Tanzania na Misaada: Tujadili hili...

Hatuhitaji misaada au mikopo
1.Migodi ya madini-dhahabu, tanzanite, almas uranium taja list yote
2.Ardhi-kubwa yenye rutuba
3.Maji-bahari, maziwa makuu, mito, maji chini ya ardhi etc
4.Mlima mrefu zaidi Africa-Kilimanjaro
5.Mbuga za Wanyama-serengeti,ngorongoro,selous, mikumi, momela taja zilizobaki
6.Rasimali watu-takriban watu million 45
7.Hali ya hewa safi
8. Amani na Utulivu
9.Bandari-Tanga, DAR, Lindi, Mtwara, Bagamoyo, Zanzibar etc
Kukiwa na nidhamu na usimamizi wa hayo Tanzania inatakiwa iwe miongoni mwa G8 lakini ufisadi, wizi, ujinga, upumbavu, kukosa uzalenda, ubinafsi tumeshindwa kutumia vyote hivo na sisi ndio ombaomba nambari one Duniani!
 
Mkuu hatupaswi kuchoka, wapo waliokosa elimu darasani lakini kupitia JF YUNIVESTI tutaelimishana na kufunguana akili.... Pamoja tutafika tu,,. Don't gv up Kamanda..
ni kweli lakin huwaga nakasirika akujadili mambo ya serikali yetu na tanzania kwa ujumla manak eyanatia hasira sana.

hivi mkuu kwa kuangalia tu pasi hata kukaa darasani mkoa wa pwani wapaswa kuwa nyuma kimaendeleo kama ulivyo ukicompare na mabonde mazuri waliyonayo tena yenye maji? angalia nazi tu na embe dodo zinazopatikana huku pwani kabla hata ya kuangalia korosho na mabonde kama ruvu na rufiji.

hebu angalia uwekezaji pekee ktk mkoa wa pwani ni vituo vya mafuta na mahotel ambayo mengi yak bagamoyo na haya hayawez kuwa na tija hasa ya ajira kwa vijana wengi, lkn kutwa nzima hakuna la maana zaid ya misafara ya rais kwennda kwake huku akichekelea vituo vya mafuta akasahau mashamba na maji yanayotirirka bure pasi kuwa na tija.stupid kabisa
 
Kenya wama-sign mkataba hivi karibuni na kampuni ya kuchimba mafuta ENI toka Italy na mgawanyo wa profits uko hivi:
78% Govt of Kenya
22% ENI (Investor)

Tanzania kama tungekuwa na viongozi makini, mikataba yote ya madini ingepitiwa upya. Na bado hujaangalia sekta ya mailiasili, na uvuvi. Hela nyingi sana zinapotea na naweza kusema kwa hakika hiyo bajeti ya Tsh 15.1 trillion tusingehitaji hata cent moja toka nje.
 
Mkuu,Tunafanyaje hapo ili tuondokane na KURITHISHA madeni Watoto na vijukuu vyetu?

haiwezi kujiendesha bila mikopo/misaada kwa sababu viongozi walioko madarakani hawana vision ya kuliondoa taifa hili kutoka iliopo sasa na kuipeleka kwenye mafanikio...
wao wameweka matumbo mbele maslahi ya taifa nyuma...
uwezekano wa kujiendesha yenyewe upo, hii itatokea endapo wananchi/umma utakapojua hatua stahiki za kuwachukulia hawa watawala wanaotanguliza mbele matumbo yao badala ya maslahi ya umma...
 
Mkuu Rwanda wameonyesha mabadiliko kwa miaka michache mnoo,
huoni miaka 50 ni mingi sana kwa Taifa lisilo na Majanga na lililo sheheni UTAJIRI WA ASILI?

Tusiilinganishe RWANDA na Tanzania.Rwanda ni nchi ndogo sana.Inaweza kuwa kama mikoa miwili au mitatu mikubwa ya Tanzania.
 
Tudhamirie kuitoa CCM madarakani tuachane na mabogas kama akina Mchemba wanaotetea upuuzi bungeni
 
[hUWA SIPENDI SANA KUJADILI HAYA MKUU LAKINI INANILAZIMU KUJADILI TUU! TATIZO NAPATA UCHUNGU SANA ILA SI ULE WANAOSEMAGE WANACCM TUKAJIFUNGUE!
1. Tuna maziwa na bahali tosha kwa uvuvi
2. tuna ardhi yenye rutuba
3. tuna gas na mito mikubwa inayoweza kutosha kuzalisha umeme
4. tuna bandari ambazo nchi zinazotungunguka hawana
6. tuna ng'ombe wengi sana nikiasi cha kuwafundisha wafugaji namna bora ya ufugaji
7. tuna mawe kibao ya cement tungekuwa tunauziwa bei chee ya 5000 tu.
8. maeneo ya watalii ni mengi sana
9. tuna watu wengi sana tena wenye elimu za kutosha
10. tunamisitu hata kama tungeamua kula kwenye misitu tu tungeishi
11. tuna mawe mazuri kweli ya kutengenezea barabara.
12. sitaki kuzungumzia madini sababu tumeuza yoote
 
Our country has none to rank with in the world, hatuwezi kataa kua misaada hasa ukizingatia ni 3rd world nation. Ila kama kutakua na usimamizi wa lasilimali za Tanzania kwa manufaa ya Tanzania basi tulistahili kua na Deficit Budget kwa mwongo mmoja tu (MIAKA 10) na mingine kuweza kulipa madeni yale na hata kuwakopesha nchi wahisani pindi wakienda vitani( They love war games).

Kwa mfano, madini pekee output kwa 2011 ilikua $ 1.9 Billion ambapo ni asilimia 19% ya budget ya 2012/13 ($ 10 Billion). Hapa sijazungumzia sekta ya Utaliina maliasili, Foregn Direct Investments(FDI), Kilimo na mengine mengi tuliojaliwa kama Tanzania.

Kumbuka pia kodi ya TRA inatenemea VAT na wachuuzi wa biashara za kawaida au wengine hupenda kuwaita SOLE PROPREATORS na wafanyakazi katika mishahara yao. Makampuni makubwa hukwepa kodi na yanajulikana na hakuna ataethubutu kuhoji juu ya hilo. Achilia mbali misamaha ya kodi kila kukicha.......

Mi nadhani TANZANIA should have been the self-fulfilled surplus BUDGET if we delete our vision of Copy and paste from poor countries with a hope phrase "Even other countries have deficity budgets with finance from WAHISANI".
 
tusiilinganishe rwanda na tanzania.rwanda ni nchi ndogo sana.inaweza kuwa kama mikoa miwili au mitatu mikubwa ya tanzania.

hili jinga linatoka wapi tena vp zanzibar???
Ni nchi kubwa sana ndo maana inashindwa kuendelea.
Hizi akili za kimagamba basi gaweni nchi hii iwe ndogo kwanini mnang'ang'ania muungano kama nchi ikiwa ndogo ndo inaendelea!???
 
Mkuu,Tunafanyaje hapo ili tuondokane na KURITHISHA madeni Watoto na vijukuu vyetu?

nafikiri wananchi tuamke na tuwe na utaratibu wa kubadili uongozi kadri iwezekanavyo...
hii itasaidia kwani kiongozi atakuwa anajua akifanya tofauti na matakwa ya umma atawajibishwa na umma huo huo uliompatia hiyo dhamana...
 
Tanzania tunaweza kujiendesha iwapo tutaiondoa CCM madarakani.
Hii ndio suluisho kamili,kuiondoa CCM ambacho ni chama cha kulindana.Kulindana ni tatizo kubwa ambalo rasilimali za nchi
zinapotea kama tupo kwenye shamba la bibi...inatia huruma.
 
Ki ukweli, Tanzania tunahitaji miaka 50 ili kujiendesha wenyewe bila misaada!
Kuhusu mikopo, hata USA wanakopa, hivyo Tanzania sidhani kama tunaweza kukwepa kukopa!

Nikirudi kwenye misaada, kutokana na mfumo tulioachiwa na wakoloni (ukoloni mambo leo) ni vigumu sisi kusimama peke yetu kwa kipindi hiki, wengine watadai kuwa tuna resources nyingi ambazo zikitumika vizuri tunaweza kujiendesha bila kutegemea misaada, lakini swali la kujiuliza ni je, vifaa, teknolojia na ujuzi wa kuvuna na kutumia hizo resources tunao?

Jibu ni HAPANA, na ili tuwe na huo uwezo naamini tutahitaji miaka 50! Hii haijalishi ni chama gani kipo madarakani, iwe CCM, CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI, au hata tukikodisha chama cha siasa kutoka nje. etc.

Kitu cha ajabu ni kuwa hata South Africa naye anategemea msaada japo ni kwa asilimia kidogo ukilinganisha na Tanzania!

Watu mnachnganya mambo, tofautisha misaada na mikopo. Mikopo hata nchi kubwa zinakopa kwa ajilia ya kufanya mambo makubwa zaidi na zina uwezo wa kurudisha bila shida. Misaada ni kitu kingine.

Halafu angalia Tz hata ikikopa huwa inarudisha au inarudishaje? Mara nyingi haiwezi kurudisha kwa sababu ya management mbaya, wizi etc., kinachotokea ni kuwaruhusu wahisani wachukue rasilimali bure kama fidia. Kitu cha kwanza iondoke CCM kwanza ndio tujue what next.
 
Ki ukweli, Tanzania tunahitaji miaka 50 ili kujiendesha wenyewe bila misaada!
Kuhusu mikopo, hata USA wanakopa, hivyo Tanzania sidhani kama tunaweza kukwepa kukopa!

Nikirudi kwenye misaada, kutokana na mfumo tulioachiwa na wakoloni (ukoloni mambo leo) ni vigumu sisi kusimama peke yetu kwa kipindi hiki, wengine watadai kuwa tuna resources nyingi ambazo zikitumika vizuri tunaweza kujiendesha bila kutegemea misaada, lakini swali la kujiuliza ni je, vifaa, teknolojia na ujuzi wa kuvuna na kutumia hizo resources tunao?

Jibu ni HAPANA, na ili tuwe na huo uwezo naamini tutahitaji miaka 50! Hii haijalishi ni chama gani kipo madarakani, iwe CCM, CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI, au hata tukikodisha chama cha siasa kutoka nje. etc.

Kitu cha ajabu ni kuwa hata South Africa naye anategemea msaada japo ni kwa asilimia kidogo ukilinganisha na Tanzania!
Tukizungumzia swala la technology tunahitaji hiyo miaka ambayo umeitaja lakini sisi kinachosumbua hata km na wenzetu wanakopa sisi tumezidi kwa mfn bajeti yetu haiendi bila wafadhili wenzetu km kenya wamewezaje kupunguza kiwango cha utegemezi?
Huhitaji teknolojia yoyote kusimamia mapato mfano ya bandari il kuweza kupunguza vimemo kutoka juu vikiwaelekeza TRA kuacha kumfatilia mfanyabiashara mkubwa ili asilipe kodi inayostahili. Ndo maana Rais Kagame yeye aliwahi kusema anahitaji kupewa bandari pekee kwenye nchi km ya kwetu wala hahitaji madini na vitu vingine kuinua uchumi wa nchi.
Kikubwa kinachosumbua ni kukosekana kwa uzalendo kwa viongozi na kukalia kujilimbikizia mali hivyo kuwafundisha na watendaji wa serikali kufanya hivyo hivyo ndo maana kila kukicha utasikis fulani kaficha trioni kadhaa nje ya nchi.Mfn km sasa inavyosemekana kuna km trilioni 16 nje ya nchi, bajeti yetu ya maendeleo ambayo kwa hakika inategemea wafadhili kwa mwaka huu wa 2012/2013 ni Tsh trilioni 3 haihitaji kuwa umesoma mpaka chuo kikuu kujua hapa kuna tatizo maana hata wakuu wa nchi hakuna hata mmoja ambaye anaujasiri wa kutuambia anafanya nini ili kurejesha hii mali iliyoibwa.
 
Unadhani Mimi na Wewe tunawezaje kuzinusuru raslimali zetu dhidi ya Wanyonyaji?
NA NDIO MAANA TUNAFUATA MATAKWA YAO KILE WANACHOSEMA UMEMSAHAU DAVID CAMEROON,UMESAHAU WANAVYOUTAKA MJI WA KIGAMBONI NA WAMEPEWA BWEREREEEEE,KWANI WATANZANIA HAWATAKI KUISHI SEHEMU NZURIIIII.nikuu ya mbunge wa kigamboni
 
Hapo ndipo shaka yangu ipo.. IWEJE TUPEWE MIKOPO na MISAADA wakati MIKOPO YA AWALI HATUJAILIPA?

Watu mnachnganya mambo, tofautisha misaada na mikopo. Mikopo hata nchi kubwa zinakopa kwa ajilia ya kufanya mambo makubwa zaidi na zina uwezo wa kurudisha bila shida. Misaada ni kitu kingine.

Halafu angalia Tz hata ikikopa huwa inarudisha au inarudishaje? Mara nyingi haiwezi kurudisha kwa sababu ya management mbaya, wizi etc., kinachotokea ni kuwaruhusu wahisani wachukue rasilimali bure kama fidia. Kitu cha kwanza iondoke CCM kwanza ndio tujue what next.
 
unadhani mimi na wewe tunawezaje kuzinusuru raslimali zetu dhidi ya wanyonyaji?
ndugu yangu hii nchi bila nguvu ya umma as individual kupigania hivi vitu ukijitokeza tu tutakukuta mabwepande kaka.hivyo.tukipata viongozi wenye kujali maslahi ya umma tutafanikiwa kwa kiasi flani japo si 100%.pia mapinduzi ya chama tawala yatasaidia sana ,tukiiondoa ssem madarakani tunaweza faulu hata kwa 65%
 
Kuna maswali mengi yamekua yanasumbua Akili,hasa akili za wenye ufahamu wa juu..
Je!! Kwa Nchi ya Tanzania inaweza kuendesha shughuli zake bila kutegemea misaada na mikopo toka Nchi za nje?

Na endapo unadhani inawezekana Tanzania ikaendesha bila huo utegemezi, au haiwezi kuachana na utegemezi..
TOA SABABU ZAKO HAPA!

Kwanini haiwezi kutegema Mikopo na misaada?

Kwanini inaweza kuendesha shughuli zake bila misaada na mikopo?

Nichangia lakini sijui kama nikotimamu,maana thead hii imetusi watu,badirisha heading mkuu. WENYE AKILI TIMAM TU!
 
ndugu yangu hii nchi bila nguvu ya umma as individual kupigania hivi vitu ukijitokeza tu tutakukuta mabwepande kaka.hivyo.tukipata viongozi wenye kujali maslahi ya umma tutafanikiwa kwa kiasi flani japo si 100%.pia mapinduzi ya chama tawala yatasaidia sana ,tukiiondoa ssem madarakani tunaweza faulu hata kwa 65%

Vipi kwenye Jimbo lako,Ulishawahi kuhoji kuhusu maendeleo yenu kwa MP wako?
Na ulishahudhuria japo kikao kimoja cha kiongoji?
 
Back
Top Bottom