Tanzania moja bei ya sukari toka Sh. 1,700 hadi 2,500

Wana jf wakati tuko kwenye sakata la Jairo jana nilienda kununua sukari kuulizia bei nikaambiwa badala ya 98,000/- kwa mfuko nikaambiwa ni sh. 105,000/- nikasema basi nitanunua kesho yaani leo kuulizia bei nikaambiwa mfuko wa kg 50 ni sh. 115,000/- kuulizia kg 1 maduka ya rejareja nikaambiwa sh. 2,500/- sijui tunaelekea wapi au tutaacha kunywa
 
Wana jf wakati tuko kwenye sakata la Jairo jana nilienda kununua sukari kuulizia bei nikaambiwa badala ya sh. 98,000/- kwa kg 50 nikaambiwa ni sh. 105,000/- nikasema basi nitanunua kesho yaani leo kuulizia bei nikaambiwa mfuko wa kg 50 ni sh. 115,000/- kuulizia kg 1 maduka ya rejareja nikaambiwa sh. 2,500/- sijui tunaelekea wapi au tutaacha kunywa chai.
 
Baada ya kikao cha Bunge usishangae kilo ya sukari ikafika 3000/=
 
Hakuna kitakachoachwa, kwani sukari ilipokuwa mfuko Tsh senti 50(Tshs 0.50) tulikuwa na uwezo wa kununua makontena? Ni wazi tulikuwa na uwezo wa kununua kile tu cha kuweza kutumia. Je ilipofika Tshs 200 kwa mfuko wa kilo 50, au ilipofika baadaye 10,000/- kwa mfuko si tulioona bei imekuwa mbaya? Daima tukilinganisha na nyuma. Vivyohivyo kwa bidhaa nyingine adimu kama dieseli. Kwa mfano miaka 10 iliyopita lita ya diesel ilikuwa kati ya tsh 250- 320, miaka mitano baadaye??? Na leo miaka 10 imepita? Je kuna kitu kinaachwa kwasababu ya ongezeko hilo la bei?
Kwa ujumla utafutaji unaongezwa. Kwa serikali makini mishahara inapanda, ruzuku inaongezwa kwenye bidhaa za kilimo, n.k na kwa sababu hiyo daima mlaji haumii sana hata kama kuna badiliko la bei.
 
Asante Mungu kwa kutuharakishia ukombozi wa kweli. Kwa hili maandamano hayaepukiki na Jk ataondoka ikulu kwa nguvu ya umma. Kikwete ameshindwa kuongoza nchi
 
Unafuata mgao wa Kitimoto. Wale wapenda kitimoto wanunue cha kutosha wahifadhi kwenye mafridge yao au wakaushe kwa moshi!
asante kwa taarifa na njia ya kutunza maana matumizt ya frigde kwa tanzania ni magumu kwani hatuna umeme
 
Back
Top Bottom