TANZANIA KUNA MAMBO: DPP amkana Hoseah asema hajapata jalada la Chenge

Watu mna kazi kweli.. hivi si imewahi kusemwa kuna undugu kati ya Feleshi na Chenge? which automatically should disqualify Feleshi kuona, na kufuatilia hili..
Ni mimi niliyeandika hapa wiki tatu zilizopita kuwa Hosea wa Takukuru na Chenge wanatoka eneo moja huko usukumani. Mtu moja akanijibu kwa kejeli kuwa "hatutizami personalities tunatizama issues." Sasa kaongezeka Feleshi ni ndugu na msukumavilevile. Na tiyari hata kabla hajaliona faili kesha sema "Chenge ashitakiwe kwa kosa gani?" Unategemea lipi hapa?
 
Hii movie itakuwa ya ajabu na based on true story......si umeona trela inavyosisismua??? beliieve me kutakuwa na viini macho!!! the good thing ni kwamba katika hili hakuna neutrality ni kusuka au kunyoa, kushtaki au la na historia itawahukumu.
Hivi huyu DPP akienda kuulizia pale masjala Ofisini kwake akaambiwa Jalada limefika tangu majuzi atasemaje? Na hizo comment za "acheni siasa" atazimemeaje? Watu wengine we acha tu!
 
Na DPP akisema hakuna ushahidi ndiyo kesi imekwisha hakuna kwa kukata rufaa au kupeleka malalamiko tena.
Kwa hili unataka kutuaminisha kwamba DPP yupo juu ya sheria maana, kama ushahidi upo na hata akipinga, bado tunawatu ambao wanaweza kumfungulia kesi, vinginevyo tuamini kwamba CCM yote ipo juu ya sheria za nchi..
 
Tazizo la nchi hii linaanzia hapa. Mambo ya kiuongozi yanafanyika kibinafsi badala ya kitaasisi. Kama hosea kapeleka file ofisi ya DPP sijaona tatizo, but tatizo ni kwa Director mwenyewe kutaka apelekewe file yeye binafsi kama Feleshi! Hii ni HATARI, kama sivyo ni usanii mwingine
 
Hapa sasa naona wakati umefika kumtambua nani chui na nani kondoo..serikali ya chama cha magamba wao wanaamini kwmaba, kuliko kumpoteza mtu mmoja kama chenge awajibishwe mahakamani ni bora Watanzania milioni 40 waendelee kuumia kila siku..Serikali haitaki kuwajibisha watendaji wake, hata kama ikionyesha nia basi huwa kuna order zinatoka mamlaka za juu kukataza kutimiza malengo hayo..kwa mfano huu wa DPP kujidai haelewi ni nini kinachoendelea hapa, anatafuta mda wa kukaa na mzee wa kaya waongee pamoja na chenge akiwepo then watamua wacheze sinema gani ili kutupumbaza sisi wananchi...cha msingi hapa tuing'oe ccm madarakani tu
 
Hosea na dpp msituchanganye watanzani na msitufanye wote sisi ni watoto wadogo. watanzania tunataka kujua jalada hili la chenge lipo wapi kati ya hosea na dpp, tena mtujulishe watanzania kinachoendelea kuhusu suala hili.

Ni haki yetu watz kujulishwa kinachoendelea kuhusu suala hili. Mwache ubabaishaji na dhamana mlizopewa kwa ajili ya watz wote...............na hata mkijichanganya namna gani ipo siku wala si mbali ukweli utajulikana tu.
 
Sometime tunakuwa na hope sana na maswala mengi tusioyajua mfano ni hii position ya Dr Hoseah PCCB. Wengi tumeshaona Dr Hoseah anapoteza muda wake na kama alishaona amefeli kufanya hii kazi au kuna tatizo ambalo tunalijua mpaka sasa ni kikwete mwenyewe. Kwanini Hoseah asiondoke na kuendelea kupambana na njia za kuikomboa taifa kwa namna nyingine politically. Myself I have issue na Hoseah, I know you are working surrounded with criminals but you to do something to prove that you are doing something for us. This is your legacy and time had already expired, most of us we think you already becoming one of them too...
 
Mada hii imesababisha nijiunge ingawa nilikuwepo enzi za jamboforums mwaka 2006.
Katika nchi zilizotawaliwa na mwingeleza na kufuata mfumo wa uingereza. Mfumo wa utoaji haki katika criminal justice system kuna chombo cha upelelezi,chombo cha uendeshaji mashtaka na chombo cha kufanya uamuzi au kutoa hukumu.
Hoseah PCCB ni chombo cha upelelezi akimaliza kupeleleza ana mpelekea DPP ambaye ni chombo cha uendeshaji mashtaka. Naye DPP ana madaraka kisheria kusoma ushahidi ulioletwa na chombo cha upelelezi na kutathimini ushahidi kama unatosheleza kama hautoshelezi halazimiki kupeleka mahakamani ambacho ni chombo cha uamuzi. Kwa hiyo kwa Hoseah kuongea na wanahabari kuwa amempelekea DPP kesi apeleke mahakamani kisheria ni makosa DPP anapeleka mahakamani kesi ambayo anaona inaushahidi. Hoseah kuzungumuza aliyozungumza ni kama kulazimisha DPP apeleke mahakamani na asipopeleka kwa sababu ya ushahidi mbovu aliompelekea DPP aseme mnaona nimepeleka lakini hajapeleka mahakamani DPP anakwamisha kesi za ufisadi ili wananchi wamwone Hoseah ni mzuri wakati ni bogus hajui kupeleleza.
 
Hakuna asiejua sasa mh rais ana wakati mgumu si katika baraza la mawaziri tu kama mh mbowe alivyosema bali ni kila sekta alioweka watuwake pengine hili ni fundisho kwa rais ajaye akiweka watuwake akifikiri wataficha mauchafu wote la hasha kuna ambao mungu amewatenga kwa ajili ya uongozi ili wachafu fulan waondoke
sipendi kwenda mbli malumbano ya sasa kati ya dk hosea na dpp yamenifanya nijiulize wako serikali moja ya kikwete
na kama kweli je nani mkweli na huyo mkweli kwa nini asije na copy yake adharani kuonyesha alituma siku fulan saa fulani watu waliosaini hawa wamepokea..mh hosea sipendi kukupinga ila haya mambo ukiweka hadharan utasaidia jamii kujua upuuzi na uchafu alioficha mh huyu dpp aliemsaidia sana mh wetu kuingia madarakani

ni wakati wa kuwatumikia wananchi na mungu awalipe mnachofanya acheni kutumikia mabwana wawili mh dpp hiki nilishawahi kusema pale mwanza mkiwa na akina masha na kundi kadhaa wakati mkijifaidisha sipndi kuweka wazi lakini nilisema kama mtakumbuka ipo siku watanzania watabadilika na kujua jinsi gan ya kudai haki zao na hili litaanzia kwenye serikali humo humo ..majuzi mbowe katoa wazo baraza livunjwe jamaa anaona aibu akifanya hivyo itasemwa mbowe alisema bila kuangalia madhaa yake

leo ni dpp felesh na hosea wapi rais huyu anatupeleka watanzania??
 
Pengine niseme ni mgongano wa maslahi na kama kweli feleshi ujapokea la chenge tuambie hayo 50 aliosema hosea kwa waandishi wa habari na semina za bunge tueleze umempa mkeo??na kama una biashara ya kuuza maandazi tuweke wazi kila mtu anakula urefu wakamba yake pengine mafaili ya kina rostam na chenge waliokuweka hapo umefungia maandazi na je unalipa tra kwenye biashara yako...ni vigumu kuamini mh kama wewe unauliza chenge ashtakiwe kwa kosa gani kwanza ningekuwa mimimwandishi ningekutukana alafu nikuombe m samaha alafu ukirudi dar nikwambie huna adabu hata kidogo na katika waliotakiwa kuchapwa bakora 12 ukiingia 12 ukamwonyeshe mkeo wewe unmgekuwa mmoja wapo pengine this time unachapwa na hela za mafisadi njoo sasa uone watu walivyojipnga kwenda mahakamani na ushahidi uone upuuzi unaoendeleakulea na madhara yake
 
Hii nayo ni senema mpya baada zile za Rostam na Riz1 sijui kafia wapi baada kashfa yake ya lori 100 zilizo mgodini,twamsubiri 2016 ajibu hizi tuhuma upya!!sasa hawa FEM (Feleshi,Edward na Manumba) wanatuanzishia senema mpya inaitwa karata tatu
 
Nilisema hapa jamvini juzi kuwa Chenge ni msukuma,Hosea ni msukuma, DPP Eliezer Feleshi ni msukuma na DCI Manumba ni msukuma, sarakasi mnazoziona ni mkakati mahsusi waliopanga hawa watu kumvua kitanzi Chenge kupitia mahakama.
 
hawa nao washakua kama mapacha duh! Hawafanyi maamuzi magumu kulingana na nafasi zao kabisa!
 
Napenda kuchangia hii mada; na kabla sijaendelea niseme kwamba simtetei mtu yeyote kati ya Fereshi na Dr. Hosea, na wala sihusiani kwa namna yoyote na waziri wa nishati na madini, na isitoshe majina yetu hayafanani kila mtu ana la kwake.

Kwa kuangalia jinsi utendaji kazi wa ofisi yoyote ile na hasa katika uchukuaji, utunzanji na usambazaji wa nyaraka mbalimbali kama vile barua za kiofisi, mafaili au makabrasha ya aina yoyote ile, kuna mifumo na taratibu katika kila ofisi. Na ndio maana kuna masijara ya wazi na masijara ya siri na idara husika kwa ajili ya kushughulika na vitu hivi. Nyaraka inapofika ofisini kwanza inasajiriwa na kisha anapelekewa ofisa yeyote ambaye anaweza kushughulikia jambo lenyewe. Kwa "case" hii ya DPP, hapa tujue ni ofisi ya mwendesha mashitaka, na si kila faili linalopelekwa kwa DPP lazima lishughulikiwe na DPP mwenyewe, kuna wanasheria wa serikali katika ofisi hiyo ambao wanaweza kabisha kufanya upitiaji wa awali kabla jambo halijapelekwa kwa DPP mwenyewe kwa uamuzi wa mwisho.

Ninachomaanisha hapa ni kwamba, Mkuu wa TAKUKURU anaposema amepeleka faili kwa DPP ni kweli anaweza kuwa kapeleka, na likapelekwa kwa ofisa yeyote ndani ya ofisi ya DPP kushughulikiwa kutegemeana na utaratibu ulivyowekwa ndani ya ofisi yenyewe ya DPP. DPP akisema hajaliona, haina maana kwamba Hosea kasema uongo, wala si kwamba Fereshi kasema uongo, anachomaanisha pengine ni kwamba bado halijafika mezani kwake yeye kama DPP, lakini bado linaweza kuwa liko katika ofisi yake kwa ofisa mwingine, na sidhani kwamba kila faili linalofika masijara lazima ajulishwe kwamba kuna faili fulani limefika, ila litapelekwa kwake kwa utaratibu wa kiofisi uliowekwa.

Pengine kwa kuwa DPP alikuwa safari Arusha, ingetosha kusema kwamba hayuko ofisini kwa hiyo hayuko katika nafasi ya kueleza kama limefika katika ofisi yake, au angeomba muda ili apate nafasi ya kuwasiliana na maafisa wa ofisi yake kuthibitisha kama faili kweli limepokelewa au la. Lakini pia hawa wakuu wa hizi taasisi za serikali, ninadhani wanaweza kuwasiliana wao kwa wao kuweka sawa mambo kama haya badala ya kurumbana kwenye vyombo vya habari ambapo wakati mwingine unaweza kunukuliwa vibaya au yale uliyoongea na mwandishi wa habari yakapotoshwa kwa makusudi kabisa.
 
Back
Top Bottom