutafuta nyingine nje kuongezea iliyo ndani. Haihitaji shule kujua hii.

Mkuu..Kwenye RED hapo. BIG UP...
Hilo ndilo somo lililozitoa Gizani Nchi zote zilizoendelea... UMEITENDEA HAKI MADA HII.. Jah Bless u..
 
Maswali mengi kwa wakati mmoja;

Hatuwezi kujiendesha wenyewe hata kidogo. Hata tuwe na utajiri wote wa mfalme Suleiman lakini lazima tutagemea wa nje ya Tanzania.

Hakuna nchi duniani isiyotegemea nchi zingine duniani. Kumbuka dunia ni kama kiwilikwili cha binaadam, huwezi kuwa na kichwa ambacho hakitegemei kubebwa na shingo, na huwezi kuwa na shingo kama hauna kichwa. Haali kadhalika viungo vingine, kila kimoja kinamtegemea mwenzake.

Na hivyo ndivyo ilivyo dunia, hakuna mwenye kujitosheleza kwa kila kitu. Utabaki unawahitaji na wako wanaokuhitaji katika hii dunia.

Leo hii hata uwe nchi tajiri vipi utaujuwaje utajiri wako kama hakuna maskini? na uwe maskini wa mwisho duniani utaujuwaje umaskini wako kama hakuna tajiri?

Being is part and parcel of life. No being No life.

Heshima yako Mkuu ZOMBA..
Swali kwako..
1.Kabla ya TIBA ni kutafuta chanzo cha ugonjwa na nini kilisababisha ugonjwa..
Sasa kama yule uliyemtegemea AGUNDUE TATIZO THEN ATOE TIBA LA TATITZO HILO,
AMESHINDWA KUGUNDUA TATIZO, (
MH.PINDA ALISEMA HAJUI KWANINI TZ NI MASIKINI) UNADHANI ATAWEZA KULIONDOA AU KULITIBIA?
2. TZ imeshagundua ina MATAJIRI wangapi na MASIKINI wangapi?
3. Baada ya Serikali kugundua idadi ya Walionacho na Wasionacho , Imefanya nini kuweka uwiano ulio sawa?Japo kwa kwa kiwango cha 40% Wasionacho na 60% Walionacho?

We need sensible conflicts and possible civil war to have Tanzanian in
full consciousness. Mahubiri, mikutano and the like is useless
kumtengeneza Mtanzania mwenye akili timamu yenye uwezo wa Kujitegemea. Kutanua UFAHAMU NA AKILI YAHITAJI MAUMIVU SI PhD!
Civil war iwe silaha ya mwisho.
Sasa hivi tuanze na wanaoihujumu nchi yetu. Tukimuona fisadi au muhujumu amekaa kihasarahasara iwe Bar au popote, tunapiga kipigo cha mwizi tunamaliza, hii itawatia adabu. Nadhani nchi yetu ikiongozwa kwa nidhamu tutaweza kujitegemea kwa at least 60%
 
Mkuu umeenda DEEP mnoo...
Civil war iwe silaha ya mwisho.
Sasa hivi tuanze na wanaoihujumu nchi yetu. Tukimuona fisadi au muhujumu amekaa kihasarahasara iwe Bar au popote, tunapiga kipigo cha mwizi tunamaliza, hii itawatia adabu. Nadhani nchi yetu ikiongozwa kwa nidhamu tutaweza kujitegemea kwa at least 60%
 
Heshima yako Mkuu ZOMBA..
Swali kwako..
1.Kabla ya TIBA ni kutafuta chanzo cha ugonjwa na nini kilisababisha ugonjwa..
Sasa kama yule uliyemtegemea AGUNDUE TATIZO THEN ATOE TIBA LA TATITZO HILO,
AMESHINDWA KUGUNDUA TATIZO, (
MH.PINDA ALISEMA HAJUI KWANINI TZ NI MASIKINI) UNADHANI ATAWEZA KULIONDOA AU KULITIBIA?
2. TZ imeshagundua ina MATAJIRI wangapi na MASIKINI wangapi?
3. Baada ya Serikali kugundua idadi ya Walionacho na Wasionacho , Imefanya nini kuweka uwiano ulio sawa?Japo kwa kwa kiwango cha 40% Wasionacho na 60% Walionacho?

Naona hauna mazowea ya kujisome na kutafuta ukweli, msome hapa kidogo Paul Sozigwa ujuwe tatizo ni nini:

What were Nyerere's impressions of China when he visited?
Chairman Mao impressed Nyerere very much and the Prime Minister, I forget his name now, impressed him and he marveled, see? The year we went to China, Tanzania was in famine. We got about thirty-thousand tons of maze from the U.S. that year. By that time, we were only fifteen million people. We went to China with one billion and everybody had a full stomach. One billion. Think of it. Why is because they eat everything. Pumpkins, pineapples, anything and they make it a habit to accept everything as food and everybody in China was working. Everybody. You wouldn't go to China, anywhere, Shanghai, anywhere, to find somebody idling. So this is his biggest impress.
He came there very hot about his own people, you see, because there were so many lazy people, particularly the educated ones, the white-collar people. They think you should get a degree, you shouldn't hold a shovel or you should not brush your shoes anymore. So this is the biggest impression and then they were not fools, the Chinese. They were making their own rails and they were engineers, building their own houses, building their own roads, you see. And here we couldn't even make a bridge. So it impressed him that you can have a billion people and put them on a discipline that gets everybody to work and there's food for everyone.

Tanzania was not there yet. It's not even, now. If we don't get the rains this month, we have it.

Source: Heaven on Earth . The Film: Paul Sozigwa Interview | PBS

Kwa mara ya kwanza tumeweza kujenga daraja letu wenyewe wakati wa Kikwete!
 
Zomba.. Nipe Majibu sio Maelezo..
Kwa Mda ule TZ ilikua na Raia Milion 15..
Na vyanzo vingi vya mapato haikua ONPE kama sasa... Lakini pia kumbuka Vita ya Uganda ilituyumbisha kiuchumi hasa,kwasababu hatukua na uzoefu wa kupigana vita baina Nchi kwa Nchi,pia ndio mwanzo tu tulikua Tumepata Uhuru hivyo kwa wakati ule nakiri ilikua bado hatujasimama sana.. So tuzungumzie leo.. Tuna MIIGODI,MADINI,GESI nk, WHY TUBAKI KUA OMBAOMBA? WHY TUAGIZE NJE TOOTHPICK wakati MITI TUNAYO? Chuma tunazalisha WHY SINDANO TUAGIZE NJE?
Naona hauna mazowea ya kujisome na kutafuta ukweli, msome hapa kidogo Paul Sozigwa ujuwe tatizo ni nini:

What were Nyerere's impressions of China when he visited?
Chairman Mao impressed Nyerere very much and the Prime Minister, I forget his name now, impressed him and he marveled, see? The year we went to China, Tanzania was in famine. We got about thirty-thousand tons of maze from the U.S. that year. By that time, we were only fifteen million people. We went to China with one billion and everybody had a full stomach. One billion. Think of it. Why is because they eat everything. Pumpkins, pineapples, anything and they make it a habit to accept everything as food and everybody in China was working. Everybody. You wouldn't go to China, anywhere, Shanghai, anywhere, to find somebody idling. So this is his biggest impress.
He came there very hot about his own people, you see, because there were so many lazy people, particularly the educated ones, the white-collar people. They think you should get a degree, you shouldn't hold a shovel or you should not brush your shoes anymore. So this is the biggest impression and then they were not fools, the Chinese. They were making their own rails and they were engineers, building their own houses, building their own roads, you see. And here we couldn't even make a bridge. So it impressed him that you can have a billion people and put them on a discipline that gets everybody to work and there's food for everyone.

Tanzania was not there yet. It's not even, now. If we don't get the rains this month, we have it.

Source: Heaven on Earth . The Film: Paul Sozigwa Interview | PBS

Kwa mara ya kwanza tumeweza kujenga daraja letu wenyewe wakati wa Kikwete!
 
Tunaweza kuendelea bila utegemezi ,lakini lazima UPUUZI HUU ukomeshwe.rasilimali kibao leo hii 76% ya vijana tz hawana ajira.?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tanzania inaelekea pabaya tena sana.

Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza’ kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.

Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?

Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA......................

Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough’.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa?
 
Ili tanganyika ipate maendeleo makubwa, tunahitaji yafuatayo:-
1. Kuiondoa ccm madarakani na udhaifu wake wote
2. Mafisadi wote waliotajwa katika sekta tofauti tuwafungulie mashtaka na kuwafilisi mali zao zote ili tuendeleze viwanda na miundo msingi mingine
3. Tanganyika in rasilimali nyingi kama vile madini, misitu, ardhi, maji na watu.Ili tuweze kuvifaidi hivi vyote tuvunje mikataba yote dhalimu ya madini,utalii, kilimo,uvuvi, n.k tuwape watanganyika kwa usimamizi madhubuti na tuikatae misada na mikopo kutoka sehemu yeyote ile
4. Tuwaajiri vijana wote wataalam waliomaliza vyuo vikuu kwa kuwapa malengo ambayo ni lazima wayatimize;wasipoyatimiza tuwakate mishahara yao kwa asilimia fulani.
5. Tuhimize kilimo cha kufa na kupona kwa kutoa nyenzo mbadala pamoja na usimamizi thabiti ili tupate chakula cha kutosha kwa mahitaji ya nchi na ziada iuzwe nje
6. Tutumie vizuri tafiti nzuri nyingi zilizofanywa na watanganyika wazalendo ambazo nyingi zinaozea kwenye makabati ya serikali ya sasa
7. Tuondoe kabisa waajiriwa wote wa kigeni katika taasisi zetu zote
Tukifanya haya yote, itatuchukue tu miaka kumi kuwa kama afrika ya kusini.Kama Kagame ameweza kuiendeleza Rwanda ktk kipindi kifupi tu, kwanini sie tulio na rasilimali za kutosha tushindwe?
 
Pamoja mkuu.. Umeitendea HAKI MADA Hii..
Swali kwako, ULISHAWAHI MHOJI MP WAKO KUHUSU USIMAMIZI WA RASLIMALI ZA Eneo LAKO?
Ulisha wai kuhudhuria vikao vya maendeleo ya eneo lenu? Ulihoji matumizi na Mapato ktk eneo lako?
Tunaweza kuendelea bila utegemezi ,lakini lazima UPUUZI HUU ukomeshwe.rasilimali kibao leo hii 76% ya vijana tz hawana ajira.?????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tanzania inaelekea pabaya tena sana.

Tangu kuingia kwa mchezo mchafu wa kikundi cha watu tena wachache kujihudumia na kutafuta utajiri kwa kuwauza wenzao, Tanzania si salama ingawa hakuna milio ya bunduki.

Uliza. Yako wapi mapambano dhidi ya ujambazi, ufisadi (ugamba), biashara ya mihadarati, kurekebisha mikataba ya kijambazi ya uwekezaji ambao ni uchukuaji na uwajibikaji? Si siri.

Kwa sasa Tanzania iko mikononi mwa maharamia tuseme majambazi hasa kiuchumi. Imefikia mahali majambazi yaitwayo wawekezaji yanakuja na kutuibia mchana kweupe kwa kushirikiana na wenzetu waroho wachache tuliwaamini.

Uliza uwekezaji kwenye Shirika la Reli uliishia wapi ilipoingia kampuni ya Kihindi iitwayo RITES?

Mijitu inakuja bila hata senti halafu eti inawekeza kwa kuilazimisha serikali iwape mikopo ili waendeleze mradi! Ni wawekezaji wangapi wanakuja na briefcases zao na makaratasi na kurejea kwao wakiwa na magunia ya dola?

Uliza. Ni wawekezaji wangapi hasa kwenye madini wanamiliki ndege na viwanja binafsi vya ndege wanavyotumia kutoroshea madini yetu bila kukaguliwa?

Ni wangapi wanachafua mazingira na hakuna anayewawajibisha?

Hebu zidi kupiga mbizi kwenye uchafu huu uone mengi. Hakuna ujambazi wa wazi kama unaofanywa na makampuni ya simu kwa sasa.

Wanakuja na kuweka mitambo chakavu halafu wanawatoza Watanzania viwango vya juu vya kutumia simu.

Huwa najiuliza. Inakuwaje kupiga simu, kwa mfano, kutoka Canada kwenda Kenya nitozwe senti tano za dola na Tanzania nitozwe senti 27 za dola kwa dakika?

Wakati viwango vya Kenya ni vidogo, mawasiliano baina ya Kenya, Uganda, Rwanda hata Burundi ni bora na rahisi wakati Tanzania ni utapeli mtupu.

Mtu unapiga simu unaambiwa ongeza salio, mara namba ya simu haipo, mara simu inatumika mara hili mara lile.

Kwanini hatusikii upuuzi huu tunapopiga nchi tulizotaja hapo juu kama hakuna namna?

Ajabu ya maajabu, kila mwaka makampuni ya simu yanabadilisha majina ili kuendelea kufaidi msamaha wa kipuuzi wa kodi.

Angalia mahoteli yenu yanavyobadili majina na wamilki kila baada ya miaka mitano ili kuendelea kufanya biashara bila kulipa kodi. Angalia watu wanavyouziana makampuni waliyookota Tanzania kwa bei ya kutupwa.

Anayebishia hili ajikumbushe Richmond ‘ilijiuza' kwa Dowans kwa bei gani ikilinganishwa na bei ya maandishi tu bila kulipa pesa iliyoianzishia biashara hii hewa.

Leo tunaambiwa kuwa pesa tunayoilipa IPTL, kwa mfano inatosha kununua na kujenga mitambo bora na mikubwa kuliko tunayolipia.

Je, kwanini tunaona kujikomboa ni dhambi wakati tukiabudia maangamizi kama haya ya IPTL na makampuni mengine mengi ya nishati.

Je, hapa hakuna rushwa na ufisadi vya wazi? Je, wahusika hawajulikani? Nani anawagusa wala kuwashughulikia? Tunakwenda wapi?

Imefikia mahali watu wakiuliza ni kwanini uchafu huu unaendelea wakati kuna mamlaka, wanakufa kwenye mazingira ya kutatanisha. Jiulize. Mbunge wetu mmoja alipatwa na nini baada ya kuhoji ni kwanini alikuwa akiona watumiaji wa mihadarati hadharani ambao wangeweza kutuonyesha wanakonunua madawa.

Tufikie mahali tuambiane ukweli bila kuogopana wala kufichana. Bila kufanya hivyo na kubadilika nchi yetu itaishia pabaya.

Ni juzi juzi serikali ya Mali imeangushwa kutokana na hasira za jeshi kushuhudia wauza unga wakiwa ndani ya serikali na serikali isifanye kitu kwa vile wakubwa zake walikuwa wakinufaika na uchafu huu.

Je, sisi tu salama na hawa wauza unga na majambazi wa kiuchumi waliotapakaa nchini mwetu? Je, wananchi wataendelea kugeuzwa mbuzi wa shughuli kila mwaka?

Huwa siachi kusema kuwa Watanzania ni viumbe wa ajabu hata kama hawana mikia au macho kisogoni.

Maana ukiangalia kwa mfano, rasilimali zao zinavyoibiwa, wanavyolanguliwa huduma kama vile umeme, simu na mahitaji mengine na wakaendelea kuvumilia unashangaa hawa ni watu wa namna gani.

Nani kwa mfano anakumbuka na kuhoji ile kashfa ya utoroshaji wanyama iliyotokea Novemba 24, 2010 ambapo ndege ya kijeshi ya Qatar ilifanikiwa kutorosha wanyama mbali mbali 130 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro?

Je, kama KIA wana uwezo wa kutorosha wanyama hai na wengi kiasi hiki wanashindwa nini kuingiza maelfu ya tani za unga?

Ukitaka kujua nini namaanisha, watafute wafanyakazi wadogo na wa kawaida viwanja vya ndege uone walivyo matajiri wa kutupwa.

Unadhani pesa hii wanaipata wapi kama si kuruhusu uchafu na jinai kama ile ya KIA......................

Nenda TRA, Bandari, Uhamiaji. Mambo ni yale yale. Uchafu, uchafu mtupu. Nani anajali iwapo wanaofaidika wameweka watu wao kufanya kazi hiyo? mfano, vituo vyetu vya mipakani vimegeuzwa maduka ya wezi wachache kupitisha wamtakaye na wakitakacho bila kuulizwa na yeyote?

Je, namna hii nchi itakuwa salama? Je, namna hii tunaweza kujisifu kuwa yaliyotokea Mali hayawezi kutokea huko tuendako ambapo wahusika wasiporekebisha hali hii wananchi katika hali yoyote wataamua ‘enough is enough'.

Tumekuwa taifa la hovyo linalowazawadia watenda maovu!

Uliza waliotimuliwa madarakani kwa kashfa wanalipwa pesa ya umma kwa kazi gani zaidi ya kupaswa kuwa mahakamani hata magerezani? Tumegeuka taifa la watenda maovu na waovu kirahisi hivi?

Je, baada ya mchezo huu mchafu Tanzania itabaki nini? Tunaviandalia nini vizazi vijavyo iwapo tunafanya mambo kama mataahira kutokana na kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa?
 
kuna maswali mengi yamekua yanasumbua akili,hasa akili za wenye ufahamu wa juu..
Je!! Kwa nchi ya tanzania inaweza kuendesha shughuli zake bila kutegemea misaada na mikopo toka nchi za nje?

Na endapo unadhani inawezekana tanzania ikaendesha bila huo utegemezi, au haiwezi kuachana na utegemezi..
Toa sababu zako hapa!

Kwanini haiwezi kutegema mikopo na misaada?

Kwanini inaweza kuendesha shughuli zake bila misaada na mikopo?

jibu ni moja tu tuwang'oe ccm wote hadi wajukuu zao kuanzia ikiwezekana vtukuu ndo wapokewe jkt ili wajazwe uzalendo upya kabisa na kila mali ya ccm irud serikalin then mchakato wa kuinua uchum uanze na tutafika tunapotaka!
Tuamke sasa!
 
na tujiulize, iweje tukopeshwe zaidi ikiwa madeni ya mwanzo hatujamaliza kulipa?
Kuna nini kimejificha hapo?
ni kwa sababu wanajua ni jinsi gani watakuja kujilipa,ndio maana wengine wanaamini ipo siku afrika itatawaliwa tena.ukijumlisha na uchumia tumbo wa viongozi wetu misaada haifai,ni aina fulani ya utwana.ila yote kwa yote we need to change our way of leading.nawasilisha.
 
Some time huwa naona kama hii ni mbinu bora zaidi tatizo ni kwamba tukishaingia kwenye civil war tutaichafua sana nchi,ila ili hii nchi ibadilike inahitajika watanzania waelewe kwamba kufa ni sehemu ya maisha.wafe kwa ajili ya nchi yao,kuliko sasa ambapo wengi wetu wamekufa huku wanatembea.wasife kwa ujinga wao.
 
Back
Top Bottom