Tanzania na Misaada: Tujadili hili...

Misaada tunaweza tukaachana nayo hata dakika hii ila sio mikopo, kwani mikopo ina matatizo gani? misaada haitufai kwa sababu inaambatana na nguvu fulani za kuwafumba midomo viongozi wetu kusimamia maslahi ya taifa letu wakati wafanyabiashara kutoka kwa mataifa hisani wanapokuwa na business interests hapa kwetu na states zao pia. mikopo si tunarudisha bwana na sio lazima tukope kutoka ulaya wala america serikali inaweza ikakopa hata hapa hapa nchini.
 
Hongereni wote mliochangia kwa hisia na kumaanisha hapo juu. Mchango wangu huu hapa.
Kuna vitu vya maana na msingi sana ambavyo vikikosekana basi harufu ya kuendelea haiwezi kuwepo kamwe.

1. Ni kufikiri na dhamira ya dhati kufikia hatua fulani. Uwezo wa kufikiri ndio msingi wa ubunifu na kujenga mikakati ya kusonga mbele. Mfano tu, kwa makadirio 90% ya watz wanawaza (wakiwemo viongozi wa nchi) wakati 10% tu wanafikiria. Uwezo wa kufikiri na dhamira hutokeza kwa kutegemea kiwango cha elimu na uchungu wa dhati wa kutokomeza shida za raia wenzako, wangapi humu jf na nchi nzima wana tabia hiyo, (....think about what you can do for your country). Hii ni sifa ambayo watz wengi tumekosa. Viongozi ni mafisadi, self-centered.

2. Kuiga na wivu. Tabia ya kuiga ni nzuri ila inaubaya, je unaiga kitu gani. Watz wengi tunaiga vitu vibaya ambavyo si vya kuonesha nia ya kuendelea. Mfano, wasomi na wajinga wengi huiga mavazi, ufahari km E. Maige anaiga kumiliki hekalu utadhani C. Ronaldo, na umasikini huu wa Watz!

Tunaye mkuu wa nchi anaenda kubembea Marekani, tutaendelea hapo kwa kuiga kubembea? Wahindi wanasifika kwa kuiga vitu vizuri, mfano hardworking, kutengeneza dawa, software na wako mbali.

Nina vitu vingi sana juu ya kujenga Tz inayojitegemea, lakini ukurasa wa jf hautatosha. Kwa ufupi, TABIA (VALUES), ndo nguzo kubwa ya kuendelea. Maliasili zote mlizotaja hapo juu ni kitu kidogo sana kama Rasilimali watu ni ziiiii.

Mwalimu aliliona hili.
TIME, very important. Angalia muda unaopotea kwenye foleni kwenye mabenki, ofisi za Tanesco, hospitali, barabarani foleni tu. JK hawezi ona foleni king'ola kinamsafishia njia barabarani.

UBUNIFU, hapa kuna fedha nyingi sana iwapo mtu utabuni/utagundua kitu (intelectual property rights). Kuna wabunifu waliyowahi jitokeza hapa Tz, serikali haiwathamini. LAKINI tunabuni NGOs ili kupata ulaji na ma-DFP.

Jamani km kweli wewe una uwezo wa kufikiri, great thinker, acha kuwaza bali fikiria. Nitarudi tena baadaye kuendeleza.
 
KIla nchi duniani ina mikopo. Kwa kifupi hatuwezi kujiendesha bila mikopo kwakuwa hata Marekani na China wana mikopo.

Mkuu, Marekani na China wanakopa wapi pesa? Marekani ni chief contributor kule World Bank, UN na IMF.

Unataka kuniambia ile stimulus package ambayo Obama alipewa imetokana na mikopo? Labda useme wanakopa kutoka Federal Reserve.

China sina uhakika kama nao wanakopa kwa mtu, isipokuwa nao serikali ilipewa stimulus package kutoka benki kuu ili iweze kuiingiza kwenye uchumi ambo kidogo umekuwa ukiyumba kwenye miaka ya hivi karibuni.

Lakini hizi nchi mkuu ni kubwa sana kiuchumi kwetu na wakizungumza wana shida si kama shida za kwetu.

Jamani tusitafute sympathy sisi ni nchi tajiri inayoweza kujitosheleza kwa kila kitu tukiwapa watu responsible kutuongoza.
 
Mkuu, samahani kama nitakachochangia kitakuwa kilishasemwa na mwingine, maana si rahisi kusoma michango yote ya wengine i.e great thinkers na none....waliomo katika thread hii. Vinginevyo hutofanya chochote cha maana ktk siku ila kuperuzi JF tu.

Nichukue mfano mmoja tu wa gesi asilia. Nchi ya urusi inatamab ulaya yote na kuitetemesha kwa kuwauzia gesi tu. Ukileta jeuri kama ilivyopata kutokea kwa Ukraine, akafunga bomba wakaanza kulalamika.

Kulingana na taarifa zilizopo japo sitokuwa sahihi, TZ ina hazina ya millions of cubic meters of natural gas ardhini ambazo zikichimbwa na kutumiwa vizuri kwa biashara na maendeleo ya Tz, inaweza kabisa kuiendesha nchi hii kwa miaka hata thelathini na zaidi huku ikiwa imefunga migodi mingine yote (dhahabu, almasi, vito n.k.) kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
 
Tutategemea misaada midogomidogo kwani binadamu hakamiliki 100%
sababu za kutotegemea misaada na mikopo kwa zaidi ya 50%
1.KATIBA MPYA
2.KWANZA WAWEKEZAJI WABANWE KWA KUTENGENEZA MIUNDO BINU ZA SEHEMU HUSIKA (MFANO GEITA[GGM],NYAMONGO[BARRICK],KAHAMA[BARRICK],CHATO[BARRICK] atc KWA KUTENGENEZA SHERIA NA KUSIMAMIA

3.ITENGANISHWE SIASA NA WATAALAM WALIOPO KAZINI
4.MAHAKAMA IWE CHOMBO HURU ZAIDI BILA UTETEZI NA UPENDELEO
5.VIPAO MBELE VYA SERIKALI VIWE VIFUATAVYO:-
i.nishati ii.elimu iii.kilimo na afya.
 
SIMPLE,woooote wanaoshinda hapa JF kutwa nzima kwa kulalamika na kutukana watu wajifunze kutumia muda wao vizuri,i mean,wafanye kazi kwa bidii zaidi!
 
Mkuu, samahani kama nitakachochangia kitakuwa kilishasemwa na mwingine, maana si rahisi kusoma michango yote ya wengine i.e great thinkers na none....waliomo katika thread hii. Vinginevyo hutofanya chochote cha maana ktk siku ila kuperuzi JF tu.

Nichukue mfano mmoja tu wa gesi asilia. Nchi ya urusi inatamab ulaya yote na kuitetemesha kwa kuwauzia gesi tu. Ukileta jeuri kama ilivyopata kutokea kwa Ukraine, akafunga bomba wakaanza kulalamika.

Kulingana na taarifa zilizopo japo sitokuwa sahihi, TZ ina hazina ya millions of cubic meters of natural gas ardhini ambazo zikichimbwa na kutumiwa vizuri kwa biashara na maendeleo ya Tz, inaweza kabisa kuiendesha nchi hii kwa miaka hata thelathini na zaidi huku ikiwa imefunga migodi mingine yote (dhahabu, almasi, vito n.k.) kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Ni kweli kabisa kwa hili hata mie mwenye uelewa mdogo ninaomba nitupie vishilingi vyangu. Ingawa sina uhakika na uwezo wa kujiendesha wenyewe lakini nadhani Watanzania wengi tumelewa na kulemazwa na ule usemi wa sisi ni masikini, watanzania ni masikini, Tanzania ni masikini na ndio maana dhana ya kuwa na rasilimali lukuki na kuendelea kuwa masikini haitokaa ieleweke hata siku moja. Ni sawa na mgeni anapokuja nyumbani kwako na kukukuta umekalia ndoo yenye dhahabu, almasi, tanzanite, gasi you name it, then anakwambia wewe ni masikini nawe unaitikia ndio mimi ni masikini kisha anakwambia nipishe nichukue vilivyomo kwenye hiyo ndoo uloikalia, nikavitengenezee utajiri kisha nije nikugaie kidogo kidogo nawe huyooo unanyanyuka ukimkabidhi ndoo yako tena kwa makofi na vigelegele mkombozi amekuja.

Bahati mbaya ulemavu huu hauko kwa watanzania tu bali pia uongozi mzima, tumelemazwa na ugonjwa wa sisi hatuwezi wala hatufundishiki na ndio maana tunashuhudia kila siku wananchi wakipokonywa ardhi zenye malighafi na kukabidhiwa wageni kwa jina la uwekezaji, tena tukishangilia kuwa watatusaidia kukuza uchumi, for heaven's sake tangu walipoanza kuchukua kwetu wametukuzia nini yarabi?

Hivi ikitokea kule kwenye Tanzanite, serikali iamue tu kuwa hakuna mtanzania atakayehamishwa kumpishga muwekezaji bali kama kuna mwekezaji anayeitaka tanzanite aje ajenge uwezo (ajira, ujuzi na vifaa) kwa kampuni za kizawa kisha wakubaliane bei itashindikana? The same kwenye gold, n.k? Tulishajua kuwa Tanzanite inapatikana kwetu tu tukiwatunishia vifua kuwa wachimbaji watakuwa wazawa (ambao wamewezeshwa) haitafika sokoni? wataigomea?

Mimi sijui siasa but ninawaza tu kwa hii akili yangu ya kiMMU.
 
Ki ukweli, Tanzania tunahitaji miaka 50 ili kujiendesha wenyewe bila misaada!
Kuhusu mikopo, hata USA wanakopa, hivyo Tanzania sidhani kama tunaweza kukwepa kukopa!

Nikirudi kwenye misaada, kutokana na mfumo tulioachiwa na wakoloni (ukoloni mambo leo) ni vigumu sisi kusimama peke yetu kwa kipindi hiki, wengine watadai kuwa tuna resources nyingi ambazo zikitumika vizuri tunaweza kujiendesha bila kutegemea misaada, lakini swali la kujiuliza ni je, vifaa, teknolojia na ujuzi wa kuvuna na kutumia hizo resources tunao?

Jibu ni HAPANA, na ili tuwe na huo uwezo naamini tutahitaji miaka 50! Hii haijalishi ni chama gani kipo madarakani, iwe CCM, CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI, au hata tukikodisha chama cha siasa kutoka nje. etc.

Kitu cha ajabu ni kuwa hata South Africa naye anategemea msaada japo ni kwa asilimia kidogo ukilinganisha na Tanzania!

Tanzania tunauwezo wa kujiendesha/kujitegemea mathalan kwa kutumia sekta ya usafirishaji kwani tunazungukwa na nchi nyingi ambazo hazina bahari hivyo kujipatia revenue ya kutosha kuendesha nchi achilia madini utalii ardhi. technolojia tunazinunua kama zilivyofanya nchi za asia halafu tunaziimprove kufuatana na uhitaji wetu wataalam/skilled tunao
kukopa kwa ajiliya shughuli za kawaida za serikali ni kujimaskinisha zaidi, nchi makini zinakopa kwa ajili ya kuwekeza ktk shughuli za maendeleo ya jamii ambapo deni litajilipa kutokana na matokeo yake. hivyo yunahitaji watu makini wenye nia thabiti tofauti na hivyo hata baada ya miaka 50 bado tutakuwa wategemezi tu
 
angalia record ya sector moja tu, actually we lead in africa yet 3% return with 100% capital allowance and 5yrs grace period on tax

tanzania gold shipments increase to record, diamonds decline


tanzania, which vies with mali to be africa’s third-biggest gold producer, increased shipments of the metal to a record last year as prices climbed.

Exports grew to $1.9 billion from $1.4 billion a year earlier, according to provisional mines ministry data provided by acting commissioner ally samaje. The central bank will release final data later this year. The value of gold shipments rose even as output dropped to 37,000 kilograms (81,571 pounds) from about 40,000 kilograms a year earlier, he said.

“the increase in exports is attributed to higher prices of gold on the international market,” samaje said in an interview in arusha, 330 kilometers (205 miles) north of the capital, dodoma. Apr. 27. Bullion for immediate delivery rose 13 percent to $1,563.70 in london last year.

Tanzania earned 876.3 billion shillings from its gold, silver and copper resources since 1998, when gold mining began in the east african nation. african barrick gold plc (abg) and resolute mining ltd. Own mines in the country. Total receipts from minerals increased to $2 billion last year from $1.5 billion in 2010, generating 2.6 percent of gross domestic product in the region’s second-biggest economy.

Gold production may drop further next year when african barrick’s tulawaka mine and resolute’s golden pride operations are scheduled to be closed, according to samaje.

“in tulawaka, barrick will conclude surface mining next year,” samaje said. “they have an option to go for underground production, or close. We have already given them permit for underground production at tulawaka.”
deo mwanyika, vice president in charge of corporate affairs at african barrick, didn’t answer his mobile phone when bloomberg called three times today seeking comment.

feasibility study

african barrick’s nyanzaga project in sengerema district has yet to produce a feasibility study and the process may take as long as four years before production starts, samaje said.

“the upcoming projects will still take time, which means our ambition of reaching annual production of 50,000 kilograms may not be achieved soon,” he said.

Gold output in tanzania peaked at 48,000 kilograms in 2004, from which the country earned $596 million in shipments, according to the ministry’s data. The other company operating in tanzania is anglogold ashanti ltd. (ang), which owns the geita gold mine, the biggest by output.

Shipments of diamonds dropped to $7.5 million last year, the lowest in 11 years, from $16.3 million in 2010, as output dropped to 28,377 carats from 80,498 carats, the data showed.

“this is because production was stopped at mwandui to rehabilitate the old processing plant,” samaje said.
Shipments of tanzanite dropped to an estimated $22.8 million last year from $25.4 million in 2010, even as production increased 17 percent to 15,000 kilograms (33,000 pounds) in the same period, according to the data.

Silver exports jumped to $11.6 million from $7.7 million, as output fell to 12,000 kilograms from 10,400 kilograms, while copper shipments fell to $30.2 million from $37 million, according to the ministry.

umetisha nakukubali
 
Maswali mengi kwa wakati mmoja;

Hatuwezi kujiendesha wenyewe hata kidogo. Hata tuwe na utajiri wote wa mfalme Suleiman lakini lazima tutagemea wa nje ya Tanzania.

Hakuna nchi duniani isiyotegemea nchi zingine duniani. Kumbuka dunia ni kama kiwilikwili cha binaadam, huwezi kuwa na kichwa ambacho hakitegemei kubebwa na shingo, na huwezi kuwa na shingo kama hauna kichwa. Haali kadhalika viungo vingine, kila kimoja kinamtegemea mwenzake.

Na hivyo ndivyo ilivyo dunia, hakuna mwenye kujitosheleza kwa kila kitu. Utabaki unawahitaji na wako wanaokuhitaji katika hii dunia.

Leo hii hata uwe nchi tajiri vipi utaujuwaje utajiri wako kama hakuna maskini? na uwe maskini wa mwisho duniani utaujuwaje umaskini wako kama hakuna tajiri?

Being is part and parcel of life. No being No life.
 
kiukweli kabisa bado tunatawaliwa kiuchumi,kisiasa,kiutamaduni na kwa sasa hata fikra zetu zilizomzuri zinatumiwa na mabeberu kututawala,kiukweli tunachomiliki ni utu na staa zetu tu ambao nazo kwa sasa zinaendelea kumomonyoka taratibu .Hivyo basi ile dhana kwamba rasirimali zetu,madini yetu,ardhi yetu n.k si vyetu ni urithi wa dunia nzima hasa kwa wale wenye nguvu nyingi,maharifa ya kutosha na wakati mwingine ujanja-ujanja tu.Hivyo basi ili kuendelea kutawaliwa ni sharti misaada itolewe
ili pawepo na fursa nyingine kadha wa kadha za mabeberu hao kuendelea kujizatiti vya kutosha.TUFAHAMU KUWA HAWA WATOA MISAADA HAWAPENDI WATANZANIA KOHOJIHOJI JUU YA DHANA HAPO JUU WAKATI WANASAIDIA BAJETI YETU NA MAMBO MENGI NA TUKIENDELEA KATIKA HAYA IPO SIKU WATATUTAWANYA.CHA MSINGI TUJITAIDI KUFANYA KAZI KWA BIDII NA ILI NCHI ISITEGEMEE MISAADA INABIDI KWANZA FAMILIA ZETU ZIJITOSHELEZE KWA MAHITAJI YAKE MUHIMU.ASANTE MTOA MADA NA WANA JF WOTE.
 
Kuna ted talk moja hivi Bill Gates anazungumzia bajeti, akasema BAJETI zinatengenezwa na watu ambayo uelewa wao katika maswala ya pesa ni mdogo sana na zina matokeo makubwa sana katika sekta zote za nchi na ni pesa nyingi sana.
Alitumia neno scrutiny,, na kusema bajeti na mipango mingi havifanyiwi scrutiny ya kutosha. Huenda kwa mahesabu yake Vasco Da Gama anafikiria anainufaisha nchi yetu,,,,,,kwa kuwa hafanyi scrutiny ya kutosha na hivi hadi leo hii hajui kwa nn TZ bado ni masikini..

Changamoto kubwa ni kwamba tunatakiwa tuwatumie vizuri hawa wanachumi wetu. Mimi nafikiri kuna mambo mengi sana ambayo wanasiasa wetu wanaamua bila kuwa na picha halisi ya kinachoendelea au impact yake in future of the country.
 
KIla nchi duniani ina mikopo. Kwa kifupi hatuwezi kujiendesha bila mikopo kwakuwa hata Marekani na China wana mikopo.
lol! unawaiga? kwa taarifa yako mikopo ya nchi kama marekani sio kama unavyoielea wewe, sio kama ya JK kwenda nje na kuomba pesa! serikali ya marekani haidaiwi, ni makampuni binafsi yanayokopa kwenye mabenki around the world kwa ajili ya bussiness project zao kwa sababu wako global, ila kwa sababu makampuni ni ya kimarekani basi inaeleweka kuwa ni denila marekani! Sio kwamba Obama kaenda kuomba pesa ili serikali yake iweze kujenga barabara!
Nchi kama Russia mbona haina deni kabisaaaaa????????????
 
KIla nchi duniani ina mikopo. Kwa kifupi hatuwezi kujiendesha bila mikopo kwakuwa hata Marekani na China wana mikopo.

Lakini mikopo si mpaka kwenye budget zao, nadhani angalau tujitutumue ifikie 80% ya budget inatoka ndani ya nchi, sie tumezidi ni sawa na mtu anachukua mkopo bank anakwenda kushona suti badala ya kuzalisha ili apate faida arudishe bank alafu mwisho wa siku ananunua suti
 
Tanzania inahitaji tu mabadiliko ya fikra potofu ya utegemezi au kuomba omba kuanzia kwa viongozi hadi raia wa kawaida na kwa muda mfupi mabadiliko yataonekana.
Kajitegemea kunaanzia kwenye mawazo halafu matendo yanafuatia. Kila raia anatakiwa ajue wajibu wake kwake mwenyewe na kwa jamii yake hadi taifa wa kuhakikisha anapambana na vikwazo vinavyomfanya asijitegemee katika mazingira yake, hii ikiwa ni pamoja na kuwajibisha mamlaka dhalimu zinazomkwamisha kwa gharama yoyote ile hata ikigharimu maisha yake kwa faida ya jamii au taifa.
Ni muhimu tuwaelimishe watu wetu, kuanzia watoto kuwa utegemezi siyo mzuri na kwamba mara nyingi unatokana tu na fikra hasi zinazosababisha watu kukosa uthubutu au kuwa waoga na matokeo yake ni umasikini. WOGA NI UMASIKINI.
Mabadiliko ya msingi yanatakiwa katika uwanja wa siasa zaidi kwani utashi wa kisiasa ni muhimu sana katika kubadilisha jamii. Na katika hili la siasa jamii imepotoka kidogo na masahihisho yanatakiwa, kwani tunashuhudia usanii ukichukua nafasi kubwa katika siasa na hii ni hatari kwa jamii na taifa kwa ujumla. Wahenga walisema kuwa Wasanii ni watu wa kutoa burudani kwa jamii na kutokana na saikolojia hawawezi kuwa waamuzi wazuri sana.
Wajibu wa kulinda rasilimali za nchi, kuwatumia wageni kwa faida ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wasitoroshe utajiri wetu kwa kuhakikisha wanaingiza zaidi kuliko kutoa (kuna tuhuma nyingi za watu wenye mamlaka kwenye vyombo vya dola kushirikiana na wageni kutorosha rasilimali), huu ni uasi dhidi ya jamii. tuhuma hizi zinatakiwa kufanyiwa kazi na hatua stahili zichukuliwe haraka.
Kanuni ya msingi ya utajiri ni kulinda mali iliyo ndani, kisha kutafuta nyingine nje kuongezea iliyo ndani. Haihitaji shule kujua hii.
 
KIla nchi duniani ina mikopo. Kwa kifupi hatuwezi kujiendesha bila mikopo kwakuwa hata Marekani na China wana mikopo.
mkuu naona kama umekuwa mtumwa sana wa nchi hizi sioni sababu ya kujilinganisha na nchi hizi kikubwa tuangalie population ya hizi nchi, na resources ndipo uje uangalie nchi yetu inakosa nini kama sio ukilazi wa viongozi wetu tulio wapa dhamana ya kutuongoza na kusimamia mali zetu
 
Back
Top Bottom