Tanzania kupeleka majeshi Zimbabwe

Wana JF, aina yetu ya watu ndiyo inayotuponza katika kupambanua mambo mengi.

Kwanza, Huyo muulizaji kwa nini aliuliza hatua ya kusaidia kijeshi wakati huu ambapo hata matokeo ya kura hayajatangazwa? Hilo halikuwa swali la msingi kwa wakati huu. Kwa mfano, kwa nini asingeilza jitihada zinazofanywa na mwenyekiti wa AU katika hali tete ya sasa huko Harare, akakimibilia jeshi?

Pili, Pinda hakujibu straight kama ambavyo mada ina suggest. Amesema :

* Suala la Zimbabwe kweli ni complex issue kwa sasa. Akafafanua kidogo.
* Kwa msaada`wowote, lazima ifike mahali msaada unaombwa, lakini kama hujaombwa msaada, huwezi kukurupuka tu na kwenda, bila kuangalia hali halisi.
*Mwisho akasema ikiwa utahitajika msaada, basi utaweza kupatikana.

Analytically, jibu la swali hili laweza kuwa baya kulingana na positioning ya mind ya muulizaji. Lakini a simple analysis show that suala la majeshi halipo na haliwezekani kwa sasa ambapo hata kikao cha kwanza cha kimataifa juu ya kusuluhisha hili hakijafanyika.

Pinda anajua kuwa SADC wanakaa keshokutwa, asingeweza kuzungumzia majeshi...likewise, ningekuwa Zitto nisingemuuliza swali irrelevant vile kwa wakati huu, kabla sijamuuliza juu ya nini kinafanywa na nchi za SADC kuhakikisha kuwa hali haizidi kuwa mbaya Zimbabwe.

If it appears the PM is a war monger, so is the Zittos. /SIZE]
 
Hapana hapa pana mbinu za kuwaweka watu bize ,wamekuja na vita vya Comoro ,wamekuja na kuvunja muwafaka sasa wanatafuta la Zimbabwe ,hivi hamuoni hawa watu wanababaisha huku na kule wakivuta mida ili watu wasiamke na hoja ya kudai KATIBA mpya ili mafisadi waendelee kutesa na kufanya mbinu za hapa na pale ili wavuke haya maskendo yaliozagaa nje nje ,maana gea wanayotaka kuondokea nayo CUF si mchezo kuanzia jumamosi mpaka liamba ni Chama cha Wanaume hicho ambacho kimeanza harakati baada ya kuwawacha CCM wakiwaita kwenye meza haraka ili wazungumze ,mnajua kuwa CCM wanafikiri haya wanayoyafanya mapolisi na majeshi wanayapenda maana hata katika usalama wa Taifa kuna watu wamechoshwa na wizi na ufisadi wa watu hawa ,kuna jamaa walisikia wakisema siku likitokea fujo ndio CCM watajua kama hata kwenye majeshi na polisi kuna wapinzani ,kumbe na wao wahoi bin taabani ,hizi trip za kuwapeleka huku na kule wamekwisha zisitukia.
 
Ishu ya Zim mtu pekee ambaye nadhani angeiweza kidiplomasia ni the late JK, sio huyu Vasco bali mwalimu. Otherwise mambo ni mabaya maana jamaa wa chama tawala wako tayari kwa lolote kuensure upinzani haukamati nchi. Kwenye matokeo ya ubunge ZANU PF wanadai majimbo mengine zaidi matano jumla 21 kwamba recount ifanyike. Na kwa historia ya hawa jamaa watachukua kwa nguvu majimbo hata kumi na tano kuretain majority.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom